Mkuu hali haikuwa nzuri.May Allah bless you but usingempotezea hata kama tunda lake hakuliitaji sababu kuna kitu ulikisababisha katika hali ya kisaikolojia.
Ulitembelewa na malaika mkuuNimepata somo kubwa kupitia uzi huu, ubarikiwe sana. Nahisi MWENYEZI MUNGU huwa anatutembelea kwa namna ya pekee kabisa,tujifunze kumheshimu kila mmoja wetu. Mie kuna siku nimeumwa nkalazwa hospital siku tano,siku nimeruhusiwa nikawa nimejilaza chumbani nikasikia hodi mlangoni,kufungua mlango nikakutana na madogo watatu wakiume,umri kati ya miaka 7-9.wakadai wameskia naumwa kwahiyo wamekuja kuniombea .Wakanambia nifunge macho wakaniwekea mikono kichwani tukaomba kwa pamoja afu wakaaga wakaondoka.ila baada yakuuliza majirani kama wanawajua hao madogo kila mmoja akasema hawajui na hajawahi kuwaona.niliwatafuta sana ila sikufanikiwa kuwaona tena.nakumbuka ilikua ni 2015 mpaka leo sijawahi kanyaga hospital wakati kabla ya hapo nilikua sikai mwaka bila kuumwa...
Unawakumbuka wa wale watoto watatu wa Fatima? Wangali wanaishi hata leoNimepata somo kubwa kupitia uzi huu, ubarikiwe sana. Nahisi MWENYEZI MUNGU huwa anatutembelea kwa namna ya pekee kabisa,tujifunze kumheshimu kila mmoja wetu. Mie kuna siku nimeumwa nkalazwa hospital siku tano,siku nimeruhusiwa nikawa nimejilaza chumbani nikasikia hodi mlangoni,kufungua mlango nikakutana na madogo watatu wakiume,umri kati ya miaka 7-9.wakadai wameskia naumwa kwahiyo wamekuja kuniombea .Wakanambia nifunge macho wakaniwekea mikono kichwani tukaomba kwa pamoja afu wakaaga wakaondoka.ila baada yakuuliza majirani kama wanawajua hao madogo kila mmoja akasema hawajui na hajawahi kuwaona.niliwatafuta sana ila sikufanikiwa kuwaona tena.nakumbuka ilikua ni 2015 mpaka leo sijawahi kanyaga hospital wakati kabla ya hapo nilikua sikai mwaka bila kuumwa...
Aliniambia mwanangu siku ile uliponipa nguo zako nilikuona zaidi ya baha yangu mzazi hasa ukizingatia sikukuomba wala nini, usiku nililia sana yani nina baba mzazi, baba mdogo wengi tu lakini hakuna anaenithamini hata kidogo na sio kwamba pesa hawana, nilijiapiza siku moja lazima nilipe wema wako na nikakuchukulia kama ndugu yangu wa damu kabisa.[emoji1752][emoji2827][emoji848]Nilichojifunza katika maisha always be humble kila kitu ulichonacho sio kwa akili na ujanja wako ila ni Mungu tu, kama alivyokupa pia anao uwezo wa kuchukua vilevile.
Nimeguswa na naomba ni share na mimi, japo kwa macho ya kawaida ni tukio dogo lakini amini wema wowote unaomtendea mtu basi unamkopesha Mungu.
Tukiwa kwenye mahafali ya kidato cha nne miaka kadhaa huko nyuma kuna jamaa yangu mpaka leo hiyo picha ninayo. Katika lile kundi la marafiki wote kwake tu mambo ndio hayakua mazuri sababu kubwa baba yake mzazi alikua ameoa mke mwingine hivyo wao wakawa wamesahaulika kabisa.
Enzi hizo wakuu form 4 ni form 4 kweli. Hivyo katika maandalizi tukawa tumepanga nguo kali za kununua, viatu n.k jamaa nae kwenye kundi ili asionekane mnyonge akawa anachangia mawzo nguo za kununua ili asibaki nyuma.
Siku tuliyokubaliana kwenda shopping jamaa akawa haonekani, tumemtafuta lakini wapi mwisho tukaenda wengine kama kawaida enzi hizo t-shirt na jeans na raba kali ndo ilikua unyama.
Tupo kwenye maandalizi kama kesho kutwa ndo mahafali nikakutana na dogo wa jamaa angu akanimbia bro haji kwenye mahafali mzee kamnyima ela ya nguo na viatu na mama kamwambia hana pesa.
Kwetu mambo hayakua mabaya wala mazuri sana tulikua familia ya daraja la kati hivyo kila sikukuu tulikua na uhakika wa kuvaa nguo mpya na viatu vipya kila sikukuu.
Kwa kujisikia vibaya jamaa alikua anajificha na kutukwepa ila kesho yake nilimvizia anakoenda kushinda nikamchagulua jeans, t-shirt na raba kali japo nilikua nilishazivaa tayari ila zilikua kama mpya, na nilimpa kimya kimya bila kumuambia mtu yoyote na hata siku ya graduation hakuna aliye notice chochote, tulipiga picha ya pamoja wana wote na mpaka leo ninayo.
Miaka kadhaa mbele mawasiliano yakiwa yamepungua kutokana na mishe mishe halafu jamaa alioa mimi sijao so tukawa wana ila sio kivile kama zamani. Mimi nilisoma mpaka ma vyuo vikuu huko yeye kutokana na life la msoto akaingia ku hustle kitaa mwisho wa siku Mungu sio Mandonga jamaa akatoboa, sasa na mimi ile ndo nimemaliza mambo ya kusoma nikaenda mkoa flan kucheki harakati mara nakutana na jamaa afu hapo katikati mawasiliano yalipungu mwisho yakafa kabisa, bahati nzuri jamaa alinikumbuka, jamaa alinisaidia sana kwenye mambo yangu mengi sana kuanzia kwenye michongo, mawazo hadi financial sababu yeye alikua ameshatoboa maisha tayari.
Aliniambia mwanangu siku ile uliponipa nguo zako nilikuona zaidi ya baha yangu mzazi hasa ukizingatia sikukuomba wala nini, usiku nililia sana yani nina baba mzazi, baba mdogo wengi tu lakini hakuna anaenithamini hata kidogo na sio kwamba pesa hawana, nilijiapiza siku moja lazima nilipe wema wako na nikakuchukulia kama ndugu yangu wa damu kabisa.
Lile jambo kwangu niliona kawaida na vile sijuagi kudai zile nguo nilimuachia kabisa sababu alichelewa kunirudishia sijui alikua anaona aibu au vipi. Ni kitendo cha kawaida lakini kwake alikipa uzito mkubwa sana, mpaka sasa bado tu wana na jamaa ananiamini sana kwa sababu katika michongo na vitu vingi alivonisaidia sijawahi kumuangisha wala kumharibia chochote.
Narudia tena wakuu, Wema ni akiba, ukipata nafasi ya kutenda wema hata kama ni mdogo kiasi gani wewe fanya ipo siku Mungu atakulipa. Wakati mwingine mambo yetu yanaenda sawa kwa sababu ya maombi ya hao tuliowatendea mema.
Umenikumbusha dogo mmoja nilimkutaga mji fulani kumbe alisomaga na mdogo wangu so yeye akanifahamu mi hata simjui. Basi nikamchukulia kama dogo langu na nikampambania nikampa kazi ofisini kwetu (nilimkuta anafanya kazi ya kutengeneza cappuccino kwenye coffeeshop moja hivi).RIP dada Mazoea. Wengine huwa tunasaidia wengine lakini wanakuona kima. Ndio maisha lakini.
Pole sasa aisee. . Dogo hajafanya fair kabisaUmenikumbusha dogo mmoja nilimkutaga mji fulani kumbe alisomaga na mdogo wangu so yeye akanifahamu mi hata simjui. Basi nikamchukulia kama dogo langu na nikampambania nikampa kazi ofisini kwetu (nilimkuta anafanya kazi ya kutengeneza cappuccino kwenye coffeeshop moja hivi).
Baada ya pale nikahama nikarudi Dar, baada ya 2 years akanipigia kuwa anataka kuja kununua gari nimkonnect na showroom,basi kweli nikampigia jamaa yangu wa show room kuwa mdogo wangu kabisa anataka gari nikampa namba. Dogo kaenda kweli show room kwa jamaa wakashindwana basi dogo akanipigia simu eti ananiwakia nataka kumdalalia, yaani ananiwakia kabisa na akanitangaza kwa wenzake. Nikashangaa sana, sijawahi kusikitika kama siku ile aisee. Hadi leo huwa inaniuma ile kitu
Ni jambo la kihisia mno, jambo lililo ndani ya moyo kabisa lisilotoka na ambalo hujirudiarudia kila Mara!
Ni kuhusu wema uliowahi kutendewa na mtu baki halafu ukaahidi kimoyomoyo kumlipa lakini isiwezekane kwakuwa hujawahi kuonana naye tena au pengine keshafariki.
Nakumbwa na hiyo hali! Namkumbuka mno Dada Jamila Mazoea R.I.P alinipenda sana na kunisaidia katika mengi, lakini kabla ya kuwa na uwezo wa kulipa wema wake kwangu alitwaliwa kutoka katika maisha haya.
Nilichoweza kumsaidia ni mwaka 1993 ambapo nilikutana naye akaniomba sh mia mbili ambayo nilimpa ile ya noti kipindi hicho, baada ya siku ile sikuwahi kuonana naye mpaka mwaka 2010 nilipoenda kwake na kuambulia kuonyeshwa kaburi lake!
Bado namkumbuka dadaangu JAMILA MAZOEA na kwenye
ulimwengu wa roho analifahamu hili
Hahah hawa walikua wakiume tu[emoji23]Unawakumbuka wa wale watoto watatu wa Fatima? Wangali wanaishi hata leo
Touching [emoji22]Kisa cha pili
Nikiwa chuo mwaka wa pili katika chuo nilichokuwepo kulikuwa na utaratibu wa kuomba field katika mtandao wa chuo then unaenda kufanya mafunzo ya vitendo yaani field , katika kufanya hivyo nikapata sehemu niliyotaraji
Ila baada ya huo mtandao kufungwa nikawa nimebadilisha mawazo kuwa niende sehemu nyingine hii kutokana na msukumo wa marafiki na pia kupunguza gharama za usafiri
Basi chuo kilikuwa na utaratibu ikiwa mtandao umefungwa na unahitaji kubadili kituo cha mafunzo inakubidi utafute kituo mwenyewe kwa kwenda kuonana na wakuu wa idara wa hiyo sehemu unataka kwenda uwaombe kufanya field hapo wakikubali wakupe barua , hiyo barua umpatie msimamizi wako wa field
Alafu uende sehemu uliyoomba kwenye mtandao ukutane na mkuu wa hiyo department umueleze kuwa hautaweza kufanyia hapo field sababu ya kuwa unaenda kwingine
Ofcourse nilifanya hivyo ila bahati mbaya sehemu ya kwanza ya field niliyoomba , mkuu wa hiyo department aliniplease sana kuwa ana uhitaji sana na watu wa fani yangu hivyo hakubaliani na maamuzi yangu
Ujana maji ya moto , mimi nikaona ananizingua ikiwa tayari nishamaliza wajibu wangu , hivyo field ilipoanza kwa muda wake mimi nikawa naenda zangu sehemu ya pili nilipoomba kwa mdomo
Later on coordinator wa field ananipigia simu kwanini sijauhudhuria kwenye field nikamueleza kuwa nipo sehemu fulani na barua nishatuma , akasema ikiwa nataka hivyo niende nimalizane na mkuu wa idara wa sehemu niliyoomba mwanzo then anipe barua pia ya kuridhia mimi kutofanya field kwake .
Hilo nilijua lisingewezekana hivyo njia pekee niliandika barua mwenyewe na nikaanza kuusaka muhuri wa ile department kupitia watu wangu wa karibu , badae nikaupata
Nikaenda Temeke nikachonga muhuri wa ile department then nikaupiga kwenye barua nikamtumia coordinator (utoto )
Siku ya assessment coordinator anasema ulinidanganya mbona mkuu wa department ya kule mwanzo hakuwahi kukuona ? Hivyo uliforge muhuri
Nikaona hili ni zali nikakubali kosa ila nikahitaji tuyamalize akakaza
Hivyo field ikaishia pale , tumerudi chuo nasubili what's up mara napigwa na barua ya kikao cha nidhamu
Siku naenda kwenye kikao nakutana na pannel ya madaktari na maprofesa wote wananisikiliza mimi huku nje polisi wananisubili .
After five hours ya kikao , hukumu inatoka kwa upande wa chuo sitakiwi chuo nimedisco na pia nakabidhiwa kwa askari ili waendelee na uchunguzi .
Ni hapo Mungu anamleta profesa mmoja anaikataa hukumu huku akihitaji sababu za yule mkuu wa department kunikatalia mimi kwenda sehemu nyingine hivyo haoni kama kuna sababu ya mimi kudisco na kutoendelea na masomo
Mara pannel yote iko kimya hakuna anayesema chochote , mara mtoa hukumu anauliza wangapi hawakubaliani na hiyo hukumu , bado yule profesa anakuwa upande wangu .
Inapangwa kikao siku nyingine , ni hapo mimi nakabidhiwa kwa askari ila sifiki nao mbali tukiwa njiani wanasimamishwa na gari la profesa aliyenitetea kwenye mataa ya fire hapo kariakoo , anawaomba tuyamalize mimi niwe huru
Note :sikuwa na undugu wowote na yule mzee wala sikuwa chini yake darasani maana hakuwepo kwenye fani yangu
Sikujua ni kiasi gani alitoa ila naambiwa dogo kuwa makini sana , nashuka kwenye difenda napanda kwenye hilux , narudishwa chuo mpaka chumba namba 16 , kwenye ofisi ya huyu mzee anaitaka historia yangu mbali na shule nampa historia anasema toka hapo mimi ni mwanaye .
Kesi iliisha kimya kimya maana sikuitwa tena nikaendelea na masomo
Profesa mawasiliano yaliendelea vizuri japo nilikuja kupoteza simu hivyo ikanichukua muda kidogo kupata namba yake maana alihama chuo na kwenda South africa,,ila usiku mmoja wenye giza nilitumiwa meseji na namba ngeni ya kuwa rafiki yako amefariki akiwa South africa
Inaniuma sana maana sina fadhila niliyolipa kwake hasa alivyonipambania
Kila nikiwaza naumia sana , nimebaki na picha za ukumbusho tu
Bahati mbaya hakuwa na mtoto wala mke
Na hakuletwa hapa Tanzania alizikwa huko
South africa
Natamani hata nilione kaburi lake , niseme asante kwa zile fadhila zake
Kila nikisikia story za chuo basi moyo umkumbuka mzee profesa na machozi hayakawii.
Kwenye huu uzi nimegundua kitu cha kushangaza na kuumiza sana.. Shuhuda nyingi zinaonesha wale waliosaidia kama hawajafa, basi wamepotea ama hawana mawasiliano na hao waliokwisha kuwasaidia🥱Daah imenikumbusha mbali sana mwaka 2012 baada ya kumaliza chuo nilisota sana bila kupata mishe yoyote ila nakumbuka kuna siku nilipata connection ya kazi moja hivi wizara(X)
Kesho yake mchana napigiwa sim na kiongoz wa hiyo sehemu nikaenda baada ya siku kadhaa bila kujua coz tulikuwa wengi ikabdi meza ipinduliwe wakasema tupige paper inatakiwa tuchujwe kuna wengi wanatakiwa waachwe.
Sasa kibaya nikwamba paper inayo pigwa ni tofauti na Maswala ambayo mimi nimesomea duuh na ukumbuke mi nimeconnectiwa tu lakini kazi inayotakiwa kufanywa mimi sijaosomea ni kada tofauti hapo niksema bhaas nishakosa kazi sijakaa sawa tumeingizwa ExamRoom sina nnachojua nakumbuka nilijaza maswali kadhaa tu hata 4 haya fiki baada y hapo chenga kiukweli nilikata tamaa kabsa kabsa akili ikawa inawaza kurud kitaa kuteseka niliumia sana kila nikiwaza.
Nakumbuka kulikuwa na madam mmjoa nishamsau jina ila sitokuja kumsahau yule madam mbaka naingia kaburini ndo alipewa dhamana ya kutusimamia kwa mtihani nakumbuka kila alipokuwa anapita kwangu akiniangalia ananiona kabsa nimekata tamaa mazima coz hata kujaza sijajaza na muda unazidi kwenda zikabaki dkk chachesana na watu wengi walishamaliza na kuondoka nakumbuka tulibaki wa 3 tu na yeye wa 4 .
Sijui ilikuwaje ila yule madam alinionea huruma sana kiukweli aliamua kujitoa na kuvunja dhamana alio pewa na kiukweli alikuja na kuzuga kama anakagua paper zangu na kunitajia majibu sikuamini ile siku niliona miujiza sana kwani alikuja nisaidia dakika za 90 mwisho kabsa kitu ambacho kisheria nikosa kubwa sana ikijulikana kazi hana.
Majibu yakaja kutoka nikiwa sina imani kabsa lakini kati ya watu walio chaguliwa kupita na jina langu lipo kiukweli watu wengi waliachwa nilitamani kulia.
Nikasema nitamfata yule madam sijakaa sawa nikapangiwa kituo cha kwenda kufanya kazi sikuweza kuonanae yule madam sababu muda mwingi alikuwa busy Redcapet ningumu kuonananae nikasema nikirud nitamtafuta kiukweli ilekazi ilinipatia fedha nyingi sana mbaka mkataba unakuja kuisha lakini ghafra mamaangu alikuja kuumwa sana kitu ambacho sikutegemea mbaka akalazwa muhimbili Lkin zile fedha zilinisaidia sana kumuuguza mama mbaka akajakupona sikuamini laiti kama ningekosa ile kazi bas sidhani kama ningeweza kuwa na mama mbaka leo hii.
Nikaja kwenda siku moja kumtafuta kwenye ile ofisi yao kwa lengo la kumlipa fadhira nikaambiwa alishaamishwaga na ata alipoamishiwaga alishaachaga kazi sabau ya kuuguwa aliumwaga na kwabahati mbaya akafariki daah [emoji24][emoji24] naumiaga mbaka kesho wakuu