Ninaacha Ualimu tangu leo

Ninaacha Ualimu tangu leo

Ndio maamuzi niliayoamua na hapa nafanya mpango kukusanya vyangu huku nilipo, najua life litazonga ila kipimo cha akili ni ugumu wa maisha, ipo siku nitatoka tu. Siwezi kuwa mtumwa kamwe.

Nilisimamia mitihani ya kidato cha pili, mtihani umeisha hatukulipwa hadi jana, jana watu wanalipwa nakuja kufatilia pesa yangu naambiwa jina langu halipo, leo nimuone afisa elimu, namuona leo anasema hakuna fungu nilisahaulika niandike Barua kufungua madai nitalipwa kwa OC (other chages) mafungu ya mkurugenzi.

Tafsiri yake ni kuwa limeshakuwa deni tayari hili, jasho langu, kila siku nilitumia tsh 8000 kwenda na kurudi kusimamia mitihani kwa siku saba. Kuja hapa halimashauri kutoka nnakoishi nakodi pikipiki elf 8 kwenda na kurudi kila siku, hapo bado kula, Nimetumia pesa eti leo nidai tena. HAPANA

Tangu nimeanza kazi nna miaka mitatu sasa ninaidai serikali, alafu leo niongeze tena kudai?

Kwa dhati ya moyo wangu nimeamua na sirudi nyuma, nimeachana na ualimu Rasmi, siwez kuwa mtumwa kwa haki yangu. Nita fight, nitatoka, sio wote wenye kazi ndio wanamudu maisha .

Mkuu kama ni kweli nakuunga miguu maana umeanza safari njema sana.

Sisi wengine hatuajiriki kwa kuchukia utumwa unaotokana na kuajiriwa.

Bravo only kama ni kweli maana bila kuvuja jasho huwezi kutoka
 
Mkuu usiondoke mikono mitupu. Wakope milioni kadhaa uache wajilipe wenyewe.
 
Huku halmashauri ya mji Masasi tuliosimamia mtihani wa kidato cha NNE tulipata partial payment, hadi Leo hatujalipwa Siku zilizobakia. Nadhani majipu haya ya uzembe na dharau yatumbuliwe pia
 
Mkuu mkwanza nakupa hongera kwa hatua uliyoichukua.

Ualimu wa Tz ni ukichaa,kazi utafanya weee ila maslahi utayapata kwa kusota.

Maafisa elimu wengi wao ni vichwa maji,wababe,wasiojua wajibu wao wala majukumu yao. Wao ni ngono tu na rushwa zisizokuwa na vichwa wala mkia.

Ukiwa mwalimu utaishia kudharaulika mbele ya jamii yako inayokuzunguka,wanafunzi wako na kila mtu( hata serikali inadharau walimu-nadhani mliona alichokuwa akifanya kikwete na kushangiliwa na wazee wa Dar ambao mimi niliwaona ni wahuni tu).

Zamani ualimu ulikuwa ni kazi ya heshima sana,utapendwa na jamii yote na kuheshimiwa na wanafunzi wako,hali ilishabadilika kitambo sana- leo wazazi wanawachukia walimu,wanafunzi wanawadharau walimu wao na kuwaona maskini wasiojiweza,watu wasio na kipato chakueleweka,waganga njaa na maadui wao! Hakuna upendo tena.
Serikali imewatupa walimu,inawadharau,inawachonganisha na jamii,mfano mkuu wa mkoa anaweza akawatangazia wazazi wasilipe mchango wa mlinzi kwakuwa ni jukumu la serikali,alafu mkurugenzi na afisa elimu wakagoma kutoa mshahara wa mlinzi wakitaka wananchi( haohao waliotangaziwa na mkuu wa mkoa wasilipe- ndio walipe)?

Mwalimu ni yatima kiukweli maana hata hiyo CWT ni ya makada wa CCM,ukiwa kiongozi wa CWT msimamia haki kwa walimu basi utajuta,utavalishwa kila aina ya ubaya na majungu.....

Binafsi niliamua kuacha ualimu mara tu baada ya matokeo yaliyoirudisha CCM madarakani mwaka huu,na niliweka uzi wangu humu jukwaani,nitarudi baada ya miaka minne kutoa ushuhuda wangu wa mafaniko niliyoyapata nje ya ualimu.

NB:- Ajira usiyoifurahia ni utumwa grade A.

Mkuu umeandika ukweli sana, walimu ni kazi ya kwanza inayokunyima status, fursa na kila kitu. Kuna watu humu wana ajira zinawapa hata exposure lkn ualimu ni zero.

True story.
Mwaka huu mwezi wa sita nilikaa counselling na mwanafunzi wa kidato cha nne kumuweka sawa ili asikate tamaa ya mtihani. Nikamwambia maisha ya sasa inahtaji watu wenye elimu.

Kwa mshangao alinambia, mwalimu wewe umesoma lakn mbona maisha yako ya kawaida sana, na kuna walimu kibao mtaani wanakopa pesa kila siku kwa watu wasiosoma na wengine wamewafundisha hapahapa. Nilizuga kwa trick kadhaa lkn hii kauli ilibaki moyoni mwangu mpk leo.

Hapo ndio utajua kazi ya ualimu, yani mwanafunzi hana cha kujifunza kwako zaidi ya content mnayo share. Lkn kwenye maisha hana cha ku imitate.
 
usichukue maamuzi ya hasira.afisa elimu sio alpha na omega.fuatilia ngazi za juu zaidi.
 
Njoo Dar, kama hauna aiba na sii mvivu fasta unatoka.
 
majaliwa, mama sita, magufuli, mwanri wangekomaa na ualimu leo hii wangekuwa hawana hata bajaj, Hongera mkuu kwa kukataa kuwa mtumwa
 
Ndio maamuzi niliayoamua na hapa nafanya mpango kukusanya vyangu huku nilipo, najua life litazonga ila kipimo cha akili ni ugumu wa maisha, ipo siku nitatoka tu. Siwezi kuwa mtumwa kamwe.

Nilisimamia mitihani ya kidato cha pili, mtihani umeisha hatukulipwa hadi jana, jana watu wanalipwa nakuja kufatilia pesa yangu naambiwa jina langu halipo, leo nimuone afisa elimu, namuona leo anasema hakuna fungu nilisahaulika niandike Barua kufungua madai nitalipwa kwa OC (other chages) mafungu ya mkurugenzi.

Tafsiri yake ni kuwa limeshakuwa deni tayari hili, jasho langu, kila siku nilitumia tsh 8000 kwenda na kurudi kusimamia mitihani kwa siku saba. Kuja hapa halimashauri kutoka nnakoishi nakodi pikipiki elf 8 kwenda na kurudi kila siku, hapo bado kula, Nimetumia pesa eti leo nidai tena. HAPANA

Tangu nimeanza kazi nna miaka mitatu sasa ninaidai serikali, alafu leo niongeze tena kudai?

Kwa dhati ya moyo wangu nimeamua na sirudi nyuma, nimeachana na ualimu Rasmi, siwez kuwa mtumwa kwa haki yangu. Nita fight, nitatoka, sio wote wenye kazi ndio wanamudu maisha .

Pole sana Dumelang , natamani kama Magufuli angesoma hili bandiko lako!
 
Last edited by a moderator:
Moja ya ethics za ualimu ni, ualimu ni wito, naona wakati wanafundisha hukuwepo.
 
Ndio maamuzi niliayoamua na hapa nafanya mpango kukusanya vyangu huku nilipo, najua life litazonga ila kipimo cha akili ni ugumu wa maisha, ipo siku nitatoka tu. Siwezi kuwa mtumwa kamwe.

Nilisimamia mitihani ya kidato cha pili, mtihani umeisha hatukulipwa hadi jana, jana watu wanalipwa nakuja kufatilia pesa yangu naambiwa jina langu halipo, leo nimuone afisa elimu, namuona leo anasema hakuna fungu nilisahaulika niandike Barua kufungua madai nitalipwa kwa OC (other chages) mafungu ya mkurugenzi.

Tafsiri yake ni kuwa limeshakuwa deni tayari hili, jasho langu, kila siku nilitumia tsh 8000 kwenda na kurudi kusimamia mitihani kwa siku saba. Kuja hapa halimashauri kutoka nnakoishi nakodi pikipiki elf 8 kwenda na kurudi kila siku, hapo bado kula, Nimetumia pesa eti leo nidai tena. HAPANA

Tangu nimeanza kazi nna miaka mitatu sasa ninaidai serikali, alafu leo niongeze tena kudai?

Kwa dhati ya moyo wangu nimeamua na sirudi nyuma, nimeachana na ualimu Rasmi, siwez kuwa mtumwa kwa haki yangu. Nita fight, nitatoka, sio wote wenye kazi ndio wanamudu maisha .

Hasira Hasara!!!
 
Pole ndugu kweli inasikitisha ni uonevu wa mtu asiyetaka kupeleka majina tu mbele

Mungu akufungulie mema na kukupa furaha
 
Je ukija huku mtaani ukapata kazi ingine...say ukajiajiri...na ikatokea issue kama hiyo unamdai mtu anakuzingua...utafanyaje??
 
Nashauri uombe likizo isiyo na mslipo badala ya kuacha kabisa, kakae uswahilini hata miaka miwili, ukishindwa kabisa rudi kazini kwako!
Nimependa wazo lako..... Asiache kwa pupa, aombe likizo,
 
Mkuu sirudi nyuma, kabla ya kuwa mwalimu mie nilikuwa fighter kitaa na nilikuwa silali njaa. Siwezi kuwa mtumwa kwa haki yangu kabisa nnayohistahili.

Mkuu tusikilize,

ile ile pesa unayoidai unitumie kama mtaji. bado kaz unaihitaji. kataa kata kata kufanya hizo kaz, tenga muda ufanye yako
 
Taja hyo halmashauri,mkurugenzi na wale wote waliokusumbua unaweza pata msaada hapa jukwaani maana wengine wapo humu kazi yao ni kutafta majipu yalipo na kumuonesha mkamuaji"
 
Huku unapokuja ni pagumu zaidi ya huko unakotoka. Tatizo sio tatizo ila tatizo ni uwezo wako wa kutatua tatizo! Komaa dogo hlo ni tatzo dogo sana kukufanya uache kazi labda kama umepata kazi nyingne
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom