Nimewahi kuwa changudoa, nimjulishe?

Nimewahi kuwa changudoa, nimjulishe?

Kutokana na uzoefu nliyouona mahali pawili tofauti napata ujasiri wakukuambia MUAMBIE ukweli huyo jamaa ako,siku akija kujua(na lazima atajua) itakugharimu zaidi ya sasa kama utamuambia,muambie ukweli wote nini kilitokea yeye ndio aamue kunyoa au kusuka na utakuwa na amani ya milele wewe na yeye..anayekuambia usimuambie hakika anakupoteza,hakuna siri ya watu itayokaa milele katika kifua cha mwanamke milele(namaanisha hao mliokuwa mnajiuza nao)..
mmh...najihisi kutetemeka napoisoma hii post
 
Pole sana dada,

Amua kuokoka, biblia inasema, ukiokoka unakuwa kiumbe kipya, ya kale yanapita. huyo mchumba usimwambie, muombe Mungu hekima kama ungependa ajue bila ya kuharibu uhusiano wenu. Mungu atakupa hekima, hasa kama umebadilika kwa dhati.

Yesu atakuweka huru na hilo doa maishani. nashauri umuombe Mungu, tafuta washirika wengine au mchungaji unayemwamini, omba naye Mungu atakusaidia.
mama alipotoka jela nliacha kabisa kujiuza kwa kuwa mama ni deal maker within a week hela alishaanza kupata
jaman kuna jambo ambalo mwanaume havumilii hata akibembelezwaje na hili langu ni mmojawapo
 
ila tukiwa barabarani usiku tumechelewa akiona machangudoa anafoka ndani ya gari yaan roho huwa inaniumaa!!!!!!!!!

hyo ni perception yake na huyo ni mume wako mtarajiwa mbadilishe hyo kitu kwa kumwambia ukwel
 
Usijaribu hata siku moja kusema, na waepuke marafiki wowote ambao ama wana mahusiano na wale mliokuwa sex workers au sex workers mliokuwa pamoja kabla.

thanks my dear!
bora niendelee kuteseka kuliko kusema, ntahama makanisa yote
 
angekuwa mume wako sijui ungeanzia wapi kumueleza akakuelewa kama ni boyfurendi tu Mwambie Mwenyewe kwasababu akijua mwenyewe itakuwa balaa kama anakupenda trust me mtaendelea na uhusiano even though weka possibility kubwa ya kuachwa

zakuambiwa changanya na zako..!!!
hata akinielewa nahisi hatakuwa na ham ya kulala na mimi tena na kila nkichelewa atatoa lugha chafu za kuniumiza
 
Si lazima iwe hivyo. Hiyo ni historia ya siku za nyuma. Akiambiwa lazima kwanza astuke lakini nina imani baada ya muda na hasa kama atapata watu wenye upeo kumshauri, atakusamehe.

Vingenevyo siku zote utaishi na wasiwasi. Je akipata taarifa hizo kwa watu wengine itakuwa vipi? Bila shaka mbaya zaidi na hapo hakutakuwa na msamaha.
mnaniweka njia panda sana............jaman itakuwa aibu sana hata washirika kanisani wataona kama nimelidhalilisha kanisa ukweli ukijulikana
 
Umeishasema ameishasikia.labda kama hana access ya jamiiforum
 
thanks my dear!
bora niendelee kuteseka kuliko kusema, ntahama makanisa yote

Naomba usiendelee kuteseka kwa kuwa Mungu anasamehe na amesema anasamehe. Usiteseke rudi kwa aliyekuumba and be free. Pengine u will be better than most of us. Binadamu ni nani? Kuwa mwema sana kwa mumeo na jamii, change so much kiasi kwamba hata akijua na ukamwambia umebadilika ataamini. Keep a low profile kwa hao marafiki zako ikibidi badili namba. Kumbuka God loves u the way u are and u deserve better. Kila la heri
 
Usithubutu kumwambia duniani na akhera kama akisikia pia kataa ukikubari huo msalaba wake kama amekwisha kuoa utakuelemea na kukutesa mpk unaingia kaburini atakunyanyasa sana huyo mwanaume. Kaa kimya tubu kwa Mungu na si kwa mwanadamu yeye kama amekukuta umeshabadika aendelee nawe kama ulivyo forget about the past.

thanks alot..........umeongea jambo nlilotaka kulisikia ila nina udhaifu sana mbele yake sijui kama naweza kumkatalia akiniuliza....nampenda sana mpaka nimekuwa dhaifu na honest sana kwake
 
Hata wakivujisha haina mashiko kila mtu duniani ana past experience ya life. Wewe unajitia uoga usio na sababu ndo mana watu wengi wanaoanaga na kutokuuliza past experience. Kamwe usifikiri kumwambia itakufanya akuone mwema na muwazi itakuharibia. As long as ulitubu hyo tabia move on hakuna aliye msafi. Kuna watu yamewakuta makubwa walipo confess walifikiri wanajenga kumbe ndo waliharibu kabisa. Nijuavyo mwanaume ukishamwambia ulikua changu atafikiri huko kote ulitumika kuanzia tigo, je ulitoa mimba ngapi? Au kutumia madawa ya kuzuia mimba. Na hapo lazima atafikiria Mara mbili na kukutema maxima. Ndo mana hata bible inasema tazama ya kale yamepita na yamekua mapya. Sasa wewe kinachokuhangaisha nini?
nataman likizo nije kwako hata kwa siku mbili....
u mk me feel i am alive
 
Tatizo lako hukubali ushauri unang'ang'ania Wakenya mata roho inakusuta.We unajifanya mgumu tu bila sababu wapewa ushauri unasema wa kupasua kichwa. Usinge kuja kuomba ushauri. Kama IPO IPO tu. Au kama kuna kitu hujakieleza unahofia.

mikato yako inafanana kabisa na mama yangu!!!
ila mjue sjawahi pata raha maisha yangu yote ya utotoni na naamin huyu ndio mwanaume wa kunipa raha maishani
 
Una hamu sana na ndoa aisee ujiue kwa sababu gani loh!
shosti ungelijua namna nlivyohangaika na kukomazwa kichwa kwa sasa nataka mume aniongoze na sii kujiongoza tena mwenyewe....
nataka mtu wa kufikiri kwa niaba yangu, nataka mtu wa kuplan kwa niaba yangu....staki tena kuwa kiongozi nataka kuongozwa
 
Na nadhani bado hajala mzigo huku akiwa na imajinasheni nyingi kwamba anaoa mke safi kumbe mke alikua changu,aisee. mnao oa mna moyo sana. kuna ule msemo kwamba kunguru hafugiki...................
 
we dada una hakika umetubu hiyo dhambi kwa roho na kweli na ukaamini Mungu amekusamehe? Nauliza hivyo kwa sababu maelezo yako yanaonyesha kuwa dhambi yako inakutangulia. Kama ulishaungama na una hakika hata ukitishiwa kiPRADO hutarudi kwenye uchagudoa basi amini umesamehewa. Ukiamini umesamehewa unakuwa na amani moyoni. Hata ukikumbuka dhambi yako inakuwa kama unavyokumbuka chakula ulichokula jana kwa hiyo husononeki wala kuogopa sijui nani atajua. Ukiwa na amani na wewe mwenyewe huwezi kukosa amani kwa wengine. Tatizo unajiona ulifanya dhambi kubwa mno kama umeua dunia. Unajiona mchafu sana kiasi kwamba hata utubu vipi huwezi kusamehewa (ni vizuri kujiona mchafu sana na ni vizuri kuamini hakuna uchafu unaoshindikana kuoshwa pale unapoamua kujirudi.

Kwa hiyo nachoweza kukuambia ni kuwa ujisamehe, utafute amani yako kwanza - kuwa mkweli kwa Mungu wako na kama umetubu amini kusamehewa na ujifunze kufurahia msamaha badala ya kuangalia angalia nyuma. Au unataka uone ishara gani ndo uamini kama umekuwa mpya? Halafu hao rafiki zako unatarajia wafichue siri kwani wao hawajipendi? Kama kweli na wao wamemrudia Mungu hawawezi kamwe kusema huo upuuzi labda utuambie mnaenda kwenye hayo makanisa kutafuta wanaume. Hapo lazima muoneane wivu.

Na kama uhusiano wako na Mungu ni mzuri na Mungu ameweza kukuinua umtumike na ukaweza kuongoza vijana vizuri, huoni kama hiyo hofu yako inakurudisha nyuma kiroho? Ona sasa umeacha huduma umekimbilia sijui nje ya mji wapi ili shoga zako wasikusemee. Hapo huwakimbii shoga zako. Unakimbia kivuli chako. Hata ukienda wapi kitakufata tu mpaka upatane nacho. Ila kama unakosa amani saaaaana kumficha huyo mchumbako basi we mwambie. Kwanini ukose amani? funguka, kitakachofuata ni matokeo tu - kuachwa au kuolewa.
pls nitaku PM nikuoneshe ugumu unaonikabili na jinsi maisha yangu yanakoelekea
note:siwezi rudia uchangudoa na kama ntaamua kufanya haramu ntafanya biashara nina back-up nzuri tu ya dhuluma na rafu kibiashara kama ntakuwa mtu wa tamaa wa PRADO
 
Ukisema tu uchangudoa utakuhusu but tym will come utamfungukia but for now piga kimya muombe Mungu akusaidie huo mtihani
 
Back
Top Bottom