Nina hakika hili lilishakutokea hata wewe

Nina hakika hili lilishakutokea hata wewe

Dahh umenigusa sana aseeh mwaka 2001 iyo nipo mjin tanga nikiwa naenda shule galanosi nikajikuta nimeibiwa kila nilichokuwa nacho kwenye mazingira ya kutatanisha niliwaona wezi wale wakikimbia kwambali na mtu mmoja alikiwa kama anawakimbiza nikaenda mpaka police kufanya taratib walichukua bag lilikuaga na vitambulisho vyote na pesa.... Ikapita kama nusu saa yule aliekuwa anawakimbiza akaja pale police akiwa na bag lile na alikuwa anavuja damu mikonon inaonekana alipata shubir kidogo dahh alikuwa kaka mmoja mapolice walisema huyu ni mkichaa na kwel mavazi yake tu yalisema alikuwa na upungufu wa akili basi bana alipo kuja na lile bag alipo liweka pale akakimbia mbio dahh nilimkimbiza bila mafanikio ..... Nilienda shule ila nilikuwa namuwaza sana nilikuwa natoroka shule kuja kuzurura town kumtafuta bila mafanikio nikaja kuambiwa amepelekwa mirembe nilifurah kwakuwa mm home dodoma na uncle alikuwa anafanya kaz pale likizo nilipo fika sikulaz damu nikaenda mirembe kwel bana nikamuona alikuwa ameshaaza kupona tulipiga story nikamkumbushia ila hakukumbuka kitu nikamwambia kwa wema alionifanyia hata asipokumbuka nitamfanya kuwa bro wangu kabisa basi likizo yote ile nilikuwa naenda sana kumsalimia pale na alipo pata nafuu alirud tanga nimerud shule kumuulizia nikaambiwa aliporud tu hakukaa sana akafariki dahh RIP brother
safi, ulifanya jambo la maana sana kumtafuta......kwa hakika, kwa mtazamo wangu, umelipa vya kutosha tu.
 
I had a friend. Mlisoma nae primary. Tulikua darasa la nne, Irene wangu alikua mchaga. It was so hard for me to make friends. And i was bullied so much at school. But when i met her things got better. No one bullied me anymore. Lakini alihama shule. Since then sijawahi kukutana nae tena na sijui alihamia wap. I hope I meet you again Irene you were my bestest friend.
inaumiza sana hiyo, umenikumbusha rafiki yangu wa ukweli niliyekuwa nae o'level yote......ni ajabu kupoteana watu katika umri na uelewa kama huo lakini imetokea. HASSAN HARUNA NKYA, where are you?!!!!
 
hii mada ni very touching, nina mawili ambayo nayakumbuka sana!

mwaka 2013, nakumbuka ilikuwa mwezi Disemba, nilikuwa nahamisha makazi kutokana Dar ambako nilikuwa kwa miaka mitatu kwa sababu za kimasomo kurudi kazini kwangu kusini mwa tanzania. kutokana na haraka niliyokuwa nayo nikamuomba rafiki yangu flani hivi wa ukweli niliyesoma nae primary ambaye makazi yake permanent sasa yalikuwa hapo hapo Dar anisafirishie vitu vyangu mi nikiwa nimetangulia. alilipokea hilo na akaniahidi atavituma siku ya pili tu. jioni ya siku ya pili, alinitumia ujumbe ambao ninao mpaka leo katika simu yangu kuwa amevisafirisha kupitia gari flani inayoitwa Mashallah na kwamba ameviandika jina lake vifaa vyote hivyo nikae tayari kuvipokea siku inayofuata. ilipofika asubuhi, wakati huo gari iliyobebea hivyo vifaa ipo njiani inakuja, napokea simu kuwa yule rafiki yangu amefariki baada ya kugongwa na gari wakati anarudi kutoka katika mizunguko yake mbagala.......kumbe mizunguko hiyo ni kule kuja kunisafirishia vifaa vyangu. UTUHUMIWA NINAOJIHISI SIJUI UTATOKA LINI!!!!!!! nilichanganyikiwa mno na kamwe sitasahau hili, alikuwa ni mtu mwema sana sana tangu udogo wake. nashukuru nipo pamoja na mama'ake na tunaelewana sana. maisha haya ukiyatafakari kwa kina, utabadilika na kuwa mtu mwema sana......sisi binadamu hakuna kitu!!

tukio la pili ni la kutenda wema kwa upande wangu. ilikuwa mwaka 2002 wakati nasoma huko kibaha, pwani. alikuja dada fulani hivi maeneo ya shule amefadhaika anatafuta mtu mwenye damu group o+, mimi ndo group langu hilo.. nikajitokeza, mwalimu aliniruhusu na tukaenda na yule dada Tumbi hospitali. tulitumia muda mrefu sana pale na hatimaye baada ya vipimo vya damu kukidhi haja nikaruhusiwa kudonate. nilidonate free of charge na niligundua kumbe ilikuwa kwa ajili yake mwenyewe. baada ya tukio hili alinishukuru yule dada, aliulizia jina na kidato na kuahidi angenitembelea siku moja...nilikuwa kidato cha tatu wakati huo. hakutokea hadi namaliza shule na kuondoka, sijui kilichoendelea katika tatizo lake la kiafya lakini naamini Mungu alimsaidia na kupona. najivunia tukio hili kwani nahisi ni kama kubwa kiasi kulifanya mtu!! kila la kheir dada Elizabeth (kama nakumbuka sawasawa) popote ulipo!!
 
Bado namkumbuka dadaangu JAMILA MAZOEA na kwenye ulimwengu wa roho analifahamu hili
Tangu jana usiku kumbukumbu zake zimekuwa zikijirudia mpaka ikabidi niitafute hii mada
 
NIMEONA umenitia simanzi mno hiyo ya huyo jamaa yako! Apumzike kwa amani
 
Nilichoweza kumsaidia ni mwaka 1993 ambapo nilikutana naye akaniomba sh mia mbili ambayo nilimpa ile ya noti kipindi hicho, baada ya siku ile sikuwahi kuonana naye mpaka mwaka 2010 nilipoenda kwake na kuambulia kuonyeshwa kaburi lake![emoji24][emoji24][emoji24]
 
Hii mada imegusa mno, imefunga sana na binafsi imeniamshia ndani yangu nia ya kutenda wema, wema ni akiba isio na mfano.
Imenikumbusha pia kushukuru, shukrani ina faida sana kwa mwenye kuitoa.
Asante sana mleta mada na walio changia, ila tujue Mungu yupo kupitia kwa wenzetu, tusiwe wabaya kwa mtu yoyote,tusudharau yoyote kwa kati yetu sote Mungu anatutumia kuwa msaada kwa wenzetu.
 
[emoji1545][emoji2827][emoji24]
 
nakumbuka kipindi flani nikiwa masomoni kwa vitendo Yaani field

nikiwa katika department ya blood transfusion and haematology, alipita daktari akiomba mtu yoyote ambae yuko willing kuchangia damu, basi vijana wote hawakua tiari but mimi dhamira yangu ikawa inanisuta

nikakubali kwenda kuchangia damu. kufika kule sehemu ya uchangiaji, wakawa wanasema kuna mgonjwa wa dharura anahitajika kubadilishiwa damu kwa haraka lakini inahitajika damu yenye group A postive... baada ya kupimwa katika wachangiaji mm nikawa pekee mwenye group A postive

Baada ya kufanikisha zoezi la kutoa damu, watoto wa yule mzee walinishukuru sana, wakaniomba nikamuone mzee wao, mimi sikutaka kwenda lakini walinisihi sana, ikanibidi niende... aisee kumbe yule mzee alikua anasumbuliwa na kansa ya damu😭 nilimuonea huruma mateso aliyokua anapata kitandan pale mpaka leo picha inanijia... nilipotoka pale wodini nililia sana😭😭

kesho yake nikapewa taarifa yule mzee alifariki usiku wa kuamkia leo mana hata ile damu hawakumungezea😢😢

aisee niliumia sana
 
nakumbuka kipindi flani nikiwa masomoni kwa vitendo Yaani field

nikiwa katika department ya blood transfusion and haematology, alipita daktari akiomba mtu yoyote ambae yuko willing kuchangia damu, basi vijana wote hawakua tiari but mimi dhamira yangu ikawa inanisuta

nikakubali kwenda kuchangia damu. kufuka kule sehemu ya uchangiaji, wakawa wanasema kuna mgonjwa wa dharura anahitajika kubadilishiwa damu kwa haraka lakini inahitajika damu yenye group A postive... baada ya kupimwa katika wachangiaji mm nikawa pekee mwenye group A postive

Baada ya kufanikisha zoezi la kutoa damu, watoto wa yule mzee walinishukuru sana, wakaniomba nikamuone mzee wao, mimi sikutaka kwenda lakini walinisihi sana, ikanibidi niende... aisee kumbe yule mzee alikua anasumbuliwa na kansa ya damu[emoji24] nilimuonea huruma mateso aliyokua anapata kitandan pale mpaka leo picha inanijia... nilipotoka pale wodini nililia sana[emoji24][emoji24]

kesho yake nikapewa taarifa yule mzee alifariki usiku wa kuamkia leo mana hata ile damu hawakumungezea[emoji22][emoji22]

aisee niliumia sana
Imagine ungejisikiaje kama ungegoma kuchangia? Nina imani ungeumia zaidi
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom