Nina hakika hili lilishakutokea hata wewe

Nina hakika hili lilishakutokea hata wewe

Maisha hutukutanisha na mengi kuanzia kuzaliwa. Makuzi kujitambua utu uzima, uzee hadi kifo.. Ni kati ya hayo mengi kuna mazuri na kuna mabaya. Kuna ya kuumiza moyo na kuna ya kuleta faraja. Kuna ya kukumbuka kwa namna ya pekee kabisa lakini pia kuna ambayo hutamani usiyakumbuke Kabisa

Kisa changu na mchunga ng'ombe Dsm Ubungo Kibo
Nitasimulia kwa vipande hivyo mtaniwia radhi
Mwanzoni mwa miaka ya tisini, nikiwa eneo tajwa nikipambana kuanza maisha nilitapeliwa kodi ya nyumba shilingi elfu 18, kodi ya miezi 6 kwa kupangishwa chumba cha mtu
Nilidhani nimepata kumbe nimepatikana kwakuwa wakati huo kodi chumba hakikuwa chini ya sh 5000.. Lakini mimi nikapatac kwa 3000 tena kina kitanda cha chuma cha BANCO na godoro lake..lakini bila foronya bila shuka

Siku ya tatu tangu kuingia makazi yangu mapya nikakutana na taharuki kubwa.. Chumba nilichopangishwa kilikuwa kimoja tu kwenye foundation ya nyumba ya vyumba vitano.. Nikakuta mtu kakaa hapo nje na mabegi na watoto wawili na mwanamke! Na ilikuwa ni saa nne usiku

Automatically hao ndio walikuwa wenye nyumba, yalitokea mengi kwa muda mchache lakini niseme tu kwamba kufika saa nne na robo usiku sikuwa na pa kulala
Nitaendelea...
 
Uzi huu umenifanya niwaze uchungu wa ili kaka mmoja mkazi wa kusin lakini alikua akisoma ilboru secondary sijui walikutana vipi na mama mdogo, lkn kila jumapili alipenda kuja kumsalimu mama mdogo alikua akipewa mahitaji yake kwani alitoka familia ya hali ya chini, nakumbuka graduation yake tulimpelekea keki alifurahi na hakuamini kwani hakua na yeyote ambae angeenda isipokua familia ya mama mdogo,
Miaka ilipita baada ya kuhitimu na bila mawasiliano siku akarudi kurudisha fadhila kwa mama mdogo kwani alikua ameshafanikiwa, kaka alienda kule alikokua akiishi mama mdogo akaambiwa alihama muda akaja kwa bibi kwan alikua tayar kama familia japo aliemzoea zaidi ilikua mama mdogo, amefik nyumban mwenyewe ana afya nzur mwili umebadilika hakuna anaemkumbuka kakaribishwa vizur ndio akamuulizia mama mdogo ameamia wapi? Tuliposema mama amefariki zile yowe yule kaka alizipiga mpaka watu wakajaa nyumbani wakijua kuna msiba , kazi ikawa kumbembeleza, aliumia sana kaka yule japo kwa sasa sijui yupo waoi tena
 
Hii imenikumbusha teja mmoja maeneo fulani
Nikiwa njiani kwenye usafiri wa uma niliumwa kichwa kisichoelezeka,hewa ikawa nzito kupumua nikawa najiskia kutapika ilinibidi nishuke na nilitapika sana macho yakawa kama yanaingiwa ukungu nikaona kifo hichi hapa,huyu kaka alipotokea sikujua alinitafutia maji akanimwagia kichwani na mengine akanipa nikasukutua akatafuta mchanga wa kufukia matapishi na kunifuta miguuni na tshirt alilokua amevaa alisimama pembeni yangu mpk nilipopata nguvu ya kuamka hapo chini

Nilimshukuru na siku nyingine nilirudi hapo nikamuulizia sikufanikiwa kumuona mpk leo,ndani yangu nafeel kama sikumshukuru vizuri lakini sijui wapi naweza muona

Somo nililojifunza ni kitomdharau mtu koz hujui nani atakua msaada kwako,kwa macho ya nje anaonekana ni TEJA ila kwa macho ya ndani alikua MALAIKA kwangu


Cc Kingsmann
Story yako imenifikirisha sana mkuu, tangu asubuhi ninairudia kuisoma, hakika duniani bado kuna watu wenye mioyo ya huruma licha ya magumu wanayopitia.
 
R. I. P
IMG_20220718_142633.jpg
 
I had a friend. Mlisoma nae primary. Tulikua darasa la nne, Irene wangu alikua mchaga. It was so hard for me to make friends. And i was bullied so much at school. But when i met her things got better. No one bullied me anymore. Lakini alihama shule. Since then sijawahi kukutana nae tena na sijui alihamia wap. I hope I meet you again Irene you were my bestest friend.
Nami pia iren kimaro sijui haya majin tena wachaga hua wanapotelea wapi
 
Maisha hutukutanisha na mengi kuanzia kuzaliwa. Makuzi kujitambua utu uzima, uzee hadi kifo.. Ni kati ya hayo mengi kuna mazuri na kuna mabaya. Kuna ya kuumiza moyo na kuna ya kuleta faraja. Kuna ya kukumbuka kwa namna ya pekee kabisa lakini pia kuna ambayo hutamani usiyakumbuke Kabisa

Kisa changu na mchunga ng'ombe Dsm Ubungo Kibo
Nitasimulia kwa vipande hivyo mtaniwia radhi
Mwanzoni mwa miaka ya tisini, nikiwa eneo tajwa nikipambana kuanza maisha nilitapeliwa kodi ya nyumba shilingi elfu 18, kodi ya miezi 6 kwa kupangishwa chumba cha mtu
Nilidhani nimepata kumbe nimepatikana kwakuwa wakati huo kodi chumba hakikuwa chini ya sh 5000.. Lakini mimi nikapatac kwa 3000 tena kina kitanda cha chuma cha BANCO na godoro lake..lakini bila foronya bila shuka

Siku ya tatu tangu kuingia makazi yangu mapya nikakutana na taharuki kubwa.. Chumba nilichopangishwa kilikuwa kimoja tu kwenye foundation ya nyumba ya vyumba vitano.. Nikakuta mtu kakaa hapo nje na mabegi na watoto wawili na mwanamke! Na ilikuwa ni saa nne usiku

Automatically hao ndio walikuwa wenye nyumba, yalitokea mengi kwa muda mchache lakini niseme tu kwamba kufika saa nne na robo usiku sikuwa na pa kulala
Nitaendelea...
Mpaka ww mzee sangoma ukatapeliwa daah kweli mbuyu kama mchicha, fanya hima tusiwe na vipande vingi kama VIKITIM kuleee kwenye story ya kugongewa yai na kaka yake mwarabu
 
Mpaka ww mzee sangoma ukatapeliwa daah kweli mbuyu kama mchicha, fanya hima tusiwe na vipande vingi kama VIKITIM kuleee kwenye story ya kugongewa yai na kaka yake mwarabu
[emoji23] nitamalizia usiku kipande kimoja tuu.. Miaka hiyo nilikuwa bado kuanza ulozi ndio maana walinichezea sana[emoji35][emoji34]
 
Naendelea

Ilibidi jamaa anitolee rambo yangu yenye kikombe cha plastic, mswaki, sabuni kipande cha mbuni, dawa ya mswaki kitaulo, fulana, kadet na ndala nikaondoka
Nikawa sijui pa kwenda mfukoni nina 500 tuu nikapita mahali uwanjani kuna kibanda cha kuuza vitu vidogo vidogo. Mwenye kibanda namjua ila hatukuwa na ukaribu sana
Nikaamua kumsimulia mkasa wangu .. Akakubali nilale pale lakini kesho niangalie Mishe nyingine
Ilibidi kukaa nje pale uwanjani na wahuni kibao wakivuta bangi mpaka saa saba usiku ndio wakatawanyika

Tuliingia kulala lakini miguu ikabaki nje [emoji23] kibanda kilikuwa kidogo mno... Kufika tisa kasoro usiku nikaamshwa na kujionea maajabu, kumbe wale wavuta bangi walikuwa wezi wa majumbani usiku
Yaani walianza kuleta vitu mbalimbali vya wizi
TV zile chogo
Deck za mikanda ya sinema
Vyombo
Nguo
Feni nknk
Vitu viliendelea kuletwa mpaka saa kumi kasoro hivi, na kama nususaa baadae wakawa wanakuja wengine kuvilipia na kuondoka navyo.. Kufika kumi na moja alfajiri hapakuwa na kitu kilichobaki aisee.. Mwana keshakunja mpunga wake mzuri tuu, kugawana baadae
Tulirudi kulala chini kwenye box miguu nje ila akaniasa kuwa pale hapanifai kwakuwa polisi hufika muda wowote na kubeba watu linapotokea tukio la wizi ama msako wa kawaida
Siku yangu iliisha kwa tabu kwasababu ya uchovu na ilipofika usiku nilirudi tena palepale
Yule mwana akanikutanisha na jamaa mchunga ng'ombe ambaye alikubali kunihifadhi kwenye chumba alichopewa na boss wake, ye ye akilala kwenye box na mimi kwenye kigodoro kidogo chembamba mpaka nilipofanikiwa kupata chumba kingine.. Alinihifadhi almost wiki 2
Baada ya mwezi toka nipate chumba nilihamia mtoni kwa Aziz Ally na huko ndio nilipata mchongo wa South na kuondoka

Nilirudi Bongo kwa mara ya kwanza 1998 lakini sikufanikiwa kuonana naye kabisa.. Natamani na naamini kuna siku kuna muujiza utatokea na tutaonana tena kama bado yuko hai.. Cha kuniumiza zaidi simkumbuki jina,[emoji19]
 
Kaka Mshana Jr ahsante sana kwa huu uzi japo unaniliza kila nikiusoma toka niuone nikianza kutype nalia kiasi kuna mtu kaniona anasema nina shida gani ?

Nina visa vingi nitashare kadri ya muda wangu .

Kisa cha kwanza .
Mwaka fulani nikiwa chini ya uangalizi wa familia ,basi mmoja wa walezi wangu alihamishiwa songea sehemu inaitwa Chabruma kambi ya jeshi hivyo kwakuwa ilikuwa likizo ya masomo kwa upande wangu ikanibidi nikawe naye kwa kipindi cha likizo zangu za masomo

Bahati mbaya tulipofika huko haikuchukua hata week akawa anatakiwa kuondoka kuelekea Sudan japo makazi yake ilikuwa ni hapo kwa huo muda sasa ikawa natakiwa kubaki hapo mpaka muda wa likizo uishe ndiyo nirudi Dar es salaam

Baada ya yeye kuondoka nikabaki mwenyewe ila niliibiwa hela zote pale ndani katika mazingira nisiyoyaelewa , kumpigia huyo ndugu naona kama ni msala basi ikabidi nikaze tu japo nikaanza kuwaza nipate vipi hela ya kula na nauli niondoke .

Ni katika harakati hizo nakutana na wazungu waliongia hapo Chabruma ambapo ni kambi ya jeshi , wazungu waliingia ili kufanya research zao japo walikosea location mlima waliokuwa wanautaka haupo kambini ila unaonekana nje ya kambi yaani kijiji cha pili ila inaonekana ilikuwa kinyemela japo walihitaji msaada wangu kuwaelekeza mlima huo , sikuwa mwenyeji ila kwa siku kadhaa nilizokuwepo na kwa maelezo yao nikajua ni mlima niuonao upande wa pili ambao upo nje ya kambi yaani ni kijiji cha pili.

Sasa kumbuka sina hela wala nini tamaa ikaniiingia kuwa hawa hawaniachi bila chochote hivyo nitapata walau nauli niende dar.

Bahati mbaya tulikamatwa na wajeda tukiwa tunavuka kumbe kuna sehemu hutakiwi kupita , mimi pasipo kujua nilistuka tunasimamishwa na wajeda na moja kwa moja tukaelekezwa kambini huko ilikuwa ni vurumai kila nikijieleza sikueleweka na mzigo wote ukaelekezwa kwangu kama vile mimi ndiye mtoa ramani ya kambi kwa wazungu , nilipigwa sana ndani ya week mpaka kiasi cha kutamani kufa .

Nikiwa katika ulinzi mzito wa wanajeshi , Mungu ananikutanisha na afande Juma baada ya wiki ya mateso makali anapewa kazi ya kunihoji namuelekeza kila kitu ananielewa vizuri siku ya pili naruhusiwa kuondoka huku yeye akinifuata nyumbani na kunipa hela ya kula na nauli ikiwa nitahitaji kuondoka.

Niliondoka pale kambini katika hizo kota baada ya siku mbili , nikiwa dar siku moja baada ya miaka minne ya hayo . Nimeenda kumuona rafiki yangu Muhimbili ndiyo nakutana na afande Juma akiwa kitandani yu dhoofu hali katika kitanda cha pembeni

Ila mwingi wa tabasamu , nikaahidi kurudi siku ya pili kumuona na pia nibebe chochote kitu , ila siku niliyofika ndiyo siku ambayo afande Juma alifariki nafika naambiwa alifariki usiku na maiti ilishachukuliwa , niliumia sana maana sikuwa na namba ya ndugu yeyote wala namba ya marehemu labda nipige yawezekana ndugu yeyote atapokea

Namkumbuka sana huyu afande maana bila yeye nahisi ningekufa pale maana nilikuwa mpira wa vijana waliotoka depo hivyo walikuwa wananifanya vile watakavyo .

Namuombea Allah aendelee kumpa kauli thabiti uko aliko , sikulipa fadhila zake .
Nimeenda kumuona rafiki yangu Muhimbili ndiyo nakutana na afande Juma akiwa kitandani yu dhoofu hali katika kitanda cha pembeni[emoji24][emoji2827]
 
Kisa cha pili
Nikiwa chuo mwaka wa pili katika chuo nilichokuwepo kulikuwa na utaratibu wa kuomba field katika mtandao wa chuo then unaenda kufanya mafunzo ya vitendo yaani field , katika kufanya hivyo nikapata sehemu niliyotaraji

Ila baada ya huo mtandao kufungwa nikawa nimebadilisha mawazo kuwa niende sehemu nyingine hii kutokana na msukumo wa marafiki na pia kupunguza gharama za usafiri

Basi chuo kilikuwa na utaratibu ikiwa mtandao umefungwa na unahitaji kubadili kituo cha mafunzo inakubidi utafute kituo mwenyewe kwa kwenda kuonana na wakuu wa idara wa hiyo sehemu unataka kwenda uwaombe kufanya field hapo wakikubali wakupe barua , hiyo barua umpatie msimamizi wako wa field

Alafu uende sehemu uliyoomba kwenye mtandao ukutane na mkuu wa hiyo department umueleze kuwa hautaweza kufanyia hapo field sababu ya kuwa unaenda kwingine

Ofcourse nilifanya hivyo ila bahati mbaya sehemu ya kwanza ya field niliyoomba , mkuu wa hiyo department aliniplease sana kuwa ana uhitaji sana na watu wa fani yangu hivyo hakubaliani na maamuzi yangu

Ujana maji ya moto , mimi nikaona ananizingua ikiwa tayari nishamaliza wajibu wangu , hivyo field ilipoanza kwa muda wake mimi nikawa naenda zangu sehemu ya pili nilipoomba kwa mdomo

Later on coordinator wa field ananipigia simu kwanini sijauhudhuria kwenye field nikamueleza kuwa nipo sehemu fulani na barua nishatuma , akasema ikiwa nataka hivyo niende nimalizane na mkuu wa idara wa sehemu niliyoomba mwanzo then anipe barua pia ya kuridhia mimi kutofanya field kwake .

Hilo nilijua lisingewezekana hivyo njia pekee niliandika barua mwenyewe na nikaanza kuusaka muhuri wa ile department kupitia watu wangu wa karibu , badae nikaupata

Nikaenda Temeke nikachonga muhuri wa ile department then nikaupiga kwenye barua nikamtumia coordinator (utoto )

Siku ya assessment coordinator anasema ulinidanganya mbona mkuu wa department ya kule mwanzo hakuwahi kukuona ? Hivyo uliforge muhuri

Nikaona hili ni zali nikakubali kosa ila nikahitaji tuyamalize akakaza

Hivyo field ikaishia pale , tumerudi chuo nasubili what's up mara napigwa na barua ya kikao cha nidhamu
Siku naenda kwenye kikao nakutana na pannel ya madaktari na maprofesa wote wananisikiliza mimi huku nje polisi wananisubili .

After five hours ya kikao , hukumu inatoka kwa upande wa chuo sitakiwi chuo nimedisco na pia nakabidhiwa kwa askari ili waendelee na uchunguzi .

Ni hapo Mungu anamleta profesa mmoja anaikataa hukumu huku akihitaji sababu za yule mkuu wa department kunikatalia mimi kwenda sehemu nyingine hivyo haoni kama kuna sababu ya mimi kudisco na kutoendelea na masomo

Mara pannel yote iko kimya hakuna anayesema chochote , mara mtoa hukumu anauliza wangapi hawakubaliani na hiyo hukumu , bado yule profesa anakuwa upande wangu .

Inapangwa kikao siku nyingine , ni hapo mimi nakabidhiwa kwa askari ila sifiki nao mbali tukiwa njiani wanasimamishwa na gari la profesa aliyenitetea kwenye mataa ya fire hapo kariakoo , anawaomba tuyamalize mimi niwe huru

Note :sikuwa na undugu wowote na yule mzee wala sikuwa chini yake darasani maana hakuwepo kwenye fani yangu

Sikujua ni kiasi gani alitoa ila naambiwa dogo kuwa makini sana , nashuka kwenye difenda napanda kwenye hilux , narudishwa chuo mpaka chumba namba 16 , kwenye ofisi ya huyu mzee anaitaka historia yangu mbali na shule nampa historia anasema toka hapo mimi ni mwanaye .

Kesi iliisha kimya kimya maana sikuitwa tena nikaendelea na masomo

Profesa mawasiliano yaliendelea vizuri japo nilikuja kupoteza simu hivyo ikanichukua muda kidogo kupata namba yake maana alihama chuo na kwenda South africa,,ila usiku mmoja wenye giza nilitumiwa meseji na namba ngeni ya kuwa rafiki yako amefariki akiwa South africa

Inaniuma sana maana sina fadhila niliyolipa kwake hasa alivyonipambania
Kila nikiwaza naumia sana , nimebaki na picha za ukumbusho tu

Bahati mbaya hakuwa na mtoto wala mke
Na hakuletwa hapa Tanzania alizikwa huko
South africa
Natamani hata nilione kaburi lake , niseme asante kwa zile fadhila zake

Kila nikisikia story za chuo basi moyo umkumbuka mzee profesa na machozi hayakawii.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom