Aisee! Imeni touch sanaKuna siku natoka mihangaikoni saa 5 usiku nipo kituo cha boda jamaa ananiambia mpaka home elfu 7, hela nilikua nayo ila nikawa na burgain kwa elfu 5, ajabu pembeni kulikua na jamaa mlevi haswa tena wale wa pombe chafu waliochoka wasio na makazi wanaolala nje akaja akampa boda buku mbili akamwambia dereva mpeleke braza akapumzike. Ilinifikirisha sana na kunipa mtazamo mpya juu ya watu tunaokutana nao.
Ni kaka wa field au?Mkuu duuuuh! Umenigusa sana
Kuna kaka mmoja (mkubwa sana kwangu) ni engineer wa mabarabara kama sikusei namtafuta japo nitamke neno Asante tu!
What he did in my life made me who I am today! Kibaya zaid sikuwah hata kulijua vizur jina lake (kitu kama BURHANI MUSSA kama sijakosea) nakumbuka sura tu ndo Huwa hainitoki, ndani ya siku 5 tu hardly 5 alibadilisha historia nzima ya maisha yangu!
Jaman ni hadithi ndefu, ila huyu kaka namtafuta mno, hadi mme wangu ameona aanze kunisaidia!
Poapoa mkuuHakuna shida mkuu kila mmoja umekuja kwa wakati wake japo maudhui yanafanana
Dah mkuu mungu awe nasi daimaNami niweke kisa changu japo ni chakawaida lakini kwangu ni moja ya tukio ninalo dumu nalo kwa kumshukuru sana Mungu kwaajili ya huyu ninaemzunguzia hapa.
Mwaka 1992 nilikua nakaa na bibi baada ya wazazi kufariki mwishoni mwa miaka ya 80.
92 hio bibi alipata shida ya macho na hakujaliwa kuona tena mpaka anakufa .
Mzazi wangu alikufa alikua ni mwanae wa mwisho 3 kufariki hivyo akawa hana msaada kwa chakula na mahitaji mengine ya kibinadamu.
Ilibidi awe ananituma mimi kuomba kwa majirani chakula, leo huku kesho kule mpaka 96 nilipopata nguvu kidogo nikawa naanza kufanya vibarua vya hapa na pale napata mia, mia mbili na wakati mwingine mia tano.
Ilitusaidia kununa mboga , kusaga mahindi, na vitu vidogo vidogo vya kutuwezesha kuishi.
Hii ilienda nikiwa nimetenga siku za kwenda shule , Jumatatu naenda jumanne naenda kibaruani jumatano shule alhamisi kibaruani ijumaa shule jumamosi kibaruani jumapili kanisani.
Kwa mfumo huo ndio nienda kupausua kokoto mahali mbali kidogo tokea asubuhi mpaka saa tisa alienipa kazi hajatokea, njaa inaniuma Sana hata kunyanyua nyundo nikashindwa, lakini mawazo yote yapo kwa yule bibi ambaye tokea jana hajala kitu na hapo alipo hawezi kusogea hata hatua moja.
Ilinibidi nitoke hapo niende kwa baba mmoja aliekuwa anatufahamu kwa lengo la kumuomba kazi yoyote hata nipate 500 tu nirudi nyumbani nikanunue chochote, bahati mbaya sikumkuta ila watoto tuu, niliwaambia shida yangu lakini hawakuwa na lakunisaidia .
Ilibidi niwaombe malimao nile maana ile njaa ilioniuma siku ile mwaka 97 mpaka leo naikumbuka.
Nilikula yake malimao nikapata nguvu kurudi nyumbani km kama 7 hivi, huku sijui itakuwaje kule nyumbani.
Lakini ile nafika tu saa 12 bibi ananiuliza nimefanikiwa chochote maana njaa inaniuma mno, chozi lilipotokea hata sijui.
Lakini nikasikia mlio wa gari yule baba akaja mpaka nyumbani ana unga sukari na mchele, hata nguo hakubadilisha alipoambiwa na watoto kwamba nimekuja na nimeomba kibarua, alishindwa kuvumilia hata kuingia ndani ilibidi aje atuletee chakula.
Hilo tukio ni moja ya matukio ambayo yananipa faraja sana kwamba Mungu yupo na nisikate tamaa hata kama jua limezama chochote kinaweza kutokea.
Nilipika kile chakula lakini nilishindwa kula ila bibi alikuala, shukrani niliompa yule baba mpaka leo sioni kama inatosha, yeye pengine aliona ni kawaida lakini mpaka sasa ni miaka 25 sasa sijasahau na sita sahau zaidi ya kushukuru na kuwa msaada kwa wengine.
Wema ni akiba ndugu zangu tena akiba isio na mfano.
Lakini pia kushukuru ni kwema mno.
Dah pole sana mkuuKuna siku natoka mihangaikoni saa 5 usiku nipo kituo cha boda jamaa ananiambia mpaka home elfu 7, hela nilikua nayo ila nikawa na burgain kwa elfu 5, ajabu pembeni kulikua na jamaa mlevi haswa tena wale wa pombe chafu waliochoka wasio na makazi wanaolala nje akaja akampa boda buku mbili akamwambia dereva mpeleke braza akapumzike. Ilinifikirisha sana na kunipa mtazamo mpya juu ya watu tunaokutana nao.
Jaribu sasa hivi mkuuKaka sikupati hewani
So touching to me this.Nikiwa nimemaliza chuo niliamua kwenda mkoa X kujifunza maisha nje na shule.
Nilibahatika kupata marafiki wengi na uzoefu wa biashara ila sikuweza kukaa sana baada ya kuamua kurudi jiji kuu kuendelea na mishe nyingine.
Ila ninachokumbuka nikiwa mkoa ule kuna mdada mmoja alitokea kunipenda na akanieleza hisia hizo mbele yangu ila kutokana uzoefu wa kuambiwa maneno hayo na wanawake kwa muda mrefu nilimpuuzia na ukizingatia nimetoka shule hata kuna muda maisha siyaelewi hivyo mapenzi kwa wakati huo hakikuwa kipaumbele hivyo sikumwambia kwa mdomo ila kwa vitendo nadhani alielewa.
Nikiwa nimerudi mjini yule dada alionyesha kila dalili za upendo ila alingonga mwamba nachokumbuka nikiwa nampango wa kufanya biashara ya kuuza viatu nilimwelekeza kiutani nikiwa nahitaji mtaji kama wa laki mbili ndani ya dk 10 kwenye simu yangu ikaingia laki 2 kutoka kwake akinisisitiza nifanye biashara niizalishe hiyo hela na nimrudishie kiukweli sikumrudishia na tukaachana kwa ugomvi.
Wema wake haukuondoka moyoni mwangu na hapa katikati nikapita na wanawake sikupata tena kama yeye ninavyoongea leo ndo mtu ninayeishi nae na ninasubilie ikimpendeza Mungu aniletee kiumbe.
Uwa namuuliza ile laki 2 bado unanidai.