Rule L
JF-Expert Member
- May 31, 2020
- 2,180
- 3,473
Ngoja namm niweke yangu hapa mkuu, ila hii ni ya kusaidia.So touching to me this.
Kuna mwaka nilikua manyara nasimamia shamba la miwa la bro, flani hivi, sasa baada ya miwa kukatwa ikabidi niende kiwandani pale manyara sugar kupelekwa ile miwa nikiwa nasubiri pale kwenye folen
akaja mzee hivi akanisalimia baada ya hapo akaanza kunieleza yanayomsibu.
aisee nilimuonea huruma vibaya mno akasema yy alikua ziwani ni mvuvi sasa alipata kama laki sita hivi wenzake aliokua anaishi nao walimuibia usiku alafu wakaondka maana n kile kipindi magufuli anapiga vita uvuvi Haram kwahiyo yeye pale alikua ana hela za kuondoka kabisa ila
baada ya kuibiwa akawa hana ujanja tena.
Ikabidi atembee kwa miguu kutoka magara, hadi pale kiwandani angalau aje apate kibarua pale, kufika pale hakuna anaemjua hata mmoj akajaribu kuomba kazi pale akaambiwa ahonge 150k ili apate kazi, wakati huo yy hana hata mia alivyoniona pale akawa anaomba kama ninayo hata buku nimpe ajitetee kwa muuza chakula pale ale, aisee jamaa hata kuongea alikua anashindwa kutokana na njaa m mfukoni nilikua na buku tatu ambayo niliuza miwa njian tena namm mwenyewe nilikua nina njaa ya hatari ila ilibidi tu nimpe yule mzee yote akaniuliza naww vp mbn hela unanipa yote nikamwambia mzee m narudi shamba saivi we usijali kule kuna hela ipo wala haina shida.
Huwezi amini yule mzee alitaka kulia ila nilmbembeleza sana ikabd tu aache, akasema kijana nmeomba watu wengi sana tena wengine n wenye hela ila hawajanipa ww umenipa?? Akaushika mkono wangu akaubusu. Baadae nilivyotaka kuondoka akaomba namba yangu ya sim nikampa tena niliandka kwenye karatasi maana hata simu walimuibia.
Baada ya siku kama tatu hivi akanipigia simu akaniambia kua alitumiwa nauli na ndugu zake hivyo anaenda zake kwao musoma. aliomba simu pale ili anijulishe kama ameondoka.
kiukwel nilifurahi sana kwa kunikumbuka kwake ila hakuwahi kunitafta tena mpaka Leo sjui alipoteza ile namba. Ama ilikuaj.