Wanawamke mkitupenda wanaume mseme, haikupunguzii chochote

Amicus Curiae

JF-Expert Member
Sep 12, 2012
4,816
6,437
Kuna hii kasumba kwamba mwanamke akifunguka kwa mwanaume kwamba amemuelewa; basi labda atajishushia heshima; kwetu sisi wanaume (sio wavulana), kasumba hii haina ukweli hata kidogo.

Nimeandika huu uzi kwasababu ya tukio lililotokea wiki mbili zilizopita. Niliitwa na mwanangu kwenye hoteli moja hapa Jijini Dsm, kufika nikamkuta yupo na wadada wawili, mmoja ni girlfriend wake, yule mwingine ni rafiki wa g'friend wake, ni kama alikuwa idle flani hivi. Baada ya kutambulishwa tukaanza kupiga stori.

Baadaye akaja mshkaji mwingine ambaye anafahamiana na huyo mwanangu aliyeniita. Baada tu ya jamaa kutambulishwa akaanza kuonyesha interest kwa yule binti aliyekuwa idle, akaomba namba palepale, akamuita mtu wa jikoni akaagiza msosi, msosi ukaja, kabla hawajaanza kula jamaa akaanza kumuwakia yule mhudumu wa jikoni kwasababu alikaanga kilo zote mbili za nyama, badala ya kukaanga kilo moja na nyingine kuirosti, nadhani mhudumu hakusikia vizuri, nikawa namtetea yule mhudumu jamaa akatulia.

Kwasababu mimi nilikuwa nimeshakula nilikotoka, nikatumia toothpick kuonja vinyango mbili tatu nikaendelea zangu kuchat kwenye simu.

Baadaye tukaagana. Sasa jana mshkaji wangu amenipigia, ananiambia kale kabinti kalikokuwa idle kamenielewa, nilikuwa nimeshasahau ila alivyonikumbusha nikakumbuka, hakataki kabisa kumsikia jamaa aliyekuwa anamshobokea!

Nikamuuliza amejuaje? Akasema dem wake ndio kamwambia. Eti kamesema jamaa sio type yake! Akaenda mbali zaidi, kwamba dem wake kamwambia wakati tumekaa pale halafu jamaa anajiongelesha na kuagiza sijui msosi na vinywaji, alikuwa anakasirika sana . Anahoji kwamba yule jamaa alikuwa na sababu gani ya kuning'iniza funguo za gari kwenye lux, anadai ule ni ushamba .

Kumbe tulivoagana tu pale, jamaa anapokelewa simu na kujibiwa sms kwa tabu sana! Zaidizaidi alikuwa anaombwa hela kwa makusudi ili asimsumbue binti.

Eti mimi ni mpole sina maneno mengi, nimevaa kikaka, nanukia vizuri, halafu nawasemesha wahudumu kwa staha hata kama wanafanya kazi yenye ujira mdogo.

Nimemwambia jamaa ampe namba. Kwa sababu na mimi ni baharia, nikachukua namba yake nikai-save. Leo kanicheki, hajui kama nina namba yake na hajui kama najua vile anahisi juu yangu , msg anazotuma hata hazieleweki maskini...

Frankly speaking, hata mimi nilimuelewa, ila anashindwa kabisa kusema, anahangaika tu.

Wadada, mkituelewa mseme, hakuna shida mbona; ingawa kwa wanaume ambao ni immature wanaweza wakaona ni jambo la ajabu. Ila kwangu mimi na baadhi ya wengine, sio tatizo hata kidogo. Hisia ziko kwetu sote, wanaume na wanawake.

Kudumu kwenye mapenzi hakuna formula kwamba nani kaanza kumtamkia mwenzake. Hata mwanamke kukukubalia mapema haimaanishi yeye ni malaya, inawezekana tu mna chemistry. Mbona wapo malaya wengi tu ambao wanaweza wakakuzungusha hata mwezi!

So mfunguke, msiogope. Na niyi wavulana badilisheni hiyo mitazamo yenu hasi.
 
Kudumu kwenye mapenzi hakuna formula kwamba nani kaanza kumtamkia mwenzake. Hata mwanamke kukukubalia mapema haimaanishi yeye ni malaya, inawekana tu mna chemistry. Mbona wapo malaya wengi tu ambao wanaweza wakakuzungusha hata mwezi!

So mfunguke, msiogope. Na niyi wavulana badilisheni hiyo mitazamo yenu hasi.
Wanaogopa kusema kwa kuwa watakuwa wamekupa hati miliki,ambayo muda wowote inaweza tumbukiza nyongo.
 
Back
Top Bottom