Nina hisia kali na mwanamke mwenzangu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nina hisia kali na mwanamke mwenzangu

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Diana-DaboDiff, Jun 1, 2010.

 1. D

  Diana-DaboDiff JF-Expert Member

  #1
  Jun 1, 2010
  Joined: Jul 13, 2009
  Messages: 380
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nlipokuwa sekondari na baadae chuo nilihisi kuwa na hisia za kimapenzi na wanawake wenzangu lakini niliweza kuzishinda na kuendelea na maisha yangu.Mwezi mmoja ulopita kuna dada kaajiriwa ofisini kwetu na toka nimuone kwa mara ya kwanza nimekuwa na hisia kali juu yake.

  Dada huyu ana tabia ya kutukumbatia kina dada wenzake anapotusalimia asubuhi sasa huu umekuwa mtihani mkubwa kwangu napenda tukumbatiane kwa muda mrefu na labda tungekuwa peke yetu ningetamani kumbusu mdomoni na hata kumpapasa. Namuwaza huyu dada muda wote hata kumuota usiku.Ndoa yangu ina miezi sita tu nampenda mume wangu lakini nashindwa kudhibiti hisia hizi kwa dada huyu.

  Dada mwenyewe ana msimamo kaisha watolea nje vijana wawili ofisini hapa kuwa hataki mpenzi kwa sasa anataka kuweka akili zake zote kazini. Msichana ni mrembo kweli, mrefu, mwembamba na ana lips za kufa mtu. Nafikiria kuacha kazi na kuhamia ofisi nyingine kuna kampuni waliniambia muda wowote ninaotaka watanichukua.

  Nishaurini wanajamvi wenzangu yamenikuta.
   
 2. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #2
  Jun 1, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,035
  Trophy Points: 280
  hii ni hatari bora uhame ofisi
   
 3. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #3
  Jun 1, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Fanya maombi kwa Mungu na atakuepusha na pia kama una uwezo wa kuhama kazi ni vizuri pia.

  zidisha dua kwa bidii sana.
   
 4. Eliphaz the Temanite

  Eliphaz the Temanite JF-Expert Member

  #4
  Jun 1, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,836
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Njia bora ya kushinda jaribu ni kulikimbia! hama!
   
 5. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #5
  Jun 1, 2010
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,002
  Trophy Points: 280
  swali la msingi je ulishawahi, kufanya mapenzi na mwanamke mwenzio au ni mpenzi wa kuangalia picha za lesbian?
   
 6. D

  Diana-DaboDiff JF-Expert Member

  #6
  Jun 1, 2010
  Joined: Jul 13, 2009
  Messages: 380
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nimefanya kazi hapa miaka kadhaa na si unajua kuanza upya vigumu? na huko nikikutana na majaribu haya nihame tena? Nipo njia panda.
  span.jajahWrapper { font-size:1em; color:#B11196; text-decoration:underline; } a.jajahLink { color:#000000; text-decoration:none; } span.jajahInLink:hover { background-color:#B11196; }
   
 7. D

  Diana-DaboDiff JF-Expert Member

  #7
  Jun 1, 2010
  Joined: Jul 13, 2009
  Messages: 380
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nimefanya kazi hapa miaka kadhaa na si unajua kuanza upya vigumu? na huko nikikutana na majaribu haya nihame tena? Nipo njia panda.
  span.jajahWrapper { font-size:1em; color:#B11196; text-decoration:underline; } a.jajahLink { color:#000000; text-decoration:none; } span.jajahInLink:hover { background-color:#B11196; }
   
 8. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #8
  Jun 1, 2010
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...sema nae.

  Msimamo wake waweza kubadilisha hisia zako kwake.
  Lakini je? iwapo atakubaliana na ushawishi wako, upo tayari kushare habari hii na mumeo?

  Je, utachukuliaje mumeo akikwambia naye alikuwa na hamu sana ya threesome, nyote watatu
  siku moja mjumuike kwenye huo mchiriku?
   
 9. A

  Audax JF-Expert Member

  #9
  Jun 1, 2010
  Joined: Mar 4, 2009
  Messages: 444
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Huyo uliyenaye ni pepo tu na utakuwa uliwahi kufanya mapezi au kuwa na uhusiano na wanawake wenzio.Ebu simama imara muaibishe shetani.Sali saan,funga kwa ajili hiyo na jaribu kufanya kazi mda mwingi-hakika mawazo potofu yatatoweka.
   
 10. R

  Ramos JF-Expert Member

  #10
  Jun 1, 2010
  Joined: May 13, 2010
  Messages: 498
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Inaweza kuwa pepo au mazoea, lakini pia ni tabia ya binadamu, sawa na baadhi ya wanaume wanavyokuwa na ham ya kunanihii na wanaume wenzao. Ukikimbia kaz haitasaidia. Utakakokwenda waweza kukumbana na kishawishi kikubwa zaidi.

  Cha muhimu elewa kuwa hiyo itakuwa tabia mbaya na sugu endapo ikianza. itaharibu ndoa yako na kushusha heshima yako mbele ya watanzania wenzio. Jikaze kisabuni kuvumilia na kumkwepahuyo dada kadiri utakavyoweza...
   
 11. D

  Diana-DaboDiff JF-Expert Member

  #11
  Jun 1, 2010
  Joined: Jul 13, 2009
  Messages: 380
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Sijawahi kufanya mapenzi na mwanamke mwenzangu wala kupenda picha za kisagaji lakini hisia tu ambazo zimeongezeka maradufu baada ya kumtia binti huyu machoni.

  span.jajahWrapper { font-size:1em; color:#B11196; text-decoration:underline; } a.jajahLink { color:#000000; text-decoration:none; } span.jajahInLink:hover { background-color:#B11196; }
   
 12. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #12
  Jun 1, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Uwe makini mama unakoelekea ni kubaya. Jitahidi kukishinda hiki kishawishi vinginevyo ndoa huna!
   
 13. D

  Diana-DaboDiff JF-Expert Member

  #13
  Jun 1, 2010
  Joined: Jul 13, 2009
  Messages: 380
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Katika dunia hiyo ya kufikirika kichwani mwangu nikisema nae akakubali kuwa nami sidhani kuna nafasi ya mwanaume tena itabidi niongee na mume wangu tuachane ili niishi na kipenzi changu kwa hiyo hilo la 'threesome' halitakuwa na nafasi.
  span.jajahWrapper { font-size:1em; color:#B11196; text-decoration:underline; } a.jajahLink { color:#000000; text-decoration:none; } span.jajahInLink:hover { background-color:#B11196; }
   
 14. Fisherscom

  Fisherscom JF-Expert Member

  #14
  Jun 1, 2010
  Joined: Mar 13, 2008
  Messages: 1,427
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Pepo mbaya huyo anakutawala. Jitahidi kumshinda,ikishindikana hama ofisi.
   
 15. D

  Diana-DaboDiff JF-Expert Member

  #15
  Jun 1, 2010
  Joined: Jul 13, 2009
  Messages: 380
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nimejaribu kupambana na hisia hizi zaidi ya miaka minane na nilifanikiwa kuzififisha lakini toka nionane na huyu mrembo nahisi sitaweza tena kuzizuia,akicheka,akiongea,akitembea,akiniangalia natamani kumkumbatia na kumueleza hisia zangu.Nimeomba ruhusa kazini siku mbili lakini haijasaidia,nampigia simu kusikia sauti na kicheko chake.
   
 16. Mpeni sifa Yesu

  Mpeni sifa Yesu JF-Expert Member

  #16
  Jun 1, 2010
  Joined: May 23, 2010
  Messages: 649
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  sasa mwanamke mwenzio atakufanyaje ndugu yangu hata maumbile ya kiume hana...au utambandika plasic...huyo ni shetani was sodoma na gomora anakutengenezea barabara ya moto wa milele kimbia nenda kaombewe kanisani haraka....
   
 17. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #17
  Jun 1, 2010
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Hapo huna jinsi, umenasa kwa kweli. Ila ukiamua unaweza kuzigeuza hizo hisia badala ya kukuelekeza kwenye mambo ya mapenzi ya ngono zikakuelekeza kwenye urafiki mzuri wa watu wawili.
   
 18. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #18
  Jun 2, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Kama jina lako, unataka kushuhulika na mtu wa jinsia yako..sasa huyo mumeo atakutosheleza kweli au umeanza kumpoteza mawazoni mwako?. Jaribu kuachana na hizo tamaa zisizo na maana na zenye kuweza kukuongezea dhambi katika daftari lako la hukumu.

  Epuka kuanza kumsifia Mwanamke mwenzio kwa staili hii ambayo inaonyesha wazi kuwa kama hukuwahi kuangukia kwenye aina hiyo ya mapenzi ya Kisagaji, basi haitachukua muda mrefu utajikuta umepotea kabisa.

  Jiulize mara mbilimbili, hivi nini raha ya kushuhulika na mtu wa jinsia yako?. Na kama unazama katika hiyo aina ya mapenzi, kwa jamii yetu ambayo ina kioo kila kona kama kamera za CCTV, utafanyia wapi hayo mapenzi nawe ni mke wa Mtu?.

  Hata kama unajaribu kuleta habari ya kufikirika, lakini kimsingi inawezakena kabisa haya yapo mawazoni mwako, yatakutafuna na kukuzamisha..mara nyingi Shetani huwa anasingiziwa..

  Lakini ukiangalia unaweza kuona kuwa Binadamu huwa tunamtengenezea Shetani jukwaa (platform) mioyoni mwetu na baadae tukionekana tunakwenda kinyume (kutenda dhambi) tunamsingizia yeye ndo katufanya tufanye hivyo.

  Haifikiriki kwa mwanamke timamu kuanza kumtamani mwanamke mwenzio kihivyo na kuthubutu kueleza hadharani na bayana hisia zako ambazo unaweza kuzithibiti mwenyewe iwpo una utimamu wa maungo na akili na ni mfuasi wa dini...Ni aibu!.  Hizo hisia za ajabu bana DD. Achana nazo na kumbuka kama unafuata maandiko, ukimtamani mwanamke kwa Kuzini nae, umekwisha zini..tubu na kuacha hiyo mambo kabisa..ni aibu sana sana na haipaswa kueleza watu hayo madudu ya kiluwani!
   
 19. pcman

  pcman JF-Expert Member

  #19
  Jun 2, 2010
  Joined: Oct 9, 2008
  Messages: 743
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  "Lakini kila mmoja hujaribiwa na tamaa yake mwenyewe huku akivutwa na kudanganywa. Halafu ile tamaa ikiisha kuchukua mimba huzaa dhambi, na ile dhambi ikiisha kukomaa huzaa mauti. Ndugu zangu wapenzi, msidanganyike. " (Yakobo 1:14-16).
   
 20. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #20
  Jun 2, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Dii Dii,
  Kwenye hiyo kufikirika..ina maana ushaamua kuwa thats what you want? Ushauri unaoutaka hapa ni upi is it namna ya kufikia ukweli wa hiyo kufikirika yako? Maana kama ushaamua kufanya kweli, ushauri wa kukukataza hautakusaidia at this stage.

  Ila ujue..binadamu anayo sehemu fulani katika maisha au akili yake ambayo hamna mtu mwingine aijuae isipokuwa mwenyewe. Kuna wanaokuuliza kama ulishafanya mapenzi na mwanamke mwenzio na umejibu hapana. Sasa hizi hisia zinazokupata ukiwa tayari mke wa mtu mamii zinakuja vipi na kwa kasi hiyo hadi unataka ushauri?

  Kama walivyosema wachangiaje wengine hapo juu, binadamu katika maisha huwezajikuta aki fantasize mambo mengi -mema na mabaya.Mfano mtu kujaribu kufantasize anaiba Bank! Ina maana wazo hili litamsumbua kiasi hicho hadi aje humu kuomba ushauri akaibe au lah?

  Mwisho nakushauri hivi - kama ni fantasy tu jiambie "wake up woman!"uamke kwenye hiyo hali usonge mbele.

  Kama siyo fantasy bali ni kitu ulishakiwaza ukadhamiria kukitenda basi hapa hakuna ushauri labda maombi tu.

  I hope sijakukwaza ndugu yangu.
   
Loading...