Nina kopi moja tu ya picha private, video private, pdf za mali, vyeti, leseni, n.k. njia gani nzuri ya kufanya backups mpya kila wiki bila bando?

Uncle bright

JF-Expert Member
Feb 9, 2023
1,040
4,080
Nimejikuta nina hofu ya kupoteza data zangu hasa baada ya matukio kadhaa ya kupoteza flash, kuibiwa simu, n.k. Data zilizokuwemo humo zilipotea moja kwa moja, ni kumbukumbu za muhimu siwezi kuja kuzipata tena.

Najua kuna online back ups lakini hizi kila mwezi inabidi ulipie na pia unahitaji bando kubwa sana ikiwa una mafaili makubwa.

nina desktop siitumiagi ya zamani pentem 4 , gb 500 hard disk nimepata wazo pengine naweza kuitumia kwa kazi hii pekee,

ninahitaji kwa sasa niwe na central backup ya kutunzia nakala zangu zote za mafaili ya simu, laptop, camera, n.k.

Mafaili yangu muhimu kwa ujumla ni gb 150 ila kila wiki naweza nikawa naongeza mapya.

Ulinzi wa data nazo backup nao ni muhimu,
 
Kama una uelewa kidogo na computer itafutie desktop wifi weka lightweight Linux weka mafile Yako humo, ukipata 500gb nyengine ukafanya backup kote kote itasaidia zaidi, kama una ujuzi zaidi weka raid kabisa.

Alternative hio 500gb inunulie kasha iwe external then fanyia backup humo.
 
Tumia terabox wanakupa 1TB,
Ila unaposema bila bando utakuwa huelewi unachozingumzia.
Nimeweka wazi kwamba kwangu mimi na watanzania wengi bando ni changamoto sina unlimited Internet kufanya backups za mamia ya GB kila wiki, kwa hio nawezaje kutumia hii desktop niliyonayo kufanya backups kwa usalama
 
Kama una uelewa kidogo na computer itafutie desktop wifi weka lightweight Linux weka mafile Yako humo, ukipata 500gb nyengine ukafanya backup kote kote itasaidia zaidi, kama una ujuzi zaidi weka raid kabisa.

Alternative hio 500gb inunulie kasha iwe external then fanyia backup humo.
Mkuu vp nikiweka partition ya gb 50 iwe ya window kisha GB 400 zinazobaki niwe natunzia backups.

Ntawezaje kufanya hili kwa usalama, sitaki mtu apate access ya mafaili yangu akichomeka hard disk kwenye computer nyingine
 
Pia sawa ila nimekushauri Linux sababu pentium 4 ni ya zamani sana windows itakaa ila itakua slow, sema sio mbaya pia kama unaona complication weka windows 7,

Pia nimekushauri HDD nyengine Incase Moja imiharibika nyengine inabaki na data. Hdd za 500GB hazifiki hata 20,000.

Unachofanya una backup data zako kwenye hdd zote mbili.
 
Hivi naweza kupata Linux online??
 
Tumia terabox wanakupa 1TB,
Ila unaposema bila bando utakuwa huelewi unachozingumzia.
Mkuu Samahani nikuulize swali pengine waweza nisaidia. Nawezaje kurudisha gmail account ambayo sikumbuki password wala no ya simu niliyosajilia. Yani in short naikumbuka hiyo gmail account tu na kuna picha za muhimu so nilikuwa nauliza alternative way ya kuipata password if possible niweze kuback up picha zilizomo kwenye hiyo gmail account
 
Hivi naweza kupata Linux online??
Zipo kibao na nimesema tu Linux kama mjumuisho ila zinajilikana kama Linux distributions, kama Ubuntu, Mint, fedora, arch, etc kutokana na specs zako unaweka itakayokufaa, zipo kama Ziron ambazo hata PC za miaka 20 iliopita zinakaa.
 
Mkuu samahani kuna picha niliziback up kwenye gmail account kitambo kidogo sasa sikumbuki password wala ile no ya simu niliyotumia wakati wa kusajili. Je naweza kupata password nikabackup picha zilizopo kwenye hiyo gmail account?
 
Unatakiwa uforgot password watakupa hint ni namba Gani ulitumia, mfano ********62 watakuekea namba mbili za mwisho za hio namba.

Ama inawezekana uliweka recovery email watakwambia utumie hio ku reset password.
 
Nimekupata mkuu. Tatizo lililopo hapo siikumbuki ile no ili niweze kureset password wala alternative email niliyotumia. Hiyo gmail account ni ya muda kidogo yani inshort naikumbuka username ya hiyo gmail account tu
 
We weka forgot password wao watakupa hint, bila kujaribu hutakumbuka.
 
Kama una uelewa kidogo na computer itafutie desktop wifi weka lightweight Linux weka mafile Yako humo, ukipata 500gb nyengine ukafanya backup kote kote itasaidia zaidi, kama una ujuzi zaidi weka raid kabisa.

Alternative hio 500gb inunulie kasha iwe external then fanyia backup humo.
nimesoma nimesikia mwangwi tu😅😅😅
 
Tafuta RaspberryPi, config kama backup server.

Moja ya jamaa yangu, nilisha wahi kuona anacho icho kidude
 
Data za muhimu 'save' kwenye 'email' yako
Naombeni tuwe tunasoma post nzima, Nimeweka wazi kwamba hapa nchini kuna changamoto ya kupata access ya unlimited internet kwa hio option rahisi huwa ni local backups ndiyo nayohitaji mawazo yake.

Kubackupa GB 200 kwa haya mabando ya kawaida ghali mno
 
Pia sawa ila nimekushauri Linux sababu pentium 4 ni ya zamani sana windows itakaa ila itakua slow, sema sio mbaya pia kama unaona complication weka windows 7,

Pia nimekushauri HDD nyengine Incase Moja imiharibika nyengine inabaki na data. Hdd za 500GB hazifiki hata 20,000.

Unachofanya una backup data zako kwenye hdd zote mbili.
Naona ni heri niweke tu hata windows 7 maana itakuwa mahsusi kwajili ya kutunzia backups tu.

Sasa mkuu, ni njia gani salama ya kuzi encrypt hizo backups yani kuzililinda mtu asipate access kirahisi mfano hadi aingize password
 
Naombeni tuwe tunasoma post nzima, Nimeweka wazi kwamba hapa nchini kuna changamoto ya kupata access ya unlimited internet kwa hio option rahisi huwa ni local backups ndiyo nayohitaji mawazo yake.

Kubackupa GB 200 kwa haya mabando ya kawaida ghali mno
Tembelea ttcl watakuhudumia kwa unlimited internet,kwa mwezi kama elfu 50 tu; ulimwengu wa sasa ni ku-save kidigitali na si kianalojia.
 
Back
Top Bottom