Kama jina lako, unataka kushuhulika na mtu wa jinsia yako..sasa huyo mumeo atakutosheleza kweli au umeanza kumpoteza mawazoni mwako?. Jaribu kuachana na hizo tamaa zisizo na maana na zenye kuweza kukuongezea dhambi katika daftari lako la hukumu. Epuka kuanza kumsifia Mwanamke mwenzio kwa staili hii ambayo inaonyesha wazi kuwa kama hukuwahi kuangukia kwenye aina hiyo ya mapenzi ya Kisagaji, basi haitachukua muda mrefu utajikuta umepotea kabisa. Jiulize mara mbilimbili, hivi nini raha ya kushuhulika na mtu wa jinsia yako?. Na kama unazama katika hiyo aina ya mapenzi, kwa jamii yetu ambayo ina kioo kila kona kama kamera za CCTV, utafanyia wapi hayo mapenzi nawe ni mke wa Mtu?.
Hata kama unajaribu kuleta habari ya kufikirika, lakini kimsingi inawezakena kabisa haya yapo mawazoni mwako, yatakutafuna na kukuzamisha..mara nyingi Shetani huwa anasingiziwa..lakini ukiangalia unaweza kuona kuwa Binadamu huwa tunamtengenezea Shetani jukwaa (plat-from) mioyoni mwetu na badae tukionekana tunakwenda kinyume (kutenda dhambi) tunamsingizia yeye ndo katufanya tufanye hivyo. Haifikiriki kwa mwanamke timamu kuanza kumtamani mwanamke mwenzio kihivyo na kuthubutu kueleza hadharani na bayana hisia zako ambazo unaweza kuzithibiti mwenyewe iwpo una utimamu wa maungo na akili na ni mfuasi wa dini...Ni aibu!.
Hizo hisia za ajabu bana DD. Achana nazo na kumbuka kama unafuata maandiko, ukimtamani mwanamke kwa Kuzini nae, umekwisha zini..tubu na kuacha hiyo mambo kabisa..ni aibu sana sana na haipaswa kueleza watu hayo madudu ya kiluwani!