Tuttyfruity
JF-Expert Member
- Dec 3, 2017
- 2,414
- 6,389
Wanaume dawa yenu ndogo, hueleweki taratibu unaeleweshwa
Habari wana bodi.
Hii ni mara yangu ya kwanza kuandika kwenye jukwaa hili, japo kuwa ni mshiriki mzuri wa kusoma na kutoa maoni kwenye mada mbalimbali jukwaani. Leo kuna kitu ningependa kuwashirikisha, pengine kuna wajuvi wa mambo ambao watanisaidia vema.
Nipo kwenye mahusiano na binti mmoja mwenyeji wa mikoa ya Kanda ya Ziwa. Ni muda wa mwaka sasa nipo naye kwenye mahusiano haya. Tumekuwa na wakati mzuri sana, japo mikwaruzano ya hapa na pale haikosekani ila sio mikubwa sana kuleta taharuki.
Kitu ambacho nakiona na najifunza kutoka kwa mwenzangu ni utayari wake wa kutaka kuolewa. Tokea mwezi wa sita mwaka huu yeye habari zake ni mahala pa kufanyia harusi, gharama za ukumbi na chakula, wangapi waje kwa harusi n.k.
Mbaya zaidi, karibia rafiki zake wote wameolewa na nimekuwa napata shinikizo kutoka kwa wenzake kwa njia zisizo za moja kwa moja.
Binafsi, sipo tayari kwa mahusiano ya ndoa kwa hivi karibuni. Ila mpango wa kufunga nae ndoa upo kwa zaidi ya asilimia 50. Shida inakuja kwa upande wa mwenzangu kulazimisha, kuwa karibu na ndugu zangu, hata kunitambulisha kwa watu wazito wa mkoani hapa.
Kilichonifanya niandike uzi huu, ni jambo lililotokea na kulishuhudia binafsi asubuhi hii. Mara nyingi, huwa akiwa amekuja nitembelea kwangu basi huwa tunaenda kuoga pamoja kila mara, iwe asubuhi au jioni au hata baada ya chakula adhimu.
Ila leo asubuhi mwenzangu akaenda oga peke yake. Wakati anaoga, nilienda taratibu kwa lengo la kujumuika naye ila nikasema ngoja nijibanze ili nimfanyie utani wa kumshtua, michezo ya hapa na pale. Mlango wa bafu ulikuwa wazi, nikaweza mtazama alichokuwa anafanya. Mwenzangu alianza kujisafisha sehem zake za siri akawa anarudia rudia mara nyingi kuliko kawaida na jambo la kushangaza, ule mkono aliokuwa anajisafishia akaudumbukiza kwenye ndoo ya maji ambayo niligundua alikuwa amenitengea nije kuoga.
Tokea asubuhi tukio hili limenifikirisha sana na kunifanya kuanza kumtazama tofauti mwenzangu. Sio kwa ubaya ila wasiwasi unanifanya niwaze zaidi.
Nje ya jambo hili, huwa tunasali pamoja na kushirikiana mambo kadha wa kadha ya sala. Ila hili la leo limenishtua mno na kunikosesha amani.
Kwa wajuvi wa mambo, je kuna haja ya mimi kuwa na wasiwasi juu ya tukio hili au nifunike kombe mambo yaendelee?
Nawasilisha.
Mkimbie huyo manzi ni mshirikina anakuandalia limbwata
Hakuna kitu chochote kibaya hapo. Ila wewe unataka kumtafutia sababu tu.
weee jamaa sasa unaogopa nini hapo tena hayo maji pigia hadi mswaki
Wanaume dawa yenu ndogo, hueleweki taratibu unaeleweshwa
Umesema huwa mnafanya sala pamoja, kwa hiyo huwa mnazini kwanza ndio mnasali au mnasali ndio mnaingia kuzini? Samahani nimeona hapo tu mengine sijui
Kabila lake tafadhali.....
We jamaa yaani mnatenda dhambi za uchafu afu eti mnasali pamoja??????! Shit! Umenikumbusha dada mmoja alikuwa anajiita mpendwa na rafiki yake akawa anakuja na Biblia eti wamekuja kuomba wakaishia kupeana mimba. Guys hamuwezi fanya mapenzi nje ya ndoa afu mkaingia kwenye sala wote mkiwa wazinzi!!
Naunga mkono hoja.Wanaume dawa yenu ndogo, hueleweki taratibu unaeleweshwa
Alichofanya ni kibaya kwanini asimpige?
Ampige na amuache.. Kumbuka huwezi jua ilikua dawa ya nini ile
Unaweza kunichokoza upate maelezo ya kutosha. Niulize maswali ya kutosha ili niweze kukujibu. Siwezi kuweka kila kitu.
Balehe inakusumbuaHabari wana bodi.