Nimewapiga wachawi—kipigo cha mbwa koko!

Nimewapiga wachawi—kipigo cha mbwa koko!

Setfree

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2024
Posts
5,527
Reaction score
7,121
Hii ni habari ya kweli kabisa. Uongo mimi nauchukia kama ukoma.

Kama huamini kuna wachawi, sikiliza vizuri: Hivi majuzi, walikuja usiku, muda mfupi baada ya mimi kujilaza kitandani. Wakaanza kunikandamiza kwa nguvu sana. Mgandamizo ulikuwa mzito, utafikiri mtu ameweka juu yangu mifuko mitano yenye saruji. Sio mzaha, nakwambia.

Sijawahi kuhisi uzito huo kamwe. Haraka sana nilitambua ni wachawi wanaotumiwa na mapepo kujaribu kunidhuru. Nikaanza kuwakemea kwa Jina la Yesu - kwa sauti ndogo, lakini yenye mamlaka watoke na kuniachia. Instantly, waliniacha na mgandamizo ule ukatoweka. Jina la Yesu lina nguvu sana. Ukilitamka, wachawi wanapigwa kipigo kikali sana na kukimbia. Hii ni mojawapo ya faida za kuokoka. Unatembea kifua mbele bila kuogopa wachawi.

Yakobo 4:7-10
"Basi mtiini Mungu. Mpingeni ibilisi, naye atawakimbia. Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia. Itakaseni mikono yenu ninyi wenye dhambi, na kuisafisha mioyo yenu ninyi wenye nia mbili. Huzunikeni, na muomboleze, na kulia. Kicheko chenu na kigeuzwe kuwa kuomboleza, na furaha yenu kuwa huzuni. Jinyenyekezeni mbele za Bwana, naye atawainua."
 
Lakini kama hujaokoka ukiwakemea wachawi au mapepo, hayatoki, sana sana yatakudhuru. Soma Matendo 19:13-16
"Baadhi ya Wayahudi wenye kutangatanga, nao ni wapunga pepo, wakajaribu kutaja jina la Bwana Yesu juu yao waliopagawa na pepo wachafu, wakisema, Nawaapisha kwa Yesu, yule anayehubiriwa na Paulo. Walikuwapo wana saba wa mtu mmoja Skewa, Myahudi, kuhani mkuu, waliofanya hivyo. Yule pepo mchafu akawajibu, akawaambia, Yesu namjua na Paulo namfahamu, lakini ninyi ni nani? Na yule mtu aliyepagawa na pepo mchafu akawarukia wawili, akawaweza, akawashinda, hata wakatoka mbio katika nyumba ile wakiwa uchi na kujeruhiwa."
 
. Wakaanza kunikandamiza kwa nguvu sana. Mgandamizo ulikuwa mzito, utafikiri mtu ameweka juu yangu mifuko mitano yenye saruji. Sio mzaha, nakwambia. Sijawahi kuhisi uzito huo kamwe. Haraka sana nilitambua ni wachawi wanaotumiwa na mapepo kujaribu kunidhuru. Nikaanza kuwakemea kwa sauti ndogo, lakini yenye mamlaka watoke na kuniachia. Instantly, waliniacha na mgandamizo ule ukatoweka. Jina la Yesu lina nguvu sana.
Ni kweli tunachosema Jina la Yesu kwenye Ulimwengu wa Roho ukiona unathibitisha lina nguvu sana

Hiyo ya kukandamizwa ndio style zao wanakosa kazi kuja kusumbua watu
Usiku wanapoteza muda
 
Hiyo ni Sleep paralysis inatokana haswa na mtindo mbovu wa maisha.

Kutokuwa na utaratibu maalumu wa kula, Uchovu mwingi, Stress, Kulala chali na kuchelewa kulala ni moja ya visababishi.
Psychology haiwezi elezea mambo ya Rohoni hata siku Moja.... Spiritual life is real like physical... Ila mambo haya yamefichwa kwa wenye hekima ya dunia... Ndio maana hawezi kuelewa mpaka pale Roho wa Mungu atakapokufunulia.... 😁
 
Psychology haiwezi elezea mambo ya Rohoni hata siku Moja.... Spiritual life is real like physical... Ila mambo haya yamefichwa kwa wenye hekima ya dunia... Ndio maana hawezi kuelewa mpaka pale Roho wa Mungu atakapokufunulia.... 😁
Unawezaje kuthibitisha kuwa huyo Roho wa Mungu unayedai anakufunulia si mawazo yako tu au hisia zako potofu?

Unajuaje kama huo ni udanganyifu wa nafsi tu?
Kwanini kila mkristo akishindwa kujibu swali anakimbilia kusema mpaka uwe na roho ndiyo utaelewa?

Kwanini lazima niamini kwanza ndipo nipate majibu na siyo nipate majibu kwanza ili niweze kuamini?
 
Hiyo ni Sleep paralysis inatokana haswa na mtindo mbovu wa maisha.

Kutokuwa na utaratibu maalumu wa kula, Uchovu mwingi, Stress, Kulala chali na kuchelewa kulala ni moja ya visababishi.
Mkuu, shule nimeenda. Najua sana umuhimu wa utaratibu wa kula, umuhimu wa kulala mapema na mambo yote muhimu kiafya. Siku hiyo sikuwa na uchovu wowote na mimi stress kwa ujumla sina. Maisha yangu yamejaa furaha sana kwa sababu Mungu amenifanyia mambo mengi ya baraka.

Inaonekana huijui vizuri Sleep Paralysis. Mtu aliyepatwa na SP hawezi ku-move wala kuongea tena hali hiyo huanza anapo-fall asleep. Mimi nimekuambia nilikemea kwa sauti, kwa Jina la Yesu na nilikuwa tu ndo nimejilaza - usingizi ulikuwa bado haujanishika.

Science haiwezi kuelezea mambo ya kiroho. Kisayansi, watu wenye sleep paralysis huwa wanaona kwa mfano shadowy figure chumbani, a presence near the bed, breathing sounds, whispers, au footsteps. Ajabu ni kwamba wanasayansi hawawezi kuyaona au kuya-prove hayo yanayoshuhudiwa na mtu mwenye SP; wanachoona tu kwenye lab ni brain activity. Huu ni udhaifu mkubwa sana wa sayansi katika eneo hilo.

Ndugu yangu Ibn Unuq shetani na mapepo wapo. Na hao ndio wanaofanya kazi pamoja na wachawi. Yesu ametupa mamlaka ya kuwafukuza kwa Jina la Yesu.
 
Yesu alisema Wapendeni adui zenu... Alfu wewe unawapiga,?🤣🤣
Adui wanaozungumzwa ni wanadamu. Mapepo tunatakiwa kuyatandika mboko za ukweli. Na si kwa nguvu zetu. Ni kwa kutamka tu: "Kwa Jina la Yesu, shindwaaa"

Ukitamka hivyo, yanapigwa sana. Kumbuka wale walioenda kumkamata Yesu. Alipowaambia: "Ni mimi hapa." Wakarudi nyuma, wakaanguka chini - puu! Ni mapepo hayo yalipigwa mweleka! Jina la Yesu linawapa vipondo vya uhakika 😀
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom