Nimewahi kuwa changudoa, nimjulishe?

Nimewahi kuwa changudoa, nimjulishe?

Umepima? Na matokeo je
...baada ya mama yako kujua ulkuwa unajiuza alikuchukuliaje,shujaa,alikupa pole...au nini.binafsi nimekupenda ww ni jasiri na naamini umetubu,kumwambi au kutomwambia inategemea kichwa cha mumeo kikoje
 
Pole mdada kama ni kweli lakini usikurupuke kumwambia dada yangu sie wanaume tunajijua hakuna kitu kinauma kama mwenzangu aniambie alishatembea nafulani au alishafanya mara kadhaa inaumaje! We lia na Mungu wako akusamehe maana hapo uliemkosea ni Mungu sie huyo mchumba wako kwani haukuwai kuwa nae kabla ya hayo useme ulimsaliti hivyo toba yako ni kwa Mungu mengineyo yawe ni kama ushuhuda tuu. Kingine jisamehe kwanza maana unajihukumu pia sali sana na tumaini liwa kwa Kristo tu kuhama kanisa haita kuponya dada yangu .
 
Carry on with your life, jisamehe nafsi yako halafu funga hiyo chapter. Hata akija kujua kutakuwa hakuna athari. Let God/Nature take its course. Ndio maana ya kumkabidhi Mungu. You are a new person now, right? Why worry......
Na kwa kuongezea, kwani umemkosea nini hadi u confess kwake, just clear your conscience and that's all.

unayoongea ni kweli ila ujua naitaji mme, naitaji mtu wa kufikiria kwa niaba yangu, naitaji mtu wa kuplan kwa niaba yangu, naitaji kuongozwa na sio kuongoza tena na huyu mmasai ndiye right person
 
Unajitesa acha kuukimbia ukweli,mwishowe utajikana mpaka mwenyewe...ur struggles made you survive and strong but dont let them define you!
najihisi nimefanya makosa makubwa mno na naona kama ikijulikana ntakuwa nalidhalilisha kanisa
 
dada, Mungu akusaidie. ninaomba usipate shida hivyo, maisha yako yapo mikononi mwa Mungu si mikononi mwa mwanadamu. mwanaume bora ataletwa na Mungu sio wanadamu. wewe mwangalie Mungu, haukuwa hata na umuhimu wa kuhama kanisa, ulitakiwa kubaki tu Mungu atakusaidia, kama kuna mtu atavujisha mwache avujishe, hata katika kuvujisha huko Mungu atakusaidia tu. hayo ni maisha ya zamani. sisi sote tulikuwa malaya sana, nimelala na wanawake wengi sana na nina watoto nje ya ndoa wengi, lakini ilifika kipindi nikaamua kumrudia Mungu, nimebadilika, nikikutana na mtu aliyekuwa malaya zamani, simhukumu kwa mambo yake ya zamani.

ya kale yamepita, tazama yamekuwa mapya. unachotakiwa kufanya, rudi palepale kanisani, wewe fanya mambo mema ili matendo yako yakutetee, hata mtu akisema ulikuwa changu kwa kuona matendo yako atasema ohhh lakini amebadilika kabisa sio kama yule wa zamani. wanawake wengi wanaoolewa walishawahi kufanywa na wanaume wengi sana, tunaoa basi tu. sisi wanaume pia tumelala na machangu wengi tu. mimi binafsi nimelala na machangu rundo, nimelala na wahudumu wa hoteli rundo, nimelala na wahudumu wa migahawa rundo....machangu wa kuwalipa kabisa rundo hadi wengine nikikutana nao siwakumbuki sura, na hata kama kanisani kwangu mtu atasema nililala na mimi, nitasema ohhh really, kumbe nilishawahi kulala na wewe, lakini nitamwambie siku hizi nimeokoka siko vile tena moyo wangu umebadilika, matendo yangu yamebadilika sasaivi nina Yesu na kwakuangalia matendo yangu yeye mwenyewe hata mdomo hatafungua na hata akifungua hatakuwa na madhara yeyote kwangu. watu wote sisi tulikuwa waovu tu zamani bila neema ya Mungu tungeshakufa zamani. wewe hauko tofauti na wanadamu wengine waliokosea sana, cha muhimu tu unatakiwa kujitahidi umwombe Mungu aondoe tamaa ya uzinzi, kama tamaa ikiondoka basi, wewe ni msafi na usiwe na wasiwasi. unasikia?

thanks na ubarikiwe
ntaku-update kila stage ntakayochukua
 
unayoongea ni kweli ila ujua naitaji mme, naitaji mtu wa kufikiria kwa niaba yangu, naitaji mtu wa kuplan kwa niaba yangu, naitaji kuongozwa na sio kuongoza tena na huyu mmasai ndiye right person

That's up to you then, you know what to do. Halafu nimekukumbuka sana Marytina you always have these weird stories.....
Interesting....
 
Last edited by a moderator:
Dah!!!!!! usijaribu aisee kumwambia, yaliyopita yamepita, uhuru gani wa moyo unaotafuta bhana??????? hata akija jua kwani wana picha zako hao watoa habari???? watu wanakana hadi kaburini wakati wamekutwa ana kwa ana ije kuwa stori yakuambiwa, Kaa na lako moyoni, ndio maana wahenga wanasema "wanawake matusi mengine toka kwa waume zao wanajitakia wenyewe"



Hawa wanaume sio kabisa, ukikosa jambo huweza kukutukania hadi kuku wa nyumbani kwenu, sembuse umwambie hilo si itakuwa kama alarm ukikosa.
bora kutukanwa naogopa kuachwa na kuonekana nimelidhalilisha kanisa
 
marytina, ulsema ulionana na madem siku moja, unauhakika gani kama wataendelea kuwepo?...alafu kumbuka hujamkosea bf wako,hamkuwa kwenye mahusiano bado,so wasiwasi wako nn?
 
Kama tyr umejisalimisha kwa Yesu,ni bora ukayatapika yote ili uwe huru,huwezi ukawa huru ikiwa kuna kitu kipo ndani yako kinakukereketa..hicho kitakutesa na kukusababishia uwe mfungwa na mtu una hana hama,katika huduma.
Nataka nikutie moyo,hakuna aliyekuwa mkamilifu sisi ni wanadamu tu,tunapitia Mengi na kwa sabb tofautitofauti,mpk pale unapopata tumaini jipya kwa kumpata Yesu Kristo.
Hivyo mwambie tuu,kama huyu ni mume wako,atakuwa wako tu.hata kama atayapokea kwa style gani yale utakayomwambia,
kama sii wako,basi Mungu atakupa wako,
Mwekani wazi tu,
Hata afya yako mweleze ukweli
Over.
naogopa sana atakavyoreact
yaan kuna siku niliota kuwa nimwemwambia yaan huo moto uliowaka usipime....ilikuwa ndoto tu ila hata kesho yake skwenda kazini kwa mawazo
 
Nini maana ya changudoa? Kufanya na watu usiowajua in return for money? Na wanaotembea na wanaume 20 kidogo in the name of boyfriend na wanapewa "hela za matumizi" are they any better? Hawa huwa wana confess kwa wachumba wao? To me kuna different levels za "uchangudoa" from kujiuza barabarani to kubadilisha partners kila kukicha na kuhongwa pesa. Sioni kama wewe ndo mkosefu kuliko wote, kila mmoja ana lake. Wangapi wamekuwa na one night stands kibao, na wanadunda tu na leo wanaweza kuku judge wewe. Songa mbele u seem to regret thats good coz ni step ya kuomba forgiveness. Truly repent and forgive urself. Hakuna atakayekuja kukwambia umesamehewa, wewe omba msamaha to ur God and be a better person everyday. Nafsi yenye kujutia dhambi ni bora zaidi na ita heal

huoni wakenya wakisema ntaishi bila nimpendaye maisha yangu yote???nimechoka sana mpaka ubongo naitaji mwanaume wa kunisaidia na huyu MMASAI ni right person...akiniacha nianze tena kujiwazia, kujiongoza i cant that...

na vipi pale kanisani nlipokuwa kiongozi wa vijana wakijajua mimi ni x-changudoa???ntaweka wapi uso wangu
 
kosa langu ni kubwa sana halivumiliki yaan ni bora ningekuwa na makosa mengiene yote hata kuua angeweza kunielewa lakini si kulala na miwanaume kibao kwa pesa

NOPE.....Jipange kwa maombi MUNGU aandae moyo wa jamaa katik kumtel ukweli otherwise utakuwa unaishi kinafiki it wil eat inside, jamaa aki learn ukweli nje itakuwa worse

WOKOVU utakuwa hauna kazi kama usipo kuwa wazi the guy anastahili ukweli tena utoke kwako otherwise jipnge for the worst
 
marytina, ulsema ulionana na madem siku moja, unauhakika gani kama wataendelea kuwepo?...alafu kumbuka hujamkosea bf wako,hamkuwa kwenye mahusiano bado,so wasiwasi wako nn?

zaidi ya salam waliambia wamepata vijiajira ARUSHA kwenye makampuni.........wapo na najua hawataondoka ARUSHA kirahisi kwani maisha Nairobi yanaitaji ujanja kuliko arusha...ambapo kingereza kinawabeba kupata vijiajira
 
it wasnt your will kua changudoa hustle za maisha zilikufanya uwe vile na hata hvyo hyo kaz ilikufanya ufike hapo ulipo sasa? naamin hata wadogo zako hawajui hilo kutokana na maelezo yako. kwa ushaur anza kuongea na familia yako ukifanikiwa hapo ukaongee na mchumba wako!

am proud of what you did si kwa kua changudoa ila kwa umr wako kuweza kusimamia wadogo zako na wewe kusoma mpaka chuo kikuu

am also personally proud of what you did, u deserve special respect from you youngs Marytina
 
Last edited by a moderator:
neno la mungu linasema "usikumbuke mambo ya zamani" hayo yalikwishapita, na ww hauko tena huko. hakuna sbb bali iwe somo tu kwako
 
NOPE.....Jipange kwa maombi MUNGU aandae moyo wa jamaa katik kumtel ukweli otherwise utakuwa unaishi kinafiki it wil eat inside, jamaa aki learn ukweli nje itakuwa worse

WOKOVU utakuwa hauna kazi kama usipo kuwa wazi the guy anastahili ukweli tena utoke kwako otherwise jipnge for the worst
kuisoma tu hii post yako natetemeka, usiku kama tumechelewa kurud akiwaona machangudoa husikitika sana na hufokea mpaka usukani wa gari anayoendesha.......roho huniuma sana
 
bora kutukanwa naogopa kuachwa na kuonekana nimelidhalilisha kanisa


Kanisa litadhalilika kivipi ili hali hilo jambo lilitoke kabla hujampokea yesu???? KIFUPI KAMA UMEOKOKA na umepokea sara ya toba ya kweli na huendelei na hiyo tabia tunasema yote yaliisha pale msalabani, sasa wewe ulipokea sara ya toba gani???????

Anyway mwambie atazidisha sana upendo hutajuta hakika, maana mie mgeni wakupenda japo nimetoa ushauri.
 
bora kutukanwa naogopa kuachwa na kuonekana nimelidhalilisha kanisa
Mkuu Marytina kwanza pole sana,lkn unanisikitisha sana kuogopa kile nilichokiwekea rangi. Hutakuwa wa kwanza kuachwa. Kutokana na Maelezo yako,pamoja na kuolewa lkn bado jambo hilo linakuumiza ww binafsi. Hapa unajaribu kumuweka mumeo km ngao ya kutoa kile kilichokukaba muda mrefu. Me nakushauri,mwambie haijalishi matokeo kwa upande wake yatakuwa chanya au hasi. Muhimu hapa ni wewe kutua huo mzigo. Akikuacha sema ahsante Mungu,baada ya kukuacha Mungu hatakuacha,lazima atakuonyesha mlango mwingine wa kutokea. Ukweli siku zote ndo wenye matokeo chanya kuliko uongo.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom