Nina mashaka kuna kikundi ndio kinaendesha nchi kwa sasa

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
182,833
2,000
Hitaji la Katiba Mpya mwangwi wake unazidi kusikika kuliko wakati mwingine wowote.

Kwa nje tu hivi ni kama kila kitu kinaenda sawa lakini kuna hali fulani ya taharuki ya kimya na sintofahamu kubwa ndani yake.

Ni kama kuna mambo yanapangwa huko halafu yanaletwa upenuni bila hata kueleweshwa vema

Kiongozi mkuu ni kama kawekewa mipaka mingi na kutengwa na hadhira.

Anahangaishwa huko na huko na kuwekwa busy kwa mambo ambayo yalistahili kufanywa na wasaidizi wake.

Kuna hofu fulani miongoni mwetu. Kuna uoga umewashika watu ni kama vile kuna jinamizi kubwa lisiloonekana linatuchungulia na kutufuatilia na kutusikiliza

Si kama nchi iko kwenye auto mode la hasha. Bali kuna kikundi cha wachache ndani ya mfumo pengine ndio kimeyateka mamlaka!
Watu hawasikiki lakini wapo

Watu hawaonekani lakini vitendo vyao unaviona!

Tunanyukwa kimyakimya!

Hii hali haina afya kwa taifa na haipaswi kuendelea kwa muda mrefu. Hawa wanaozungukana huko ndani hawana nia njema na taifa hili. Sinema si kwamba zimeisha bali zinaandaliwa zingine kutuweka busy tena tuyasahau haya!

Kama hizi hisia zangu ni kinyume na uhalisia basi napaswa kuonana na tabibu haraka! Ila kama si kinyume. MUNGU TUSAIDIE
 

chizcom

JF-Expert Member
Jul 31, 2016
4,484
2,000
Kuna watu fulani wakifa wote na vizazi vyao ndio nchi mpaka chama ccm kitakuwa salama.

Ila to late maana watoto zao wameshakuwa na wajukuu.

Umeshawahi kusikia miaka ya nyuma japo ni siri sana “mtoto wa jamhuri”

Hawa kwa sasa wanawatoto ila babu zao bado wapo na kwani wanachelewa kufa
 

Unknown2

JF-Expert Member
Oct 16, 2016
2,216
2,000
Mkuu, tusilaumu watu.

Mama yetu sio mfuatiliaji, ni mtu anayepokea ushauri bila kuutafakari.

Ni mtu wa safari, mikutano na matamasha.

Hajui nchi iende wapi, mipango ya kuifanya Tanzania iwe ya viwanda (Malengo ya Magu) haipewi kipaumbele tena, demokrasia (iliyoonekana kuwa leadership style yake) anaiongea mdomoni tu.

Kwa ufupi mama hakujiandaa kuwa Rais, hata baada ya kuwa bado hawazi na kutenda kama Rais. Katika hali kama hiyo ni wazi kuwa kuna watu bila kutaka ndo wanaongoza nchi.

Kwa ufupi nchi inaongozwa na washauri.
 

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
182,833
2,000
Mkuu, tusilaumu watu.

Mama yetu sio mfuatiliaji, ni mtu anayepokea ushauri bila kuutafakari.

Ni mtu wa safari, mikutano na matamasha.

Hajui nchi iende wapi, mipango ya kuifanya Tanzania iwe ya viwanda (Malengo ya Magu) haipewi kipaumbele tena, demokrasia (iliyoonekana kuwa leadership style yake) anaiongea mdomoni tu.

Kwa ufupi mama hakujiandaa kuwa Rais, hata baada ya kuwa bado hawazi na kutenda kama Rais. Katika hali kama hiyo ni wazi kuwa kuna watu bila kutaka ndo wanaongoza nchi.

Kwa ufupi nchi inaongozwa na washauri.
Hapa ndipo ninapoona hitaji la katiba mpya. Leo nimeambiwa tozo kwenye mabenki zimeanza rasmi
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom