NIMUOKOE NANI? (Swali kwa wanaume tu)

Power G

JF-Expert Member
Apr 20, 2011
3,887
1,193
Wapendwa wanaJF, enzi zile kabla hapajawa na bongo flava, kuna mwanamziki mmoja hapa kwetu Tz aliomba ushauri jinsi gani awezefanya kutatua tatizo lililoluwa linamkabili.

Kwa ufupi ni kwamba huyu jamaa alikuwa anasafiri kwenye ngalawa/mashua akiwa na Mama yake, Baba yake, Mke wake na Mwanaye. Kufika katikati ya bahari, chombo kilikumbwa na upepo mkali na kikaanza kuzama. Huyu jamaa alikuwa ni mtaalamu sana katika kupiga mbizi. Hata hivyo uwezo wake unaishia kumuokoa mtu mmoja tu ili aweze kupiga mbizi naye. Ndiyo akaomba wana JF mmshauri amuokoe nani????
 
Akifanikiwa kumuokoa Mke wake ...oh ..then ... atajitengenezea familia mpya ..na kuujza ulimwengu!!
 
Mama tu,
Wake wa ku-replace wako kibao tu,
Na baba nae aweza akawa nae si baba yako vilevile,
 
Mama! Kwa sababu mke atamuoa mwingine, watoto atawapata wengi tu, baba hajulikani kama ni halali au feki lakini mama ni mmoja tu na haiwezekani kumpata mwingine tena!
 
Naokoa mwanangu kwa sababu mbegu zawezakuwa zilikuwa za huyo mtoto mmoja tu ukimuokoa mama utazaa nae?,ukimuokoa baba mtazaa nae?,vilevile mkeo kama mayai ya uzazi yalikuwa yamemwishia yeye au wewe mtazaaje? Chukua chata yako yenyewe ndo itakayokuza ukoo wenu kuanzia kwa wazazi wako hadi ukweni wote watakuwa wanasema MTOTO WA MTOTO WETU.
 
Mama tu,
Wake wa ku-replace wako kibao tu,
Na baba nae aweza akawa nae si baba yako vilevile,
Shark, Unaona ni busara kweli kumuokoa mke wa mtu (mke wa baba) ukamuacha mke wako? Kwa nini usimuache aka-RIP na mme wake? Je ukimuokoa kila siku akawa anakulilia amemkumbuka mme wake utamsaidiaje???? Mwache ampe kampani baba kwani katika kiapo cha ndoa waliapa kuwa pamoja katika shida na raha, Nawe pia uliapa kuwa pamoja na mkeo katika shida na raha!! Iweje leo umuache katika shida peke yake????
 
Bora niokoe mke maana hata huyo mtoto yawezekana co wako, so bora nichukue ubavu wangu maana niliapa kuwa ntaambatana nae kwenye shida na raha, maradh na uzima hata kifo ki2tenganishe ss iweje leo nimwache?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom