Nina elimu na maisha yananipiga, wapi nimejikwaa?

Nina elimu na maisha yananipiga, wapi nimejikwaa?

Mleta mada kweli we umevurugwa na maisha´

Hebu tuamibie umewahi kufunga na kuomba mara ngapi juu ya shida yako? Una uhakika Bwana Yesu umemshirikisha ktk shida yako? Daudi wa kwenye Zaburi anasema sitautumainia upanga wangu wala mkuki wangu hautaniokoa, sasa wewe mwenzetu je unatumainia vyeti vikuokoe kabla ya kumshirikisha Mungu awezaje mambo yote?
 
Leo najuta ni kwanini nilikazana kwenda shule..!
matokeo yake nimefika mwisho kazi sijapata na interview kibao nimefanya lakn hadi leo bado sijafanikiwa..!
cha kushagaza zaidi yale ambayo nimefundishwa shuleni hayafanan hata kindogo na jamii yangu.
bora hata nigesoma namna ya kuwatuza kondoo nigefaidika sana
kwa sasa sizani kama mtoto wangu nitakubali afundishwe na mufomo na mitahara kama hii.

ELIMU..!?.! MHMMM.

Pole sana, ulisomea taaruma gani? kwanza nikupe hongera kwa kuwa unaitwa kwenye interview ila una upungufu ndani yako hasa uelewa wa fani husika unapoitwa kwenye interview, na hiyo ni sababu ya mfumo wa elimu ya kibongo wanafunzi wengi hawawezi kujieleza hata km wana GPA kubwa, kwaani elimu ya kibongo tunasoma ili tufaulu mitihani, mfano course work inakuwa na mark 40% including test 30% na assignment 10% (10% ndiyo ina presentation skills) tena mara nyingi wanafunzi wanadesa yaani copy and paste assigment za watu na mwalimu hana muda wa kuziangalia au kusimamia presentation, mwanafunzi akimaliza coursework anasuburi final exam 60%. sasa hapa tunategemea nini? uwezo wa kujieleza tena kwa kidhungu mbele ya maboss watarajiwa itatoka wapi? Kuna jamaa yangu alikuwa kusoma huko nje miaka ya nyuma alinieleza kuwa coursework ni marks 80% yaaani ikifeli presentation huwezi fanya final. final exam inachukua mark 20% na walimu wanasimamia presentation na project kwa saana na mara nyingi wanafanya practical e.g wanaenda kutembelea taasisi fulani au kiwanda wakirudi wanaandika paper na individual presentation, wanapigwa maswari na wanajenga hoja kwa muda wa miaka 3 mwanafunzi anamaliza akiwa vizuri.

USHAURI:
1. Tafuta wazoefu wakuelekeze kabla hujaenda kwenye interview husika. na zaidi soma jinsi ya kupambana na waendesha iinterview kwa sababu wao wanakuwa wamejipanga.

2. ungeweza kujipanga kufanya shughuru zako lkn najua tatizo litakuwa mtaji lkn pia sijui km una skill za business kwa sababu nayo ni taaruma.
 
Muhubiri 9.11 inasema NIKARUDI NA KUONA KUWA CHINI YA JUA SI WENYE MBIO WASHINDAO KATIKA MICHEZO WALA SIO WALIO HODARI WASHINDAO KTK VITA WALA SIO WATU WENYE UFAHAMU WAPATAO MALI WALA WENYE USTADI WAPATAO UPENDELEO. LAKINI WAKATI BAHATI HUWAPATA WOTE. MAANA MWANADAMU NAYE HAJUI WAKATI WAKE KAMA SAMAKI WANAVYOKAMATWA KATIIKA NYAVU MBAYA NA MFANO WA NDEGE WANAONASWA MTEGONI. .
 
I dont see the relation btw education and life success
 
Muhubiri 9.11 inasema NIKARUDI NA KUONA KUWA CHINI YA JUA SI WENYE MBIO WASHINDAO KATIKA MICHEZO WALA SIO WALIO HODARI WASHINDAO KTK VITA WALA SIO WATU WENYE UFAHAMU WAPATAO MALI WALA WENYE USTADI WAPATAO UPENDELEO. LAKINI WAKATI BAHATI HUWAPATA WOTE. MAANA MWANADAMU NAYE HAJUI WAKATI WAKE KAMA SAMAKI WANAVYOKAMATWA KATIIKA NYAVU MBAYA NA MFANO WA NDEGE WANAONASWA MTEGONI. .
Matola umemaliza, hata nikiwa na uchungu moyoni kiasi gani, au nimekaa chini kwa kukata tamaa,........nikiwaza andiko hili huwa napata nguvu na kusonga mbele, halafu namalizia kwa "USIKU UMEENDELEA SANA, KUCHA KUMEKARIBIA" Thumb up guy
 
Last edited by a moderator:
Leo najuta ni kwanini nilikazana kwenda shule..!
matokeo yake nimefika mwisho kazi sijapata na interview kibao nimefanya lakn hadi leo bado sijafanikiwa..!
cha kushagaza zaidi yale ambayo nimefundishwa shuleni hayafanan hata kindogo na jamii yangu.
bora hata nigesoma namna ya kuwatuza kondoo nigefaidika sana
kwa sasa sizani kama mtoto wangu nitakubali afundishwe na mufomo na mitahara kama hii.

ELIMU..!?.! MHMMM.

Daudi Kipara
Najua hata nikikupa pole haitabadili situation uliyonayo, elimu ya kwetu haimsaidii mtu kukabiliana na mazingira zaidi ni kufaulu mitihani tu BRN, madhara yake ndio haya, ni kweli ungesoma kufuka kondoo ungekuwa umefanya la maana sana na wala usingekuwa unalaumu zaidi ungekuwa unafikiria jinsi ya kukuza mtaji, Je wajua kondoo aina ya merino wanauzwa bei gani sokoni? fanya utafiti jibu lake utashangaa
Nakumbuka mie nilikataa kabisa kuendelea na masomo sijui mnaita degree, 0 au master degree nikafuata kusomea kitu roho yangu inapenda ufundi, japo wazazi walinipinga sana kwa kila namna ila hawakuweza kuzima ashki ya moyo wangu.
Kwa sasa ndio wanatambua nilikuwa na uamuzi sahihi,, na wala sijutii hilo
Simaanishi kusoma sio kuzuri ila kusoma kusikokuwa na mapenzi ndani yake ni tatizo kubwa sana
 
Elimu ni ufunguo wa maisha....tafuta kufuli la maisha lilipo ufungue uingie.
 
tatizo lenu mnataka kusoma alafu wote mnataka kuwa katika maofisinI.....jaribuni kuangalia fursa zingine jaribu kubuni mradi wako ujiajiri.tusipende wote kungangania mijini tunazidi kubanana tu,
 
Pole yako,YAANI UMEPATA ELIMU UNAJUTIA??????????? Jaribu kukaa chini omba msamaha kwa Mungu wako alokuwezesha kupata elimu. Halafu jaribu kuangalia changamoto zinzokukabili wewe na jamii inayokuzunguka ili uzibadilishe zile fursa na wewe uweze kutoa ajira. Mfano kama mtaani kwenu kuna takataka nyingi na haziondolewi na magari ya jiji au mji uliopo. Wewe anza kuzikusanya nyumba tu nyumba na uwatoze pesa kasha peleka dampo utapata pesa na baadae jaribu kutafuta sehemu zenye semina ya ujasiriamali wa kutengeneza mkaa kupitia takataka zitokazo majumbani then utengeneze mkaa kwani una soko kubwa sana hapa Tanzani.
 
Kama elimu uloipata haiajakusaidia, nakushauri urudishe vyeti vyote ulivyonavyo kwenye taasisi/chuo/shule husika, au uvichome moto.... Hapo ndo utaona mwanzo wa mafanikio yako!
 
kuna rafiki yangu tokea
1.primary......amesoma international skul....
2.o..level education amesoma loyola..... ......
3.advance level......amesoma feza boys..........
4.chuo amesoma oxford university uingereza ................

Gharama za kusoma ukijumlisha ni mamilioni...50 .alikaa mtaani miaka 7 bila kazi ....hadi alitamani kujiuwa....ila mungu yu mwema saivi amepata job bot mungu yupo ongeza maombi
 
Daudi Kipara
Najua hata nikikupa pole haitabadili situation uliyonayo, elimu ya kwetu haimsaidii mtu kukabiliana na mazingira zaidi ni kufaulu mitihani tu BRN, madhara yake ndio haya, ni kweli ungesoma kufuka kondoo ungekuwa umefanya la maana sana na wala usingekuwa unalaumu zaidi ungekuwa unafikiria jinsi ya kukuza mtaji, Je wajua kondoo aina ya merino wanauzwa bei gani sokoni? fanya utafiti jibu lake utashangaa
Nakumbuka mie nilikataa kabisa kuendelea na masomo sijui mnaita degree, 0 au master degree nikafuata kusomea kitu roho yangu inapenda ufundi, japo wazazi walinipinga sana kwa kila namna ila hawakuweza kuzima ashki ya moyo wangu.
Kwa sasa ndio wanatambua nilikuwa na uamuzi sahihi,, na wala sijutii hilo
Simaanishi kusoma sio kuzuri ila kusoma kusikokuwa na mapenzi ndani yake ni tatizo kubwa sana

chukua "like" fundi
 
kuna rafiki yangu tokea
1.primary......amesoma international skul....
2.o..level education amesoma loyola..... ......
3.advance level......amesoma feza boys..........
4.chuo amesoma oxford university uingereza ................

Gharama za kusoma ukijumlisha ni mamilioni...50 .alikaa mtaani miaka 7 bila kazi ....hadi alitamani kujiuwa....ila mungu yu mwema saivi amepata job bot mungu yupo ongeza maombi

duuuh!!!hapoa laima ujute
kingine mara nyingi tukiwa shuleni na vyuoni tunakia ma higher expectation kwamba nikimaliza naajiriwa sehemu nzuri faster ila maisha asa hv yamebadilika kabisa ajira ngumuna za kuwekana na wengi tukimaliza vyuo tunawaza kuajiriwa mtu anaona haya kuanza biashara ndogo ndogo
 
Back
Top Bottom