walitola
JF-Expert Member
- Nov 28, 2014
- 4,832
- 5,632
Kwanza nikupe ongera una moyo wa huruma sana mkuu mana ni wachache wenye moyo kama huo wako, tuje sasa kwenye suala la kuoa kwa hapo yakupasa ukae utafakari moyo wako ndio uamue sio kukupreshalaizi kuingia kwenye maisha ya ndoa pasipo ridhaa yako ndoa ina mambo mengi sana uyo mwanamke asikupakinikishe eti umuoe mwisho wa siku mambo yaende ndivyo sivyo kaa fikiri fanya maamuzi
Mpango upo, mkubwa mtu. Labda niwashikirikishe jambo jingine. Mbali na kumuhudumia yeye kimahitaji yote ya kiuchumi, kumfungulia duka la nguo na vifaa vya watoto na akina mama, kumpatia moja ya gari langu kutumia. Lakini pia nalipia sehemu ya ada ya mdogo wake.
Hayo yote yanaonesha utayari wangu wa kuwa na yeye kwa muda mrefu hata ndoa. Ila hatuwezi tu kuanza kuoa. Katika kipindi hiki chote mbali na niliyomkuta nayo, ni binti mkarimu na mwenye adabu sana. Muelewa na mcheshi hata kwa ndugu zangu wanaomfahamu.
Samahani, nimekujibu yote kwa urefu maana kuna mchangiaji mmoja amesema huyu binti anajitolea na nampoteza muda. Nadhani akipitia hapa ataelewa na mimi jinsi nilivyoanza kuwekeza kwake.


