Nina kopi moja tu ya picha private, video private, pdf za mali, vyeti, leseni, n.k. njia gani nzuri ya kufanya backups mpya kila wiki bila bando?

Tembelea ttcl watakuhudumia kwa unlimited internet,kwa mwezi kama elfu 50 tu; ulimwengu wa sasa ni ku-save kidigitali na si kianalojia.
Hao ttcl nawajua mkuu, tangu enzi za internet cafes.

Kuwekewa tu hio internet yao ni bei sana ukiwa haupo eneo zenye nguzo zao.

Na hata kama nikiwa nayo hio ya elf 50 ku upload ni MB 1 kwa sekunde, Mzigo wangu wa GB 200 hapo hadi umalizike ni zaidi ya siku mbili.

Ndio maana nimeomba ushauri wa local backups, kwa hapa bongo online backups ni changamoto sana
 
Naona ni heri niweke tu hata windows 7 maana itakuwa mahsusi kwajili ya kutunzia backups tu.

Sasa mkuu, ni njia gani salama ya kuzi encrypt hizo backups yani kuzililinda mtu asipate access kirahisi mfano hadi aingize password
Encryption zipo nyingi tu, sema nazo ni risk, hasa ukipoteza hio key ndio umepoteza data zako so kuwa makini.

Software ya Bure ambayo watu wengi wanatumia ni veracrypt ambayo inaset password unapowasha computer kabla hujaboot windows itakudai password, hata mtu akichomoa HDD akiweka machine nyengine Bado itadai password ile ile. Ni software ya Bure.
 
Back
Top Bottom