Nina hakika hili lilishakutokea hata wewe

Nina hakika hili lilishakutokea hata wewe

Nilienda kumtembelea rafiki yangu kijiji fulani kilometa 20 kutoka katikati ya jiji sasa jirani kwenye kaya masikini sana nikakuta kuna mgogoro kijana yuko form four shule ya kata hataki shule yaani anataka kubaki mtaani akae vijiweni eti anasema shule ngumu na haelewi chochote. Dogo alikuwa anagombana na baba yake basi nikaomba kukaa na yule dogo nikajaribu kuongea naye kwa dakika 30 then akakubali kuendelea na shule.
Sasa mwaka mmoja badae niko ofisini mjini kati nikaambiwa kuna mgeni wako. Nikatoka kwenda kwenye benchi nakuta mzee simjui yeye akajitambulisha na kunikumbusha kuwa mtoto wake alikataa shule ba alikataa ushauri wa ndugu wote mimi nikaongea naye akakubali kurudi shule sasa yule kijana alifaulu kwa division three na akapata post ya chuo ngazi ya diploma ya miaka mitatu.
Sasa mzee alitembea kilometa 20 kuja kunishukuru na alinipa shilingi Mia tano (500) kama shukurani maana ndio aliokuwa nayo siku hyo. Kwa kweli nilijizuia kulia mbele yake nilikataa ile Mia tano lakini mzee alinisuhi sana niichukue.
Nikagundua huku duniani unaweza kuona umetoa msaada mdogo sana lakini kumbe umegusa maisha ya mtu sana.
ANGALIZO: Tusisahau matapeli pia wapo, tuwe macho.
Sasa mzee alitembea kilometa 20 kuja kunishukuru na alinipa shilingi Mia tano (500) kama shukurani maana ndio aliokuwa nayo siku hyo. Kwa kweli nilijizuia kulia mbele yake nilikataa ile Mia tano lakini mzee alinisuhi sana niichukue. [emoji848][emoji2827][emoji1752]
 
Kuna sehemu nimewahi kufanya kazi 2007-2008. Boss wangu alikuwa kila siku anatusisitiza nendeni mkaongeze elimu sisi wengine tumekaribia kustaafu na akituona kila siku ni madongo tu kwamba vijana nyie hapa mnapoteza muda tu. Kuna namna alitupambania mpaka mambo ya kawa sawa na tukaondoka na kazini tuliondoka watatu kwenda kusoma. Sasa mambo yanasonga juzi napiga story na jamaa mmoja ambae ndio tulitoka wote kwamba tumpelekee yule mzee zawadi, kuja kufuatilia ili tupate namba zake tukaambiwa amefariki mwaka huu mwezi wa 6. Dah inauma sana.
Nyaishozi sekondari??

Sent from my SHV45 using JamiiForums mobile app
 
Kuna watu dunia hapa Mungu awape maisha marefu.

Mwaka huu mwezi wa tano nikiwa natoka kwenye mishe zangu niko na pikipiki langu kuna jamaaa hata sijui alinigonga vip kwa nyuma na pikipiki lake nilipata ajali mbaya sana nilizimia pale sikua naelewa kitu chochote nimekuja kuzinduka niko hosptali sielewi hata nimefika vip hapo hosptali ..inshort nilikua km naona ni ndoto baada ya kupata hudum na akili yangu kukaa sawa ikabidi niulize nimefika vip pale.

Ndio yule doctar akasema pumzika kwanza ila nikawa namsisitza sana aniambie ni nn kimetokea mpaka mm nimefika hapo ndo akaniambia kuna watu wamekuleta hapa na gari umepata ajali na walifanikiwa kupata simu yako wamewapigia watu ulio andika jina kaka wamewapata ..kaka zako wanakuja.

Mm roho ikatulia maana nikua siko sawa plus nilikua na maumivu makali sana mwilini nimekuja kupata nafuu sasa ndo nikapata mkanda mzima.

Nilipo pata ajari watu walikua wanapita tu na magari wakiogopa kunibeba maana nilikua natokwa na dam nyingi sana mwilini kwa hiyo wakawa wanasema nitachafua gari lakin kuna huyo bro wala simjui mpaka sasa ndo alikubali kunibeba kwenye gali lake docta anasema gar lake siti ya nyuma nilichafua sana na dam na bado huyo ndo aliitumia simu yangu ndogo ambayo vibaka hawakuniibia maana simu kubwa na hela waliiba pale ndo aliitumia kuwapigia ndugu .Docta anasema jamaa alikataa kuacha no yake akasema mm shida yangu ni huyu dogo afike sehemu apate huduma.
Brooo popote ulipo Mungu akuongezee na akupe Afya njema ww na kizazi chako [emoji2972]
Duh Huyo jamaa ni mwema sana
 
Nilichojifunza katika maisha always be humble kila kitu ulichonacho sio kwa akili na ujanja wako ila ni Mungu tu, kama alivyokupa pia anao uwezo wa kuchukua vilevile.

Nimeguswa na naomba ni share na mimi, japo kwa macho ya kawaida ni tukio dogo lakini amini wema wowote unaomtendea mtu basi unamkopesha Mungu.

Tukiwa kwenye mahafali ya kidato cha nne miaka kadhaa huko nyuma kuna jamaa yangu mpaka leo hiyo picha ninayo. Katika lile kundi la marafiki wote kwake tu mambo ndio hayakua mazuri sababu kubwa baba yake mzazi alikua ameoa mke mwingine hivyo wao wakawa wamesahaulika kabisa.

Enzi hizo wakuu form 4 ni form 4 kweli. Hivyo katika maandalizi tukawa tumepanga nguo kali za kununua, viatu n.k jamaa nae kwenye kundi ili asionekane mnyonge akawa anachangia mawzo nguo za kununua ili asibaki nyuma.
Siku tuliyokubaliana kwenda shopping jamaa akawa haonekani, tumemtafuta lakini wapi mwisho tukaenda wengine kama kawaida enzi hizo t-shirt na jeans na raba kali ndo ilikua unyama.
Tupo kwenye maandalizi kama kesho kutwa ndo mahafali nikakutana na dogo wa jamaa angu akanimbia bro haji kwenye mahafali mzee kamnyima ela ya nguo na viatu na mama kamwambia hana pesa.
Kwetu mambo hayakua mabaya wala mazuri sana tulikua familia ya daraja la kati hivyo kila sikukuu tulikua na uhakika wa kuvaa nguo mpya na viatu vipya kila sikukuu.

Kwa kujisikia vibaya jamaa alikua anajificha na kutukwepa ila kesho yake nilimvizia anakoenda kushinda nikamchagulua jeans, t-shirt na raba kali japo nilikua nilishazivaa tayari ila zilikua kama mpya, na nilimpa kimya kimya bila kumuambia mtu yoyote na hata siku ya graduation hakuna aliye notice chochote, tulipiga picha ya pamoja wana wote na mpaka leo ninayo.

Miaka kadhaa mbele mawasiliano yakiwa yamepungua kutokana na mishe mishe halafu jamaa alioa mimi sijao so tukawa wana ila sio kivile kama zamani. Mimi nilisoma mpaka ma vyuo vikuu huko yeye kutokana na life la msoto akaingia ku hustle kitaa mwisho wa siku Mungu sio Mandonga jamaa akatoboa, sasa na mimi ile ndo nimemaliza mambo ya kusoma nikaenda mkoa flan kucheki harakati mara nakutana na jamaa afu hapo katikati mawasiliano yalipungu mwisho yakafa kabisa, bahati nzuri jamaa alinikumbuka, jamaa alinisaidia sana kwenye mambo yangu mengi sana kuanzia kwenye michongo, mawazo hadi financial sababu yeye alikua ameshatoboa maisha tayari.

Aliniambia mwanangu siku ile uliponipa nguo zako nilikuona zaidi ya baha yangu mzazi hasa ukizingatia sikukuomba wala nini, usiku nililia sana yani nina baba mzazi, baba mdogo wengi tu lakini hakuna anaenithamini hata kidogo na sio kwamba pesa hawana, nilijiapiza siku moja lazima nilipe wema wako na nikakuchukulia kama ndugu yangu wa damu kabisa.

Lile jambo kwangu niliona kawaida na vile sijuagi kudai zile nguo nilimuachia kabisa sababu alichelewa kunirudishia sijui alikua anaona aibu au vipi. Ni kitendo cha kawaida lakini kwake alikipa uzito mkubwa sana, mpaka sasa bado tu wana na jamaa ananiamini sana kwa sababu katika michongo na vitu vingi alivonisaidia sijawahi kumuangisha wala kumharibia chochote.

Narudia tena wakuu, Wema ni akiba, ukipata nafasi ya kutenda wema hata kama ni mdogo kiasi gani wewe fanya ipo siku Mungu atakulipa. Wakati mwingine mambo yetu yanaenda sawa kwa sababu ya maombi ya hao tuliowatendea mema.
Amina mkuu, ubarikiwe kwa wema ulioutenda. Kwa kawaida maisha haya tunayoishi hatuwezi kujua kesho yetu itakuaje na ni Mungu pekee ndo ajuaye kesho yetu na anatulipa kwa wema tunaoutenda hata kama ni kidogo kwa namna ya pekee kabisa
 
Mimi nachokumbuka nikiwa mwanafunzi wa chuo kimoja huko mkoa wa nyanda za juu kusini.

Chuo chetu kina hospitali ya rufaa hivyo kuna mwanamke alikuja chuoni na mtoto mgongoni akiomba uongozi wa chuo umsaidie ili aweze kupata wanafunzi wa kwenda kumsaidia mwanae aweze kupata damu kwa ajili ya blood transfusion uongozi wa ulikataa.

Hapo ndipo mimi na mwenzangu ikabidi tumfuate yule mama mwenye mtoto wodini aliko na kumwambia tutakutolea damu ila tunaomba iwe siri .kiuhalisia ikawa ndo tabia yetu tunapokezana kila baada ya miezi mitatu anaenda mwingine kumtolea damu .

Mtoto wake alizaliwa na kidonda hivyo ilibidi afanyiwe skin graft na zilikuwa zinakataa zaidi ya mara 3 mara ya nne ikakubali na yule mama wa mtoto alikaa hospitali miaka miwili hadi muda anaondoka aliweza kujipatia ndugu na marafiki wengi sana hadi leo nawasiliana nae.
Aiee mungu akubariki kwa kweli umekuwa muungwan mno
 
Nakisaidia hua nasahau kabisa.

Sitakiwi kukumbuka,ikiwa Mungu amenifanyia mengi mema makuu.
Kwanini mimi ni nani ama ni bora kuliko wengine?lah!
Ni baraka tu za Yehova.
Una sahau kwa njia ipi? Kweli ufanye Jambo fulani halafu usahau? Tufundishe mkuu jinsi ya kusahau pia
 
Amina mkuu, ubarikiwe kwa wema ulioutenda. Kwa kawaida maisha haya tunayoishi hatuwezi kujua kesho yetu itakuaje na ni Mungu pekee ndo ajuaye kesho yetu na anatulipa kwa wema tunaoutenda hata kama ni kidogo kwa namna ya pekee kabisa
Amen ubarikiwe pia mkuu
 
Nakumbuka siku moja jioni ya saa 1 nilimsindikiza rafiki yangu mahali alikuwa na kikao cha chakula cha jioni hoteli flani.
Nilipofika karibu na hiyo hotel nili park pembeni ya barabara kuu ili kumshusha.

Wakati nimesimama kuna gari iliingia road kwa speed sana kutokea ile hotel na kuivaa pikipiki ambayo ilimbeba binti flani wa umri wa miaka 23.

Jamaa alupoona ameginga alikimbia sana lkn kuna pikipiki ilimkimbiza kwenda kusoma namba.

Mimi na yule rafiki yangu tulielekea kwenye eneo walipogongwa wale watu na binti alikuwa na hali mbaya yaani anarusha miguu kama vile anakata roho.

Kwasababu mimi nilipark karibu na tukio kuna raia walifikiri kuwa gari yangu ndio imewaginga lkn kuna watu wakasema aliyegonga amekimbia.

Watu wakaanza kushikiniza nimbebe haraka kuwahi hospital lakini niliwaambia wasubirie nitoe taarifa polisi ili yasijekunigeukia mimi


Baada ya kutoa ripoti polisi ndipo nikaomba msaada wa kumbeba kwani kwa alivyokuwa ilikuwa inaogopesha kulihitajika umakini kumbeba...cha ajabu watu wote wakawa wanarudi nyuma kukwepa kumbeba.

Nikajikuta ninashout kuwa mmejaa bure hamna msaada mnachonga tu hapa.
Nilimshika jamaa mmoja kwa nguvu...njoo tumbebe pamoja na yule rafiki yangu.

Kweli tukambeba na tukaondoka wote na watatu na mgonjwa wa 4 lkn dereva boda hakuumia sana na aliposikia tunaenda polisi badala ya kupanda gari alikimbia.

Polisi tukapewa pf3 na kuelekea hospital.
Nilipofika nikapewa gharama nikalipia na kuhakikisha amewekewa drip na mengine yakaendelea.

Kilichosaidia zaidi yule jamaa niliyemlazimisha kubeba na tukaenda naye alikuwa anamfahamu kwa sura na alimfahamu rafiki yake flani.
Ndipo akaanza kupiga simu mtaani kwao hadi rafiki yake akaja.

Muda huo ilishafika saa 7 usiku nikawaaga rafiki zake na kuwaachia namba kuwa watanijulisha maendeleo.

Baada ya miezi 8 nilipokea simu toka huyo binti.

Akajitambulisha kuwa; kaka mimi naitwa Given.
Tarehe flani nilipata ajali na nilipopona niliambiwa kuwa ulifanyika msaada mkubwa sana kwangu.

Plz naomba nikufahamu.
Kweli tulipanga na tukaona, binti alinishukuru mnoo.

Akawa ananipigia kila mara.
Kuna wakati nikao ana kila dalili ya kunipa shukrani na alianza kutamka; kaka kama inawezekana iwe.......[emoji849]

Wazee wa Cuba mtanielewa.
Ndipo taratibu nikampotezea kwani nilimsaidia sio kwa kusudi lolote bali niliona kuwa nilifanyika mkono wa Mungu kwa kutoa msaada na nisije kubeba utukufu wa Mungu nikaadhibiwa.

Given popote ulipo uishi maisha marefu mdogo wangu
Ubarikiwe sana kwa moyo huo
 
Uzi wa mshana umeni touch sana saa saba hii usiku nmeona niandike kitu
Mzee wangu alioa wake wawili mamaangu mimi akiwa ni bi mdogo na wote kwa pamoja waliishi nyumba moja ispokua kila mtu alikua na upande wake wa nyumba

Nikiwa darasa la kwanza sitokuja kusahau nilipatwa na malaria hivyo sikuweza kwenda shule kwa siku kadhaa nilishinda nyumbani na mama zangu ambao wote walikua ni kina mama wa nyumbani

Sasa sku moja nikiwa nishaanza kupata nafuu nje ya nyumba yetu kulikua na tanki/karo la maji lililofunikwa na mabati na juu kuwekewa mawe ili mabati yasibebwe na upepo nikaona maji yamejaa kwenye lile Karo mpk yanamwagikia kwa nje, kwa akili zangu za utotoni niksogea karibu ili nitoe ule mpira ulikua unatoka bombani kuingia kwenye tank

Bahati mbaya nikahisi kizunguzungu na kuangukia kisimani,mama zangu wote wawili walinishuhudia nilivyotumbikia lakini mamaangu mzazi akapigwa na butwaa yani akawa Kama ameganda basi huyu mamaangu mkubwa akawahi akajakuingiza mkono kwenye kile kisima akanishika mkuu maana tayari nilikua kichwa chini miguu juu nazama

Akaniopoa tayari nikiwa sijitambui wakanipa huduma zote nikatema maji ya kutosha namshkuru Mungu mpk leo nipo na huyu mama mkubwa alieniokoa nmetoka kumkumbusha hiki kisa juzi tu juu ya wema ambao siwezi kuusahau alowahi kunifanyia.

Mungu awape maisha marefu wazee wetu.
 
.
 

Attachments

  • FB_IMG_1668588122082.jpg
    FB_IMG_1668588122082.jpg
    57.3 KB · Views: 25
Mkuu duuuuh! Umenigusa sana

Kuna kaka mmoja (mkubwa sana kwangu) ni engineer wa mabarabara kama sikusei namtafuta japo nitamke neno Asante tu!

What he did in my life made me who I am today! Kibaya zaid sikuwah hata kulijua vizur jina lake (kitu kama BURHANI MUSSA kama sijakosea) nakumbuka sura tu ndo Huwa hainitoki, ndani ya siku 5 tu hardly 5 alibadilisha historia nzima ya maisha yangu!

Jaman ni hadithi ndefu, ila huyu kaka namtafuta mno, hadi mme wangu ameona aanze kunisaidia!
ulifanikiwa kumpata?
 
Kuna siku natoka mihangaikoni saa 5 usiku nipo kituo cha boda jamaa ananiambia mpaka home elfu 7, hela nilikua nayo ila nikawa na burgain kwa elfu 5, ajabu pembeni kulikua na jamaa mlevi haswa tena wale wa pombe chafu waliochoka wasio na makazi wanaolala nje akaja akampa boda buku mbili akamwambia dereva mpeleke braza akapumzike. Ilinifikirisha sana na kunipa mtazamo mpya juu ya watu tunaokutana nao.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom