Nina mashaka na huyu mwanamke

Nina mashaka na huyu mwanamke

Habari wana bodi.

Hii ni mara yangu ya kwanza kuandika kwenye jukwaa hili, japo kuwa ni mshiriki mzuri wa kusoma na kutoa maoni kwenye mada mbalimbali jukwaani. Leo kuna kitu ningependa kuwashirikisha, pengine kuna wajuvi wa mambo ambao watanisaidia vema.

Nipo kwenye mahusiano na binti mmoja mwenyeji wa mikoa ya Kanda ya Ziwa. Ni muda wa mwaka sasa nipo naye kwenye mahusiano haya. Tumekuwa na wakati mzuri sana, japo mikwaruzano ya hapa na pale haikosekani ila sio mikubwa sana kuleta taharuki.

Kitu ambacho nakiona na najifunza kutoka kwa mwenzangu ni utayari wake wa kutaka kuolewa. Tokea mwezi wa sita mwaka huu yeye habari zake ni mahala pa kufanyia harusi, gharama za ukumbi na chakula, wangapi waje kwa harusi n.k.
Mbaya zaidi, karibia rafiki zake wote wameolewa na nimekuwa napata shinikizo kutoka kwa wenzake kwa njia zisizo za moja kwa moja.

Binafsi, sipo tayari kwa mahusiano ya ndoa kwa hivi karibuni. Ila mpango wa kufunga nae ndoa upo kwa zaidi ya asilimia 50. Shida inakuja kwa upande wa mwenzangu kulazimisha, kuwa karibu na ndugu zangu, hata kunitambulisha kwa watu wazito wa mkoani hapa.

Kilichonifanya niandike uzi huu, ni jambo lililotokea na kulishuhudia binafsi asubuhi hii. Mara nyingi, huwa akiwa amekuja nitembelea kwangu basi huwa tunaenda kuoga pamoja kila mara, iwe asubuhi au jioni au hata baada ya chakula adhimu.

Ila leo asubuhi mwenzangu akaenda oga peke yake. Wakati anaoga, nilienda taratibu kwa lengo la kujumuika naye ila nikasema ngoja nijibanze ili nimfanyie utani wa kumshtua, michezo ya hapa na pale. Mlango wa bafu ulikuwa wazi, nikaweza mtazama alichokuwa anafanya. Mwenzangu alianza kujisafisha sehem zake za siri akawa anarudia rudia mara nyingi kuliko kawaida na jambo la kushangaza, ule mkono aliokuwa anajisafishia akaudumbukiza kwenye ndoo ya maji ambayo niligundua alikuwa amenitengea nije kuoga.

Tokea asubuhi tukio hili limenifikirisha sana na kunifanya kuanza kumtazama tofauti mwenzangu. Sio kwa ubaya ila wasiwasi unanifanya niwaze zaidi.

Nje ya jambo hili, huwa tunasali pamoja na kushirikiana mambo kadha wa kadha ya sala. Ila hili la leo limenishtua mno na kunikosesha amani.

Kwa wajuvi wa mambo, je kuna haja ya mimi kuwa na wasiwasi juu ya tukio hili au nifunike kombe mambo yaendelee?

Nawasilisha.
limbwata unalolisikiaga redioni ni hilo sasa.
 
Mpaka kuoana kuna asilimia hahaha acha mpigwe juju tu maana huwezi mpotezea muda mpendwa wa watu akajiaminisha kwa kila mtu kesho na kesho kutwa unaenda kuoa kijijini kwenu.
 
Kuna muda nawaza sawa sawa na jinsi ulivyosema hapa.
Kwa sababu umeshamuona anachofanya basi limbwata lake halitafanya kazi tena. We endelea kujilia mema ya nchi.

Kingine cha muhimu, mpaka hapo umeshamjua hana uvumilivu. Nyakati kama hizo ndizo huwa nzuri kumjua mwenzio uvumilivu wake ukoje. Kwa dalili hizi huko mbeleni mkipatwa na magumu basi hatasita kufanya mambo tofauti na unavyotegemea.
 
mkuu ukifuatilia matendo ya binadam yeyote kwa siri ni rahisi sana kujawa na hofu akat kumbe hakuna kibaya au ubaya wowote anaoufanya, kumbuka kila binadam ana utahira fulani ambao mara nyingi huudhihirisha akiwa pekee
 
Nimeweka asilimia kuonesha uwezekano wa mimi kufanya hivyo. Chini ya 50, maana yake sina mpango huo wa kufanya hilo jambo. Zaidi ya hapo kuna uwezekano.

Sio kupotezeana muda, maana kama hali ndio hivyo basi hata mimi napoteza muda. Halafu ndoa ni makubaliano ya wote wawili na sio kila mahusiano lazima yaishie kwenye Ndoa. Siku zote naamini hivyo.
Mpaka kuoana kuna asilimia hahaha acha mpigwe juju tu maana huwezi mpotezea muda mpendwa wa watu akajiaminisha kwa kila mtu kesho na kesho kutwa unaenda kuoa kijijini kwenu.
 
Hili limenipa faraja.

Lengo langu sio kutafuta sababu ya kuachana nae kama baafhi wanavyojaribu kuonesha. Lengo ni kuwa na uhakika katika haya anayoyafanya ni sahihi, kuna watu wanafanya au ndio jipya kwetu sote?
mkuu ukifuatilia matendo ya binadam yeyote kwa siri ni rahisi sana kujawa na hofu akat kumbe hakuna kibaya au ubaya wowote anaoufanya, kumbuka kila binadam ana utahira fulani ambao mara nyingi huudhihirisha akiwa pekee
 
Mstiri mtoto wa watu acha kutafuta sababu. Mtu mpaka anakuhangaikia hivyo ni ww ndio huenda unayataka, anakupenda halafu unataka kujifanya kichwa ngumu.
 
Yaani wewe hutaki kuoa ila unataka kufaidi ya ndoani? Kama hunampango wa kuoa hivi jirani na unawakwa na tamaa ya mwili watafute wanaofanya hayo bila malengo ya kuoana, otherwise waache innocent garls wenye malengo ya ndoa watimize ndoto zao. Ni very boring bint anajitolea akijua ndoa ipo kumbe wewe unataka kupata huduma yake kwa Sasa wakati hunampango wa kuoa soon
 
Nionavyo mimi hapo uyo dada anaonekana ndio anajifunza ayo mambo ya kiafrika pia nia yake sio mbaya sana kwako, kingine anashawishika alipowaona wenzake wameolewa ndio kachanganyikiwa sana, labda nikuulize swali mzee baba kwako mpango wa kumuoa uyo mdada upo au ndio kiburudisho tu na je itachukua mda gani mpk uje umuwowe? Mana ninavyoona mimi kinachofuata hapo ni kwenda kwenye mizizi na habari ya mizizi si mchezo utaenda mwenyewe kutangaza ndoa
 
Shukrani sana. Nitafanya hivyo, maana amenipa wasiwasi sana.
.................Elewa sipingani na ushauri alioutoa mdau hapo juu ila kwa manufaa ya muda mrefu ushauri huo hautakuwa na afya kutokana na hatua utakayofikia baada ya kuufata itaweza ije ikuumize maisha yako yote.

Huyo mwanamke ni mshirikina na usikubali kufanya naye ndoa ukiwa forced anataka kuolewa kuwaiga wenzake hali ya kuwa hazijui changamoto za ndoa atakuja akusumbue ujute,pia maoni yangu mwaka mmoja kwa uchumba ni mdogo sana kufanya mfikie kwenye ndoa chakata akili kama muislam owa mbele ya safari akibadilika utamalizana naye kiutu uzima ila kama mkristo kaa chini uwaze sawa sawa.
 
Back
Top Bottom