Nina miaka mitano sijala UGALI

Sawa kabisa,huenda miili iliyojazwa ugali imejengeka bila kwenda gym kwa kazi ya mituringa ya kubeba maboksi.
 
Nipo site na wana hapa wamelizungusha tunapiga.
Nyie nao mnakulaje ugali wa makapi? Huo ndio ugali ambao ni useless sasa, ugali ambao mahindi yake hayana kiini.

Bila shaka mtakuwa ni watu wa dar nyie.
 
Kwa sasa nimetimiza miaka mitano bila kula chakula aina ya ugali.

Kuhusu faida ni nyingi Sana mpaka sasa.

Nitazielezea Ila faida kubwa ni kuwa na mwili ambao umejengeka vizuri bila hata kwenda Gym.


"Niliwahidi tisheti nimeleta sijaleta "?
Ndio maana udumavu wa akili ni mkubwa sana Africa hasa nchi za kusini mwa jangwa la sahara, haya mahindi yanatakiwa kuchunguzwa vizuri.
 
Jaman watu tumetofautiana sana, hiv vyakula vingne nitakula ila bila ugali hamna kitu, nikila ugali nahisi nimekula chakula mwili unakua mkakamavu, ila sijui viazi, tambi, mihogo, wali, chips, hamna kitu mwili unakua lelemama
Mazoea na imani tu, unaweza kutoka hapo ulipo ukaenda kuishi sehemu hakuna access na vyakula ulivyozea na kuishi bila huo ugali. Chakula is more mental, unaweza kuwa na njaa usipofikiria chakula wala haikusumbui na ukiwa na imani unashiba kama huna hata ujaze tumbo vipi hautaridhika mpaka ule kile unachokiamini
 
Mazoea ndiyo mtihani!

Watu tunapiga hizo ndizi,tambi etc halafu tunakazia na nguna ili walau tuende 4hrs full tank.

Hayo makolokolo mengine njaa baada ya nusu saa tu halafu wala mtu hufanyi kazi ngumu.
 
Kwa sasa nimetimiza miaka mitano bila kula chakula aina ya ugali.

Kuhusu faida ni nyingi Sana mpaka sasa.

Nitazielezea Ila faida kubwa ni kuwa na mwili ambao umejengeka vizuri bila hata kwenda Gym.


"Niliwahidi tisheti nimeleta sijaleta "?
Uliwezaje EMBU nambie ulikua unakula nini? Mimi na Cha kujifunza hapa.
 
Uliwezaje EMBU nambie ulikua unakula nini? Mimi na Cha kujifunza hapa.
Mimi naenda hivi
Asubuhi


Chai ya rangi, bila sukari wala asali


Smoothie mix ya yogurt, ndizi mbivu, avocado, tende, korosho au karanga mbichi na mayai 2 ya kuchemsha

Mchana

Viazi vitamu/ maboga,/mihogo/ndizi mzuzu/mshale na samaki au kuku, maharage/ njegere na mboga za majani

Jioni
Chai rangi, matunda, korosho

Jtatu na Alhamis : fasting

Daku: saa11 alfajiri chai rangi na tende 5-7pcs
Iftar Jioni: samaki/kuku/maharage/njegere/ na mihogo/viazi vitamu/boga/ndizi mzuzu na tende


NB: naishi jirani na ofisi kwa hiyo muda mwingi nakula nyumbani
Pilau/Biriani kwa sikukuu tu kama kuna ulazima
 
Nimeipenda Sana ndugu Ila kwa sisi wasukuma tumezoea ugali ,wali , nyama,samaki, dagaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…