Well, ulianza vzr kama vile mtu aliyejutia ile kazi, yale maisha na consequence zake, na nikachukulia sasa umeamua kurudi kwa Mungu ki ukweli hivyo Yesu Kristo achukue adhabu yako(mshahara wa dhambi=mauti),misiba yako,aibu yako na kukubali kununuliwa kutoka jela ya shetani(kwako uchangu) kwa kulipiwa kwa Damu ya Thamani ya Yesu Kristo Mkombozi wetu. Hapo nilikupenda na nilitaka kukuombea upate msaada wa kimungu huyo uliyemkimbilia! Sasa unasema,eti ukimwambia akikumwaga, huyo aliyekushauri akutafutie mdhambi mwingine, mmmh, bado hujapona! Ushauri, jiachilie kwa Mungu wako wholy, jinyenyekeze kwake,mtumikie na kumtegemea yeye tu mbona Mungu huyu nimtumikiaye Anaweza? Yesu anasema alikuja kwa wenye dhambi ili wapate kutubu. Ukitubu kisawasawa mpaka ukawekwa huru, utaona unakuwa na ujasiri wa kutamka ulikopitia, tena sio kwa huyo mchumba tu, (ambaye kuna kazi ya kufanya ili awe wako) bali utapata ujasiri wa kupanda madhabauni na kutoa hiyo stori kama 'ushuhuda'! Kuanzia hapo, hata hao machangu wa Kenya kama bado wapo kwenye hiyo fani watakuogopa, lkn kama wameacha au wanataka kuacha, basi watakuona wewe ni shujaa, nawe utakuwa kioo kwao. Huyo njemba kama ni wako atakupenda zaidi, akiishia ujue yupo aliye wako anakuja! Lkn haya yote inategemea na kanisa unalosali, je wanaelewa maana ya 'Deliverance of the Soul'! Kama hamna, huko kwenye wazo mbadala mie siko! Mkubali Yesu na Mtumikie Mungu wa Moyo wako wote. Barikiwa mama.