Nimeumizwa sana na Dr. Slaa

Nimeumizwa sana na Dr. Slaa

Taarifa niliyoisikia kutoka kwa Mwenyekiti wa CHADEMA kuwa wameridhia KATIBU mkuu wetu Dr Slaa, kupumzika kwa mda usio julikana. Kiukweli nimeumizwa na kusikitishwa kwa uamuzi huo wa Dr Slaa hasa nikikumbuka taabu na mateso aliyoyapata katika kukikuza na kukisimamia leo anaamua kuacha kwa namna alivyo amua kufanya.

Naomba nitumie fursa hii kumuomba mh😀r Slaa fikiri mara nne ni maumivu makali kiasi gani utakuwa umeyasababisha kwa watanzania wenzako na hasa tunao kuunga mkono na kutambua umuhimu wako na mchango wako ndani ya chama cha CHADEMA na UKAWA kwa ujumla tafadhari nakuomba rejea kambini kwa masilahi ya chama na Taifa.

Tabu tumepata sie watu wa chini tuliokuwa tunatembea kwa mguu na kujichangisha pesa zetu,Dr Slaa alikuwa analipwa milioni karibu Kumi kwa mwezi.Alikuwa anafanya kazi ya mshahara,mtu analipwa milioni kumi unataka alale? Lazima afanye kazi bwana.Kaacha ajira atakuja mwingine
 
Taarifa niliyoisikia kutoka kwa Mwenyekiti wa CHADEMA kuwa wameridhia KATIBU mkuu wetu Dr Slaa, kupumzika kwa mda usio julikana. Kiukweli nimeumizwa na kusikitishwa kwa uamuzi huo wa Dr Slaa hasa nikikumbuka taabu na mateso aliyoyapata katika kukikuza na kukisimamia leo anaamua kuacha kwa namna alivyo amua kufanya. Naomba nitumie fursa hii kumuomba mh😀r Slaa fikiri mara nne ni maumivu makali kiasi gani utakuwa umeyasababisha kwa watanzania wenzako na hasa tunao kuunga mkono na kutambua umuhimu wako na mchango wako ndani ya chama cha CHADEMA na UKAWA kwa ujumla tafadhari nakuomba rejea kambini kwa masilahi ya chama na Taifa.
We unajua ni maumivu kiasi gani aliyopata dk.slaa mara baada ya mtu aliyetajwa kwa ufisadi, kupokelewa na viongozi wachache wa cdm na kupewa nafasi kubwa kuliko dk.slaa aliyekipigania chama cha cdm hadi kikajengeka kiimani kwa watanzania walio wengi?
 
ANGALIZO KWA DR SLAA NA LOWASA
Kabla sijaanza kuelezea lolote napenda kumukumbusha Slaa ambaye ana taalum ya upadri.
Katika kitabu cha matendo ya Mitume kuna ushahidi kwa Sauli alikuwa muuaji na tena alikuwa anauwa mitume lakini alipata padiliko la kweli na kujiunga na mitume wengine.

Wakati Sauli anafanya hivyo Mitume wengine walianza kumunyanyapaa na kumuogopa lakini katika bibilia , imethibitishwa kwamba hadi leo Paulo (aliyekuwa Sauli) ndiye aliyefanya kazi kuliko Mitume wote.

Bila shaka kuna watu ndani ya Chadema na hata nje ya chadema wanataka kujenga hoja ya kumunyanyapa LOWASA ati ni Fisadi , hata mimi niliingia mtego huu lakini napenda kuhojhi yafuatayo:
(1)Lowasa amehama CCM na kwa hatua hiyo ameingamiza nafsi yake kwa kiwango Kikubwa.
(2)Lowasa yupo tayari kutumia Pesa yake na mali yake kubomoa CCM
(3)LOWASA anahasira kali na CCM na miungu watu ndani ya CCM
(4)LOWASA kama waziri Mkuu mstafu ametake risk ya Kifo kiasi kwamba anataka kupiga CCM kwa Nyaraka zito za Siri ambazo Slaa hawezi kuzielezea
(5) Lowasa anajua mikakati ya Wizi wa Kura ndani ya CCM kwa miakazaidi ya 40
(6) Ndani ya CCM hawakutarajia wala hawakuwahi kupanga kuwa mtu kama Lowasa ambaye amewshijka nafasi nyeti kama waziri mkuu anaweza kuasi serikali kiasi hiki
Huu uasi unatisha na haujawahi kutokea, na hata pale ulipojaribu kutokea wahusika hawakubaki hai
(7)Kwa sasa CCM wanahaha sana juu ya Lowasa kuchukua form. Mikakati ya CCM iliielekeza Nguvu kumshambulia Slaa lakini Mungu amebadili Plan ghafla na kumuleta Lowasa amabaye hawajajipanga nan i Pigo kubwa
(8)Kwa sasa Uasi uliojitokeza CCM ni vigumu kujua nani yupo kwa nani
Angalia mtandao wa Lowasa ndani ya CCM unatisha na umetulia Kimia.
Mtandao huu jumlisha nguvu ya Umma ni lazima CCM ibaki kama KANU
MAONI KWA SLAA.
(1)Wakati unagombea urais ulikuwa na Rozi Kamili ukamwacha na kumuoa Josephine
Rozi Kamili alikubali ujio wa Josephine lakini leo Josephine huyo amekuwa kikwazo kwa maamuzi yako.
(2)Mambo ya Chama huwezi kumuhusisha Mwanamke, huo ni udhaifu mkubwa na kama kweli unamsikiliza mwanamke basi ujue hutapata nafsi ya kurudi kwenye jamii na wakakuamini na kukupa heshima kama walivyokupa.
Mke ni mshauri wake kwa mambo yote lakini kikao kama kamati kuu kinapopitisha maamuzi harafu mkeo anapinga maana yake mke huyo hafai kuwa First Lady na hata wewe hufai kuwa Kiongozi
MAONI KWA LOWASA
(1)Umeitwa Mwizi kwa siku nyingi sana na hata mimi nimekuita hivyo , sasa huu ni wakati wa wewe kutuambia mwizi halisi ni nani na utoe Ushahidi
(2) Zipo taarifa kwamba CCM wanapanga kukata jina lako kwenyenye tume ya uchaguzi hivyo nakusihii usikate tama .Muombe Mungu .Hii ni safari ya ushindi na si matumaini tena
(3)Usiogope kushambulia Ikulu kwa kuwa Mussa alikaa Ikulu ya Farao na kulelewa hapo lakini Mungu alimupa kazi ya kumuangamiza Farao.
Hivyo Lowasa umepewa kazi ya Kuingamiza CCM hivyo fanya kweli ujue kwamba Slaa hajui haya.

Natamani ujumbe huu ungebebwa na wazee waliojawa HEKIMA, BUSARA na UCHAJI WA MUNGU na kumfikishia Dr. SLAA mahali popote alipo ili aweze kuutafakari kwa kina. Hakika uamuzi wake utakuwa umewakwaza wengi na kwa upande mwingine itakuwa ni furaha na faraja kwa wote wasioitakia mema MAMA TANZANIA.

Dr. SLAA sikia kilio, kiu na matamanio ya wazalendo wa nchi yetu. Hakika bado unahitajika na ni vyema ukatambua wazi kuwa hata MATEKA WA VITA na WALE WANAOJISALIMISHA hutumiwa pia kama SILAHA na NYENZO NZURI katika kukabiliana na ADUI kwa minajili ya KUPATA USHINDI.

LOWASA japo ametuhumiwa kwa mengi lakini kwa kujisalimisha kwake anaweza kutumiwa kama NYENZO na SILAHA nzuri katika kupambana na adui CCM na hatimaye kupata USHINDI
 
Msimamo wangu kuhusu Dr.Slaa: Rai yangu ni kwamba waafrika tubadilike kisiasa. Tujenge MIFUMO IMARA ya kisiasa (strong political institutions), siyo kutengeneza MABABE WA KISIASA(strong men). Dr.Slaa kwa uamuzi wake alioufanya akiwa na akili timamu wa "kujificha", ni ushahidi tosha ya kwamba amevaa joho la UBABE dhidi ya mfumo wa chama chake. Hii siyo demokrasia ya kimamboleo ambayo imejengwa ktk misingi ya "wengi wape,wachache wasikilizwe". Alisikilizwa.Dr. Slaa ameshindwa kabisa kuonyesha ukomavu wa kisiasa. Ni dhaifu. Kama hakubaliani na maamuzi halali ya chama chake, basi ajiunge na chama kingine(ana haki) ikimpendeza, au atangaze kufilisika kisiasa. Sina sababu za msingi za kumbembeleza, na nawapuuza wanaombembembeleza kama ninavyompuuza anayejenga mazingira ya kupata umaarufu kwa kubembelezwa. Hayo ni mambo ya zamani sana. Msingi wa chama cha siasa siyo "mtu", bali ni mfumo imara na sera safi za chama husika. Tuondoe HOFU za bandia.
 
Hakuna maumivu,,hapo huwez kukaribisha wez kwenye ukomboz,,,Slaa yuko sahihi mwache apumzike tu.....
 
hiyo ndio ilikuwa hoja ya Slaa lkn akaambiwa yeye sio altimatum na kama hataki aondoke Chamani-dharau na dhihaka

Hata kama Kamati Kuu ya CDM ilikuwa na nia njema kiasi gani ilishindwa kuwa proactive except Dr.Slaa naona ndiye aliyebaki proactive ni Slaa who has decided to stick to values and principles. The rest have decided to make decisions however big they are based on events, conditions, audience moods and what have you. Kama ambavyo watu wanataka Slaa aheshimu matakwa ya wengi lakini na wao wengi wanatakiwa waheshimu values and principles of CDM na za Slaa as a person and charismatic leader. Kwa kuwa ndani ya Katiba ya CDM hakuna kanuni inayosema karibisha mtu anayekuja na mafuriko. Kilichoangaliwa ni ushindi kuliko kuangalia unaupataje. Tunu na kanuni zilizoifanya CDM ikakwa tofauti na vyama vingine vitaenziwa na watu ambao hawajakuzwa na CDM? mfano wa Saul wa Biblia anayekuja kugeuka na kuitwa Paulo unaweza ukawa sahihi au usiwe sahihi. Kung'oka kwa Paulo ulikuwa mpango wa kinabii na sasa tunapaswa basi kutopuuza tunu na kanuni bali ushawishi wa kumleta Dr.Slaa akiwa hajapunguza hata tone la values na principles ili ziwe labda ni kichocheo cha Lowasa kubadilika kweli kuwa Saul. Halafu Mweyekiti Mbowe na Kamati wanapaswa kukubali kuwa wamekosea na wao kama binadamu kwa kutumia majority dictatorship na kufanya maamuzi kwa kuangalia miemuko ya kisiasa
 
Kusamehe ni tabia ya kristo yesu alikaa na maadui. Dr hili lifikilie kwa makini naamini upadrii bado umo moyoni mwako ni Mimi mwinjilist.

Sisi ndo tunapaswa kumsamehe Lowasa, Slaa hana ugomvi na Lowassa..slaa ana ugomvi na rushwa na ufisadi. Naheshimu maamuzi yake
 
Msimamo wangu kuhusu Dr.Slaa: Rai yangu ni kwamba waafrika tubadilike kisiasa. Tujenge MIFUMO IMARA ya kisiasa (strong political institutions), siyo kutengeneza MABABE WA KISIASA(strong men). Dr.Slaa kwa uamuzi wake alioufanya akiwa na akili timamu wa "kujificha", ni ushahidi tosha ya kwamba amevaa joho la UBABE dhidi ya mfumo wa chama chake. Hii siyo demokrasia ya kimamboleo ambayo imejengwa ktk misingi ya "wengi wape,wachache wasikilizwe". Alisikilizwa.Dr. Slaa ameshindwa kabisa kuonyesha ukomavu wa kisiasa. Ni dhaifu. Kama hakubaliani na maamuzi halali ya chama chake, basi ajiunge na chama kingine(ana haki) ikimpendeza, au atangaze kufilisika kisiasa. Sina sababu za msingi za kumbembeleza, na nawapuuza wanaombembembeleza kama ninavyompuuza anayejenga mazingira ya kupata umaarufu kwa kubembelezwa. Hayo ni mambo ya zamani sana. Msingi wa chama cha siasa siyo "mtu", bali ni mfumo imara na sera safi za chama husika. Tuondoe HOFU za bandia.
 
Huyu babu, bora afe tu hakiri zake zimezeeka,kwani yy haoni hata kenya walifanyaje?, Tafadhali josophine huyo babu mushauli arudi kazini. Elewe kuwa huyo Dr ana miaka michache sana hapa duniani anahitajika kwa Mungu. Sasa ukimung'ang'ania muwe munashinda nae ndani utaishije ck babu akifa.
 
Cdm nadhani waroho,ila mzee nafsi imetosheka,,maandiko yanasema; haitamfaa mali yake wala alichokichuma,ila matendo yake tu...hivo bas slaa yuko sahihi hanunuliki kwa ngawira ambazo huzikwi nazo......safi mzee Slaa
 
Slaa alipoukosa uaskofu jimbo kuu la arusha akaanza kuacha upadre
 
Hata kama Kamati Kuu ya CDM ilikuwa na nia njema kiasi gani ilishindwa kuwa proactive except Dr.Slaa naona ndiye aliyebaki proactive ni Slaa who has decided to stick to values and principles. The rest have decided to make decisions however big they are based on events, conditions, audience moods and what have you. Kama ambavyo watu wanataka Slaa aheshimu matakwa ya wengi lakini na wao wengi wanatakiwa waheshimu values and principles of CDM na za Slaa as a person and charismatic leader. Kwa kuwa ndani ya Katiba ya CDM hakuna kanuni inayosema karibisha mtu anayekuja na mafuriko. Kilichoangaliwa ni ushindi kuliko kuangalia unaupataje. Tunu na kanuni zilizoifanya CDM ikakwa tofauti na vyama vingine vitaenziwa na watu ambao hawajakuzwa na CDM? mfano wa Saul wa Biblia anayekuja kugeuka na kuitwa Paulo unaweza ukawa sahihi au usiwe sahihi. Kung'oka kwa Paulo ulikuwa mpango wa kinabii na sasa tunapaswa basi kutopuuza tunu na kanuni bali ushawishi wa kumleta Dr.Slaa akiwa hajapunguza hata tone la values na principles ili ziwe labda ni kichocheo cha Lowasa kubadilika kweli kuwa Saul. Halafu Mweyekiti Mbowe na Kamati wanapaswa kukubali kuwa wamekosea na wao kama binadamu kwa kutumia majority dictatorship na kufanya maamuzi kwa kuangalia miemuko ya kisiasa

Watu wanasahau Dr.Slaa alikua tayari kumuachia Samuel Sitta 2010, Mbowe anaoverlook mambo kwa majority rule ambayo inaignore basics and principles. Ajabu sana leo Chadema mtu akiwa muwahi kwa dhamira yake anaonekana adui, wataukumbuka huu mwaka kwa uamuzi wanaoufanya. Namashaka na thinking capacity na nia ovu ya viongozi wa Chadema.
 
eti arudi ccm amekataa limssfisha fisadi mmoja ndo akasafishe lundo ya ccm wote mafisadi
 
Kwani hata Dr. Slaa angesimamishwa kugombea urais kupitia ukawa angeshinda? Mm nahakika asingeshinda. Nguvu alionayo Lowasa na uwingi wa wafuasi wake ni dhahiri atashinda.Dr Slaa angeungana na wapambanaji wengine kuing'oa ccm.maana nia ni kuiondoa ccm madarakani

Lowasa alidhaminiwa na wanaccm laki moja na huku chadema 1.6 milioni, jumla 2.4. Je, hizi ndizo kura atakazopata mwezi oktoba ?
 
Kwani hata Dr. Slaa angesimamishwa kugombea urais kupitia ukawa angeshinda? Mm nahakika asingeshinda. Nguvu alionayo Lowasa na uwingi wa wafuasi wake ni dhahiri atashinda.Dr Slaa angeungana na wapambanaji wengine kuing'oa ccm.maana nia ni kuiondoa ccm madarakani

Lowasa alidhaminiwa na wanaccm laki nane na huku chadema 1.6 milioni, jumla 2.4. Je, hizi ndizo kura atakazopata mwezi oktoba ?
 
Dr Slaa alipaswa kuelewa kuwa mabadiliko ni muhimu sana pasipo kujali mabadiliko hayo yanaletwa na nani. Kama CCM walishasema watashinda hata kwa goli la mkono, ilikuwa muhimu sana kwa UKAWA nao kuhakikisha wanashinda kwa goli la mikono miwili. Walichofanya CHADEMA na UKAWA kwa ujumla kilikuwa muhimu sana kwa wakati huu tulionao. Kujiondoa kwa Dr Slaa kunamfanya aoneshe dhahiri ubinafsi wake.
 
Back
Top Bottom