HALELUYA MOSHI
JF-Expert Member
- Aug 14, 2014
- 2,121
- 1,205
Jaribu kumtafuta kwenye mitandao ya jamii kama Facebook, na CRB. Hebu ungetuwekea alichofanya tushee(share) experience.
Fb nimemtafuta kwa jina hilo but nahic nakosea unless awe hajaweka picha ambayo naweza kumtambua!
CRB nimeuliza tena kuna baadhi ya watu ambao nawafaham kabisa huko but kwa hilo jina hatambui (kitu ambacho nahic wanajuana kwa majina ya makumpuni yao zaid) unless watu wawe wanafahamian from a long way!
Ilikuwa hiv
Nilikutana na huyu mheshimiwa wakiwa kwenye semina ya CRB Mkoa fulani, hapo mahali walipotumia kisemina ndipo nilipokuwa napatumia sana kupata mkate wangu wa kila siku (tubiashara coz palikuwa panaleta watu sana) mtaji wangu ukiwa laki moja baada ya kuikusanya almost miaka 2 (you won't believe this )
Siku 5 za semina yao,alifanya haya!
1. (Sidhan kama alitaka kweli kununua biashara yangu) akawa ananisema kwa stail ya maswali sanaaaaaaaa! And of the day akanipa ushaur kama napenda na naweza nirud shule! Of which naona aligundua napenda ila maisha hayajaruhusu, (nakumbuka alisema unaonekana ukiwa binti mzuri rudi shule itakusaidia ) I DID AS HE DREAMED (nakumbuka hiyo day 2 ya semina ilikuwa, mda wake wote wa lunch alitumia hapo kupiga story na mimi) mwenyewe nikiwa niko busy kukaribisha watu kwa ajili ya riziki,
2. Day 3 ya semina, the same time, (lunch time) akaja akiwa anataka mrejesho wa ushauri wake je nimeuchukuliaje ! Nilianza kumuona kama ananifuatilia sana maisha yangu, nakumbuka nilimjibu in a very like rude way! Wala hakuonesha kuchkizwa cha ajabu akanipa hela nikale (nakumbuka moyoni nilianza kumuona wale wale kasoro majina) akasema lifanyie kazi suala la shule!! Akaondoka
3. Day 4 ya semina yao, akaja na kunipa business card, aliongea sana siku ile, akiwa kagundua kuwa nampuuza, akasema acha na hizi biashara, nikisema nikusaidie mtaji iko siku utaibiwa na hakutokuwa na biashara tena, umri wako bado unaruhusu kurudi shule nenda shule! Akasema ukiwa tayar mda wowote niambie namba hizo hapo nimekula naongea na wewe kama mdogo wangu wala sio kama unavonifikia! Akaondoka ( only God knows nilivojisikia siku ile nililia sana Nilipofika home)
Siku ya 5 ya semina yao na ikiwa ndo ya mwisho mimi sikuenda , but nilipoenda nikakuta matatizo kwa secretary wa pale kwamba kuna mtu Anasema amekupa namba umpigie! Nilitumia simu ya yule dada, aliongea sana yule kaka, akasema ntapiga baada ya siku mbili uwe umetafuta shule!
In short,
Nilitafuta shule (kimasihara tu maana nilikuwa hata siamin) ajabu alituma hela nakumbuka kwa njia ya basi, akiwa amefunga na vitu vingine kukiwemo na simu (so mtu asingeweza kujua kama kuna hela na alimkabidhi dereva ) nikapokea na kurudi shule tena, na kila nilipohitaj maskin hajawahi kusita hadi nimeliza! (Ilikuwa level ya advance )
Niwakumbushe tu tangu ile semina hatujaonana kwa macho zaid ya kumweleza kwa simu nilipofikia na hajawah kunikatisha tamaa kabisa!
Na alilipa ada zoooooooote na pocket money juu! (Mtaniuliza wazazi wangu je! Yaachen it's another long story )
Nilitafuta kibarua, thank God nikapata, nikamwambia kwa simu tu (I took him more than a brother to me since then) good or bad nikapangiwa mkoa mwingine nikamjuza akanitia moyo sana kuwa maisha ni popote!
Tulivopoteana sasa,
Nikiwa kikazi kule tukavamiwa nilipokuwa naishi, was bad indeed (tuliibiwa kila kitu in short tulisafishwa na simu zikaibiwa)