Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 269,634
- 697,845
Hitaji la Katiba Mpya mwangwi wake unazidi kusikika kuliko wakati mwingine wowote.
Kwa nje tu hivi ni kama kila kitu kinaenda sawa lakini kuna hali fulani ya taharuki ya kimya na sintofahamu kubwa ndani yake.
Ni kama kuna mambo yanapangwa huko halafu yanaletwa upenuni bila hata kueleweshwa vema
Kiongozi mkuu ni kama kawekewa mipaka mingi na kutengwa na hadhira.
Anahangaishwa huko na huko na kuwekwa busy kwa mambo ambayo yalistahili kufanywa na wasaidizi wake.
Kuna hofu fulani miongoni mwetu. Kuna uoga umewashika watu ni kama vile kuna jinamizi kubwa lisiloonekana linatuchungulia na kutufuatilia na kutusikiliza
Si kama nchi iko kwenye auto mode la hasha. Bali kuna kikundi cha wachache ndani ya mfumo pengine ndio kimeyateka mamlaka!
Watu hawasikiki lakini wapo
Watu hawaonekani lakini vitendo vyao unaviona!
Tunanyukwa kimyakimya!
Hii hali haina afya kwa taifa na haipaswi kuendelea kwa muda mrefu. Hawa wanaozungukana huko ndani hawana nia njema na taifa hili. Sinema si kwamba zimeisha bali zinaandaliwa zingine kutuweka busy tena tuyasahau haya!
Kama hizi hisia zangu ni kinyume na uhalisia basi napaswa kuonana na tabibu haraka! Ila kama si kinyume. MUNGU TUSAIDIE