Nina elimu na maisha yananipiga, wapi nimejikwaa?

Nina elimu na maisha yananipiga, wapi nimejikwaa?

Umetoka fresh from college huna hata mia...wazazi washakutema uwez kuwakamua hela tena wanasubr wakukamue wewe hela zao za kukusomesha....ajira za tabu....demu wako anataka matumizi coz anajua aftr college unaingia ofisini...lazima udate aiseee.....ila ni kumuomba Mungu ni kipindi kigumu sana kushinda hata kile cha kufeli form4.....
 
Jibu maswali yafuatayo ili tuone tatizo lako liko wapi hadi ukose ajira.

1) Unasema umesoma, je, ni kwa kiwango gani? Form 4, Form 6, Degree, Masters, PhD au Professa?

2) Umesomea taaluma/ujuzi gani na ufaulu wako ukoje?

3) Kazi unazoomba ni za taaluma/ujuzi uliyosomea?

4) Umehitimu lini?

Ukijibu maswali haya tutajua ni kitu gani kinakufanya ukose ajira. Pengine elimu ni ndogo au kubwa sana? Pengine taaluma haina soko au GPA ndogo? Pengine unaomba kazi na taaluma tofauti? Inawezekana umehitimu mwaka jana tu halafu kelele nyingiii?

Mshua
 
Leo najuta ni kwanini nilikazana kwenda shule.

Matokeo yake nimefika mwisho kazi sijapata na interview kibao nimefanya lakini hadi leo bado sijafanikiwa.

Cha kushagaza zaidi yale ambayo nimefundishwa shuleni hayafanani hata kidogo na jamii yangu.

Bora hata nigesoma namna ya kuwatuza kondoo nigefaidika sana

Kwa sasa sizani kama mtoto wangu nitakubali afundishwe na mfumo na mitaala kama hii.

Kaka pole kwa mwendo huu wa kuandika ELEMU, SIZANI sijui kama kuna kitu unaweza kufanya hapa duniani achilia mbali kujiajiri labda uajiriwe.Habari ya KUTUNZA kondoo hakuna mwenye kondoo atakayekupa utunze kwasababu kondoo wanafugwa. Pia acha kusingizia umesoma mpaka mwisho. Nionavyo mimi unatudanganya au unajidanganya tuu hapa, wengine mlienda shule mkaishia kukaa kwenye madawati na vimbweta na kusoma madesa mkamaliza chuo mkaona mmesoma. Wengine mnakimbizana na Masters za coursework mnasema mmesoma mnadhalilisha neno kusoma. Acheni kusingizia kusoma nyie ni veta tu "Nowadays Universities are but Glorified VETA"( Chachage 2001). So usituzingue tuache tuliosoma tujenge taifa
 
The truly educated never graduate na elimu ina umuhimu wake.....ndugu kupata elimu kwa kiwango ulicho fikia(haijalishi kipi) ni jambo la kumshukuru sana Mungu....Maana wapo pia wanodhani kukosa kwao elimu ndio chanzo cha umasikini wao,ili hali sivyo.

Na tushukuru kwa kila jambo basi,amini ya kuwa Mungu amekuandalia mema mbele.Na kamwe usimtegemee mwanadamu(maana sote tunashida tofautitofauti).Tumtizamie Mungu pekee!
 
kuna rafiki yangu tokea
1.primary......amesoma international skul....
2.o..level education amesoma loyola..... ......
3.advance level......amesoma feza boys..........
4.chuo amesoma oxford university uingereza ................

Gharama za kusoma ukijumlisha ni mamilioni...50 .alikaa mtaani miaka 7 bila kazi ....hadi alitamani kujiuwa....ila mungu yu mwema saivi amepata job bot mungu yupo ongeza maombi

Huwa nawashangaa sana wazazi wanaotumia hela nyingi sana kusomesha watoto wao nje ya nchi, ni bora hata wangewasomesha hapa Tanzania na hizo hela wawatunzie ili wakimaliza chuo waje kuanzisha hata biashara.
Ufahari unaangamiza familia nyingi sana
 
the best people always get job, try to find what is wrong with you! anza na kuchek jinsi unavyooandika cv, interview jinsi unavyojieleza nk maana kama ulisoma ukapata cheti tu kupata kazi ni ngumu!
 
Back
Top Bottom