Pls ukiweza share nasi unaweza kupata relief fulani moyonimshana umenigusa sana baba, naamin weng wamefanikiwa kutokana na kujitoa kwa moyo kwa watu wengne tofaut na ndug zao. Umenkumbusha mbal mbal mbaaal sana bado natafakar sana
Pole Mkuu Mshana,hata mimi nina tabia ya kuwa guilty iwapo sijarudisha hisani,hata hivyo Mungu atakufariji kwa kuwa nia yako ni nzuri kwa aliekusaidia Mkuu,R.I.P Jamila Mazoea.Ni jambo la kihisia mno, jambo lililo ndani ya moyo kabisa lisilotoka na ambalo hujirudiarudia kila Mara!
Ni kuhusu wema uliowahi kutendewa na mtu baki halafu ukaahidi kimoyomoyo kumlipa lakini isiwezekane kwakuwa hujawahi kuonana naye tena au pengine keshafariki.
Nakumbwa na hiyo hali! Namkumbuka mno Dada Jamila Mazoea R.I.P alinipenda sana na kunisaidia katika mengi, lakini kabla ya kuwa na uwezo wa kulipa wema wake kwangu alitwaliwa kutoka katika maisha haya.
Nilichoweza kumsaidia ni mwaka 1993 ambapo nilikutana naye akaniomba sh mia mbili ambayo nilimpa ile ya noti kipindi hicho, baada ya siku ile sikuwahi kuonana naye mpaka mwaka 2010 nilipoenda kwake na kuambulia kuonyeshwa kaburi lake!
Bado namkumbuka dadaangu JAMILA MAZOEA na kwenye ulimwengu wa roho analifahamu hili
Daah Pretta na urembo wote huo mtu akuone kima?,anyway mimi umeshindwa kunisaidia niki rest in peace si utajikula roho sana mamii? au unamuogopa shemeji yangu?RIP dada Mazoea...........wengine huwa tunasaidia wengine lakini wanakuona kima.......ndio maisha lakini......
Mkuuu we ni kamilioniNiliwahi kuanguka kutoka ghorofa ya tatu hadi chini, nikapelekwa amana, sio siri yule dada alinihudumia vizuri sana, kama vile private, niliwah kwenda cku moja wakaniambia ameingia shift nyingine, nakushukuru sana dada mary siku moja nitakuja kusema ahsante mbele yako
Story yako japokuwa ni kwa ufupi ila imenipa kitu fulani ndani yangu.Mungu ambariki huko alipo na afanikishe kukutanisha nae kwa mara nyingine tena.Fb nimemtafuta kwa jina hilo but nahic nakosea unless awe hajaweka picha ambayo naweza kumtambua!
CRB nimeuliza tena kuna baadhi ya watu ambao nawafaham kabisa huko but kwa hilo jina hatambui (kitu ambacho nahic wanajuana kwa majina ya makumpuni yao zaid) unless watu wawe wanafahamian from a long way!
Ilikuwa hiv
Nilikutana na huyu mheshimiwa wakiwa kwenye semina ya CRB Mkoa fulani, hapo mahali walipotumia kisemina ndipo nilipokuwa napatumia sana kupata mkate wangu wa kila siku (tubiashara coz palikuwa panaleta watu sana) mtaji wangu ukiwa laki moja baada ya kuikusanya almost miaka 2 (you won't believe this )
Siku 5 za semina yao,alifanya haya!
1. (Sidhan kama alitaka kweli kununua biashara yangu) akawa ananisema kwa stail ya maswali sanaaaaaaaa! And of the day akanipa ushaur kama napenda na naweza nirud shule! Of which naona aligundua napenda ila maisha hayajaruhusu, (nakumbuka alisema unaonekana ukiwa binti mzuri rudi shule itakusaidia ) I DID AS HE DREAMED (nakumbuka hiyo day 2 ya semina ilikuwa, mda wake wote wa lunch alitumia hapo kupiga story na mimi) mwenyewe nikiwa niko busy kukaribisha watu kwa ajili ya riziki,
2. Day 3 ya semina, the same time, (lunch time) akaja akiwa anataka mrejesho wa ushauri wake je nimeuchukuliaje ! Nilianza kumuona kama ananifuatilia sana maisha yangu, nakumbuka nilimjibu in a very like rude way! Wala hakuonesha kuchkizwa cha ajabu akanipa hela nikale (nakumbuka moyoni nilianza kumuona wale wale kasoro majina) akasema lifanyie kazi suala la shule!! Akaondoka
3. Day 4 ya semina yao, akaja na kunipa business card, aliongea sana siku ile, akiwa kagundua kuwa nampuuza, akasema acha na hizi biashara, nikisema nikusaidie mtaji iko siku utaibiwa na hakutokuwa na biashara tena, umri wako bado unaruhusu kurudi shule nenda shule! Akasema ukiwa tayar mda wowote niambie namba hizo hapo nimekula naongea na wewe kama mdogo wangu wala sio kama unavonifikia! Akaondoka ( only God knows nilivojisikia siku ile nililia sana Nilipofika home)
Siku ya 5 ya semina yao na ikiwa ndo ya mwisho mimi sikuenda , but nilipoenda nikakuta matatizo kwa secretary wa pale kwamba kuna mtu Anasema amekupa namba umpigie! Nilitumia simu ya yule dada, aliongea sana yule kaka, akasema ntapiga baada ya siku mbili uwe umetafuta shule!
In short,
Nilitafuta shule (kimasihara tu maana nilikuwa hata siamin) ajabu alituma hela nakumbuka kwa njia ya basi, akiwa amefunga na vitu vingine kukiwemo na simu (so mtu asingeweza kujua kama kuna hela na alimkabidhi dereva ) nikapokea na kurudi shule tena, na kila nilipohitaj maskin hajawahi kusita hadi nimeliza! (Ilikuwa level ya advance )
Niwakumbushe tu tangu ile semina hatujaonana kwa macho zaid ya kumweleza kwa simu nilipofikia na hajawah kunikatisha tamaa kabisa!
Na alilipa ada zoooooooote na pocket money juu! (Mtaniuliza wazazi wangu je! Yaachen it's another long story )
Nilitafuta kibarua, thank God nikapata, nikamwambia kwa simu tu (I took him more than a brother to me since then) good or bad nikapangiwa mkoa mwingine nikamjuza akanitia moyo sana kuwa maisha ni popote!
Tulivopoteana sasa,
Nikiwa kikazi kule tukavamiwa nilipokuwa naishi, was bad indeed (tuliibiwa kila kitu in short tulisafishwa na simu zikaibiwa)
So touchingNi jambo la kihisia mno, jambo lililo ndani ya moyo kabisa lisilotoka na ambalo hujirudiarudia kila Mara!
Ni kuhusu wema uliowahi kutendewa na mtu baki halafu ukaahidi kimoyomoyo kumlipa lakini isiwezekane kwakuwa hujawahi kuonana naye tena au pengine keshafariki.
Nakumbwa na hiyo hali! Namkumbuka mno Dada Jamila Mazoea R.I.P alinipenda sana na kunisaidia katika mengi, lakini kabla ya kuwa na uwezo wa kulipa wema wake kwangu alitwaliwa kutoka katika maisha haya.
Nilichoweza kumsaidia ni mwaka 1993 ambapo nilikutana naye akaniomba sh mia mbili ambayo nilimpa ile ya noti kipindi hicho, baada ya siku ile sikuwahi kuonana naye mpaka mwaka 2010 nilipoenda kwake na kuambulia kuonyeshwa kaburi lake!
Bado namkumbuka dadaangu JAMILA MAZOEA na kwenye ulimwengu wa roho analifahamu hili
Emotional oneDahh umenigusa sana aseeh mwaka 2001 iyo nipo mjin tanga nikiwa naenda shule galanosi nikajikuta nimeibiwa kila nilichokuwa nacho kwenye mazingira ya kutatanisha niliwaona wezi wale wakikimbia kwambali na mtu mmoja alikiwa kama anawakimbiza nikaenda mpaka police kufanya taratib walichukua bag lilikuaga na vitambulisho vyote na pesa.... Ikapita kama nusu saa yule aliekuwa anawakimbiza akaja pale police akiwa na bag lile na alikuwa anavuja damu mikonon inaonekana alipata shubir kidogo dahh alikuwa kaka mmoja mapolice walisema huyu ni mkichaa na kwel mavazi yake tu yalisema alikuwa na upungufu wa akili basi bana alipo kuja na lile bag alipo liweka pale akakimbia mbio dahh nilimkimbiza bila mafanikio ..... Nilienda shule ila nilikuwa namuwaza sana nilikuwa natoroka shule kuja kuzurura town kumtafuta bila mafanikio nikaja kuambiwa amepelekwa mirembe nilifurah kwakuwa mm home dodoma na uncle alikuwa anafanya kaz pale likizo nilipo fika sikulaz damu nikaenda mirembe kwel bana nikamuona alikuwa ameshaaza kupona tulipiga story nikamkumbushia ila hakukumbuka kitu nikamwambia kwa wema alionifanyia hata asipokumbuka nitamfanya kuwa bro wangu kabisa basi likizo yote ile nilikuwa naenda sana kumsalimia pale na alipo pata nafuu alirud tanga nimerud shule kumuulizia nikaambiwa aliporud tu hakukaa sana akafariki dahh RIP brother