Mkuu sirudi nyuma, kabla ya kuwa mwalimu mie nilikuwa fighter kitaa na nilikuwa silali njaa. Siwezi kuwa mtumwa kwa haki yangu kabisa nnayohistahili.
Mkuu mkwanza nakupa hongera kwa hatua uliyoichukua.
Ualimu wa Tz ni ukichaa,kazi utafanya weee ila maslahi utayapata kwa kusota.
Maafisa elimu wengi wao ni vichwa maji,wababe,wasiojua wajibu wao wala majukumu yao. Wao ni ngono tu na rushwa zisizokuwa na vichwa wala mkia.
Ukiwa mwalimu utaishia kudharaulika mbele ya jamii yako inayokuzunguka,wanafunzi wako na kila mtu( hata serikali inadharau walimu-nadhani mliona alichokuwa akifanya kikwete na kushangiliwa na wazee wa Dar ambao mimi niliwaona ni wahuni tu).
Zamani ualimu ulikuwa ni kazi ya heshima sana,utapendwa na jamii yote na kuheshimiwa na wanafunzi wako,hali ilishabadilika kitambo sana- leo wazazi wanawachukia walimu,wanafunzi wanawadharau walimu wao na kuwaona maskini wasiojiweza,watu wasio na kipato chakueleweka,waganga njaa na maadui wao! Hakuna upendo tena.
Serikali imewatupa walimu,inawadharau,inawachonganisha na jamii,mfano mkuu wa mkoa anaweza akawatangazia wazazi wasilipe mchango wa mlinzi kwakuwa ni jukumu la serikali,alafu mkurugenzi na afisa elimu wakagoma kutoa mshahara wa mlinzi wakitaka wananchi( haohao waliotangaziwa na mkuu wa mkoa wasilipe- ndio walipe)?
Mwalimu ni yatima kiukweli maana hata hiyo CWT ni ya makada wa CCM,ukiwa kiongozi wa CWT msimamia haki kwa walimu basi utajuta,utavalishwa kila aina ya ubaya na majungu.....
Binafsi niliamua kuacha ualimu mara tu baada ya matokeo yaliyoirudisha CCM madarakani mwaka huu,na niliweka uzi wangu humu jukwaani,nitarudi baada ya miaka minne kutoa ushuhuda wangu wa mafaniko niliyoyapata nje ya ualimu.
NB:- Ajira usiyoifurahia ni utumwa grade A.