Nimewahi kuwa changudoa, nimjulishe?

Nimewahi kuwa changudoa, nimjulishe?

Utupe mrejesho, manake kama maushauri tu umeyapata.

Kama hutajali tunaomba utumwagie kisa kifupi lakini cha kusisimua ulichokumbana nacho enzi ya uchangu.
 
Usije jaribu kumwambia mtu yoyote maisha yako ya gizani. Kaa nayo mwenyewe.
 
mnaniweka njia panda sana............jaman itakuwa aibu sana hata washirika kanisani wataona kama nimelidhalilisha kanisa ukweli ukijulikana

Moja ya sifa ya kanisa lolote ni mtu kutubu na kuamua kufuata yaliyo mema ama sahihi machoni pa Mungu. Hakuna aibu katika kutubu. Aibu unamwonea binadamu mwenzio au Mungu? Wanatubu wauwaji itakuwa wewe?
 
ila pia dini zetu hazitaki uongo na kuna uongo unatesa sana maisha yoote
hapa naogopaga hata kwenda kwenye baadhi ya sherehe maana kuna wadada wakenya hapa ARUSHA wanaweza kuniharibia

Marytina;
Nasema na weye kama mtaalam wa mambo hayo unayo yapitia kwa sasa. Umeandika humu jf kuomba msaada hivyo huu ndo msaada wangu;
1. Hakuna kitu kibaya kama yule umpendaye akija funuliwa kwako thru another source. (Third party)
2. Umpendaye hawezi kuwa mwovu tena kama umemjua na akikuhakikishia kuwa kabadilika (II Cor. 5 : 16 Wherefore hence forthknow we no man after the flesh,......
3. Umesema weye ni mtu wa Kanisani, unatengeneza mambo yako na Mungu, huwezi kutengeneza mambo na Mungu usiye muona, halafu umfiche ambaye anakuja kuwa wako wa milele. Hapana, tengeneza naye kwanza.
UAMUZI:
Mwambiye taratibu kabisa, bila hofu yeyote. Kama ni wako atakupokea tu. Hukuenda kujiuza kwa sababu ya tamaa zako, usingelimalizia shule kwa njia nyingine. Mbona sisi tumekuelewa, Ukimwomba Mungu atakutetea. Bora ajue akukatae mapema kabla ya ndoa kuliko kuja kukukataa kwenye ndoa.
 
Kama unasukumwa na dhamiri ya dhati mwambie lakini tumia hekima kubwa au waweza ukamueleza kama unatoa ushuhuda fulani juu ya maisha yako. Huku ukionesha kulia machozi ya mamba
 
Ukimwambia utaachwa nakuambia. Hivi nyie hamjui kuwa wanaume wana ego eeh! Don't tell him, unless uwe unataka kuachwa.
 
Mi mbona nimewanunua sana machangu mpaka niliemuoa nae nilitoa huko huko na ametulia tu. Usiogope unawezakuta hata huyo mchumba ako aliwahi kua shoga nae anaogopa kukwambia....hii dunia hii iache tu.
 
wewe mdiye wa ajabu
miaka mitatu YES
FORM FOUR MMOJA then chuo miwili au wewe kwako chuo lazma Universuty na lazma mtu asome ADVANCE LEVEL????
yes ni miaka mitatuna tena mama alinikuta sjamaliza
Hadithi za Shigongo
umesahau kuwa Mama yenu aliwafuata Shule TZ Primary akawapeleka Shule
Wote watatu tukapelekwa boarding skuli Nairobi-Kenya, mama akarejea nakuru miaka minne baadae mama
Kenya ipo mpaka la 8 (STD VIII) haya ukaingia Sekondary miaka 4 na ukajiunga na Chuo cha Cherehani au mapishi ?
huku TZ hatuna vyuo vya mwaka
 
Mwombe Mungu akupe Neema na Amani ya kuongea jambo hilo,kwanza mwambie mchugaji wako maana yeye ni mtuza siri za watj wa Mungu, naye atakupa ushauri nink cha kufanya,usianze kwanzq na mchumba wako kabla ujapata kibari cha mchungaji na Amani ya Kristo iamue Moyoni mwako kwanza.
 
Ukimwambia utaachwa nakuambia. Hivi nyie hamjui kuwa wanaume wana ego eeh! Don't tell him, unless uwe unataka kuachwa.

acheni uoga wa kunguru, kama ndoa ipo hakuna kizuizi, its only truth will set gateway of happier marriage.
 
Pole.. kwani unadhani yeye msafi? Labda kwa sasa lakini hapo mwanzo?
Acha maisha yaende Unafiki ni sehemu yake,wala usijaribu sisi wanaume huwa hatuoi changudoa hata kwa kusikia tu
 
Sikia sister, ,maisha ni mafupi sana kuhishi kwa hofu na kukimbia kukwepa watu, taarifa kama hiyo kwa mara ya kwanza huwa inaleta shock sana kwa wanaume, bt time inavyoenda ukijumuisha na upendo kama upo mambo yata tulia tu.

Wew ndo wamjua vema mwenza wako tafuta njia sahihi ya kumwambia, ila usije mshirikisha yeyote wakati unamweleza haya muwe walili tena home.
kosa langu ni kubwa sana halivumiliki yaan ni bora ningekuwa na makosa mengiene yote hata kuua angeweza kunielewa lakini si kulala na miwanaume kibao kwa pesa
 
Kheri asikie kutoka kwako kuliko kusikia kutoka kwa watu wengine,utakuwa huru sana ukifunguka kwake na kumwambia ukweli usifiche uhalisia wako utakuwa unajidanganya ww na kumdanganya huyo mwenza wako.Kama anakupenda atakupenda pamoja na kasoro zako.Tegemea vilevile kasoro yako hio inaweza kutumiwa kama fimbo ya kukuchapia mkikwaruzana..All in all natumai jamaa atakuwa muelewa.Kila la kheri

shosti wewe utakubali kaka yako amuoe x-changudoa???
najiona sifai kabisa
 
acheni uoga wa kunguru, kama ndoa ipo hakuna kizuizi, its only truth will set gateway of happier marriage.


Dhambi zingine tunatubu kwa Mungu tu bila kushirikisha wenzi wetu na tunaamini anatusamehe. Huyo binti aende faragha yeye na Mungu wake aombe msamaha, then atakuwa na amani ya moyo na maisha yataendelea.
 
Binadamu haeleweke unaweza kumwambia basi ikatokea lolote kwenye maisha yenu akachukulia tukio ulilomweleza lina apply sasa. Kabla ya kumweleza je ni mtu wa gubu na anachukuliaje vitu pale anapogundua au kujua kitu kidogo
i missed u alot bw
si mkorofi si mtu wa gubu wala mihasira ila kuna wakati tukichelewa iwe kwenye sherehe wakati tukirudi akiona machangudoa anasikitika na kuanza kuufokea mpaka usukani wa gari....roho huwa inaniuma sana
 
Back
Top Bottom