Mwaka 98 nikiwa darasa la nne pale shule ya msingi Mwananyamala Kisiwani. Siku moja tukiwa tupo mapunziko yale ya saa nne, mimi na wenzangu tulienda nyuma ya Shule kwaajili ya kununua vitu mbalimbali ili kulituliza tumbo kutokana na njaa. Nakumbuka siku hiyo nilikuwa na njaa sana hivyo nikaona ili kuituliza ninunue viazi vitamu vya kukaanga. Kipindi hicho kiazi kimoja Sh 50, kwa kuwa nilikuwa na sh 200 hivyo nikanunua viazi vitatu kisha nikabakiwa na sh 50 kwaajili ya kununua barafu la kwenda kulia darasani. Kwa bahati mbaya vile viazi vilifungwa kwenye gaazeti, na kutokana na mchuzi kuwa mwingi lile gazeti lilichanika na hatimaye viazi kuanguka chini sehemu chafu. Kutokana na njaa niliyonayo nikasimama pale huku nikifikiria niviokote ama niende darasani!!!? Wakati naendelea kiwaza namna ya kufanya akatokea mkaka hivi na kunambia dogo achana navyo hvyo chukua hii 500 ukanunie vingine. Kitendo hiki mpaka leo hakitoki kichwani mwangu na kimeniathiri kiasi kwamba ninapokuwa na niko vizuri kisha nikaona watu wanagombana kwa kudaina pesa ambayo naweza kuimudu kuilipa basi ni heli nimlipie mdaiwa kisha maisha yaendelee.
Yaani kiufupi huwa sipendi kukutana na mtu anataabika njiani, kama ninauwezo wa kumsevu huwa nafanya hvyo. Yule jamaa simkumbuki hata kwa sura.
Ila ninachoweza kukitolea ushuhuda ni kwamba ukiwa na tabia ya kusaidia watu kwenye matatizo bila kutarajia malipo, basi nawe utajikuta ukipata msaada kwenye magumu bila kutarajia ulipotokea.