Nimeumizwa sana na Dr. Slaa

Nimeumizwa sana na Dr. Slaa

Siipendi cdm. Lkn msimamo wa dk Slaa taukumbuka daima. Huyu mtu ana sifa zote, msomi, mkongwe na mweledi wa siasa. Anajipambanua kwa kuchukia wahujumu uchumi/mafisadi. Sioni muujiza wowote wa kumkutanisha na Lowasa. Slaa hana bei ila ana principal anazoishi nazo. Utu wake uko kwenye ukweli wake. Namshauri aende CCM, CCM wamemsikia wamemwelewa na wameanza kazi ya kuwafyeka mafisadi. Slaa anajua ufisadi ni hulka, haupo ktk maandiko ya vyama. Kwa hiyo, mtu anahama na hulka na anaachana na makatazo ya maandiko!!!

wewe jamaa ni mwandishi mzuri sana, yaan sentens chache ambazo meseji yake ni kitabu kizima-ningetaman Dr Slaa aisome hii, tupia km thrread/kigodoro
 
ANGALIZO KWA DR SLAA NA LOWASA
Kabla sijaanza kuelezea lolote napenda kumukumbusha Slaa ambaye ana taalum ya upadri.
Katika kitabu cha matendo ya Mitume kuna ushahidi kwa Sauli alikuwa muuaji na tena alikuwa anauwa mitume lakini alipata padiliko la kweli na kujiunga na mitume wengine.

Wakati Sauli anafanya hivyo Mitume wengine walianza kumunyanyapaa na kumuogopa lakini katika bibilia , imethibitishwa kwamba hadi leo Paulo (aliyekuwa Sauli) ndiye aliyefanya kazi kuliko Mitume wote.

Bila shaka kuna watu ndani ya Chadema na hata nje ya chadema wanataka kujenga hoja ya kumunyanyapa LOWASA ati ni Fisadi , hata mimi niliingia mtego huu lakini napenda kuhojhi yafuatayo:
(1)Lowasa amehama CCM na kwa hatua hiyo ameingamiza nafsi yake kwa kiwango Kikubwa.
(2)Lowasa yupo tayari kutumia Pesa yake na mali yake kubomoa CCM
(3)LOWASA anahasira kali na CCM na miungu watu ndani ya CCM
(4)LOWASA kama waziri Mkuu mstafu ametake risk ya Kifo kiasi kwamba anataka kupiga CCM kwa Nyaraka zito za Siri ambazo Slaa hawezi kuzielezea
(5) Lowasa anajua mikakati ya Wizi wa Kura ndani ya CCM kwa miakazaidi ya 40
(6) Ndani ya CCM hawakutarajia wala hawakuwahi kupanga kuwa mtu kama Lowasa ambaye amewshijka nafasi nyeti kama waziri mkuu anaweza kuasi serikali kiasi hiki
Huu uasi unatisha na haujawahi kutokea, na hata pale ulipojaribu kutokea wahusika hawakubaki hai
(7)Kwa sasa CCM wanahaha sana juu ya Lowasa kuchukua form. Mikakati ya CCM iliielekeza Nguvu kumshambulia Slaa lakini Mungu amebadili Plan ghafla na kumuleta Lowasa amabaye hawajajipanga nan i Pigo kubwa
(8)Kwa sasa Uasi uliojitokeza CCM ni vigumu kujua nani yupo kwa nani
Angalia mtandao wa Lowasa ndani ya CCM unatisha na umetulia Kimia.
Mtandao huu jumlisha nguvu ya Umma ni lazima CCM ibaki kama KANU
MAONI KWA SLAA.
(1)Wakati unagombea urais ulikuwa na Rozi Kamili ukamwacha na kumuoa Josephine
Rozi Kamili alikubali ujio wa Josephine lakini leo Josephine huyo amekuwa kikwazo kwa maamuzi yako.
(2)Mambo ya Chama huwezi kumuhusisha Mwanamke, huo ni udhaifu mkubwa na kama kweli unamsikiliza mwanamke basi ujue hutapata nafsi ya kurudi kwenye jamii na wakakuamini na kukupa heshima kama walivyokupa.
Mke ni mshauri wake kwa mambo yote lakini kikao kama kamati kuu kinapopitisha maamuzi harafu mkeo anapinga maana yake mke huyo hafai kuwa First Lady na hata wewe hufai kuwa Kiongozi
MAONI KWA LOWASA
(1)Umeitwa Mwizi kwa siku nyingi sana na hata mimi nimekuita hivyo , sasa huu ni wakati wa wewe kutuambia mwizi halisi ni nani na utoe Ushahidi
(2) Zipo taarifa kwamba CCM wanapanga kukata jina lako kwenyenye tume ya uchaguzi hivyo nakusihii usikate tama .Muombe Mungu .Hii ni safari ya ushindi na si matumaini tena
(3)Usiogope kushambulia Ikulu kwa kuwa Mussa alikaa Ikulu ya Farao na kulelewa hapo lakini Mungu alimupa kazi ya kumuangamiza Farao.
Hivyo Lowasa umepewa kazi ya Kuingamiza CCM hivyo fanya kweli ujue kwamba Slaa hajui haya.

Kwani Paul aliendea kuwachukia watu kwa kiasi hicho?
Mtu hawezi ukatumia pesa nyingi sana kupata madaraka afu ukawa na malengo mazuri?
 
Inaskitisha na inanisononesha kwa uamuzi wako dr slaa.Hata kama umeingia kinyongo hukupaswa kuamua katika kipindi hiki tunapoelekea kwenye uchaguzi,naomba urudi tuendelee kuiokoa nchi hii

Kwanini na wenyewe wamenfanyia hicho wakati huu
 
Amani iwe kwenu watanzania wote!

Kumekuwa na mtikisiko ndani ya Chadema baada ya Dr slaa kutoonekana ndani ya vikao vya chama. Bila Dr slaa Lowassa huwezi kushinda urais hili liko wazi.

Kama unania njema ya kwenda Ikulu nakuomba kwa kutumia hiyo nia njema liunganishe Taifa kwanza kwa kumrudisha Dr Slaa Chadema. Ukishindwa hilo najua wewe ni msanii hutufai umekuja kutubomoa!

Nimekuwa kwenye maombi kwa siku 5 bila kula mlo wa kutosheleza ili Dr slaa arudi Chadema.

Mungu ibariki Chadema, Mungu mbariki Dr slaa, Mungu ibariki Tanzania.
Amina!
 
ANGALIZO KWA DR SLAA NA LOWASA
Kabla sijaanza kuelezea lolote napenda kumukumbusha Slaa ambaye ana taalum ya upadri.
Katika kitabu cha matendo ya Mitume kuna ushahidi kwa Sauli alikuwa muuaji na tena alikuwa anauwa mitume lakini alipata padiliko la kweli na kujiunga na mitume wengine.

Wakati Sauli anafanya hivyo Mitume wengine walianza kumunyanyapaa na kumuogopa lakini katika bibilia , imethibitishwa kwamba hadi leo Paulo (aliyekuwa Sauli) ndiye aliyefanya kazi kuliko Mitume wote.

Bila shaka kuna watu ndani ya Chadema na hata nje ya chadema wanataka kujenga hoja ya kumunyanyapa LOWASA ati ni Fisadi , hata mimi niliingia mtego huu lakini napenda kuhojhi yafuatayo:
(1)Lowasa amehama CCM na kwa hatua hiyo ameingamiza nafsi yake kwa kiwango Kikubwa.
(2)Lowasa yupo tayari kutumia Pesa yake na mali yake kubomoa CCM
(3)LOWASA anahasira kali na CCM na miungu watu ndani ya CCM
(4)LOWASA kama waziri Mkuu mstafu ametake risk ya Kifo kiasi kwamba anataka kupiga CCM kwa Nyaraka zito za Siri ambazo Slaa hawezi kuzielezea
(5) Lowasa anajua mikakati ya Wizi wa Kura ndani ya CCM kwa miakazaidi ya 40
(6) Ndani ya CCM hawakutarajia wala hawakuwahi kupanga kuwa mtu kama Lowasa ambaye amewshijka nafasi nyeti kama waziri mkuu anaweza kuasi serikali kiasi hiki
Huu uasi unatisha na haujawahi kutokea, na hata pale ulipojaribu kutokea wahusika hawakubaki hai
(7)Kwa sasa CCM wanahaha sana juu ya Lowasa kuchukua form. Mikakati ya CCM iliielekeza Nguvu kumshambulia Slaa lakini Mungu amebadili Plan ghafla na kumuleta Lowasa amabaye hawajajipanga nan i Pigo kubwa
(8)Kwa sasa Uasi uliojitokeza CCM ni vigumu kujua nani yupo kwa nani
Angalia mtandao wa Lowasa ndani ya CCM unatisha na umetulia Kimia.
Mtandao huu jumlisha nguvu ya Umma ni lazima CCM ibaki kama KANU
MAONI KWA SLAA.
(1)Wakati unagombea urais ulikuwa na Rozi Kamili ukamwacha na kumuoa Josephine
Rozi Kamili alikubali ujio wa Josephine lakini leo Josephine huyo amekuwa kikwazo kwa maamuzi yako.
(2)Mambo ya Chama huwezi kumuhusisha Mwanamke, huo ni udhaifu mkubwa na kama kweli unamsikiliza mwanamke basi ujue hutapata nafsi ya kurudi kwenye jamii na wakakuamini na kukupa heshima kama walivyokupa.
Mke ni mshauri wake kwa mambo yote lakini kikao kama kamati kuu kinapopitisha maamuzi harafu mkeo anapinga maana yake mke huyo hafai kuwa First Lady na hata wewe hufai kuwa Kiongozi
MAONI KWA LOWASA
(1)Umeitwa Mwizi kwa siku nyingi sana na hata mimi nimekuita hivyo , sasa huu ni wakati wa wewe kutuambia mwizi halisi ni nani na utoe Ushahidi
(2) Zipo taarifa kwamba CCM wanapanga kukata jina lako kwenyenye tume ya uchaguzi hivyo nakusihii usikate tama .Muombe Mungu .Hii ni safari ya ushindi na si matumaini tena
(3)Usiogope kushambulia Ikulu kwa kuwa Mussa alikaa Ikulu ya Farao na kulelewa hapo lakini Mungu alimupa kazi ya kumuangamiza Farao.
Hivyo Lowasa umepewa kazi ya Kuingamiza CCM hivyo fanya kweli ujue kwamba Slaa hajui haya.
Naunga mkono hoja .naomba Mungu ujumbe huu usomwe na Dr Slaa .na haupokee kama ujumbe rasmi kutoka kwa wanachadema wote Tanzania.kwa kumalizia .ataa akisusa sisi tunaendelea hatuna namna ccm out 2015 ni lazima. .SAUTI YA WENGI NI SAUTI YA MUNGU.
 
Kwako katibu wetu mkuu Dr W. Slaa, mi ni mwananchi wa kawaida kabisa nimeona nami nijaribu kukufikia kwa njia hii kwa kuwa siwezi kufika nyumbani kwako pia siwezi kukufikia kwa simu. Hivyo kwa heshima kubwa nakuomba Mheshimiwa uusome ujumbe huu huku ukiwaza kuwa tupo wananchi wengi sana wa aina yangu ambao wangependa kukutana nawe na kukueleza haya nitakayokuomba.

Mwaka 2010 ndiyo mwaka ambao chama cha Chadema kilikua kwa kasi ya ajabu hii ilitokana na uamuzi wako wa kugombea urais baada ya kuombwa na chama, na toka wakati huo umekuwa unaishi mioyoni mwa watu tukiamini siku moja utakuja kuongoza watanzania kwani ni dhahiri pasipo shaka wewe ni mtu msafi.

Dr. Umekuwa mvumilivu sana toka kuisha kwa ule uchaguzi wa 2010 wewe pamoja na mama yetu Josephine mmetukanwa sana kwenye hii mitandao na wana CCM na ndio ambao wameendelea na kejeli zao kwa kujifanya wana chadema ili tu uudhike na pengine kuamua kuachana na Chadema ili lengo lao litimie. Dr, wananchi tulio wengi kweli kabisa tulipenda wewe uwe mgombea urais.

Sasa ombi langu kwako ambalo ndilo la watanzania wengi kwa heshina kubwa nakuomba Dr sikia kilio cha watanzania rudisha moyo wako Dr umekuwa mtu thabiti wakati wote.

Mama Josephine wewe ni mtu muhimu sana kwa kuwa hakuna linalofanyika na Dr wewe usijue wewe ndio mshauri wake wa karibu, Mama kwa heshima kubwa nakuomba rudisha moyo wako muendeleze mapambano.

Watanzania watafurahi sana endapo watawaona mmetokea kwenye vikao vya chama vinavyoendelea.

Mungu awape nguvu na ustahimilivu na kusahau makwazo yote kama yapo unganeni na viongozi wenzenu kwa PAMOJA TUTASHINDA.
 
dk slaa kwisha habari yake kwan anahatimiliki ya kugombea urais
 
Dr Slaa plz rudi kambini lengo ni kuiondoa CCM madarakani tu
 
Huo wote. ...ni mchezo. ...wanapima upepo kama upepo ukikaa sawa Dr anafanya come back ambayo itaongeza nguvu ya kampeni
 
Kwa kweli pamoja na ujio wa mwamba wa kaskazini, kuleta amsha amsha, Lowassa hakutakiwa kupewa nafasi ya juu kiuongozi. kwanza hajakijenga chama. Yeye alitakiwa kuandamana na MTU ambaye angeteuliwa kugombea urais kwenye mikutano yote ya campaign.

Kwa kweli Dr upo sahihi sana kwa maamuzi yako. Naomba tuheshimu maamuzi yake.

Sio chadema hii .chadema ni mpango wa Mungu .atudanganyiki .asuse sisi tunaendelea hatuna namna ccm out 2015 nilazima .Sauti ya wengi ni sauti ya Mungu .wewe na Dr ninani muweze kumkwaza Mungu.
 
Tumeyaheshimu na tunaendelea kuyaheshimu maamuzi yake....

Ndio maana tumeamua kuendelea kwa sababu wengine katika chama tuko tayari kuendelea na yeye atakapokuwa tayari atatujoin mbele ya safari...

Kwa kweli pamoja na ujio wa mwamba wa kaskazini, kuleta amsha amsha, Lowassa hakutakiwa kupewa nafasi ya juu kiuongozi. kwanza hajakijenga chama. Yeye alitakiwa kuandamana na MTU ambaye angeteuliwa kugombea urais kwenye mikutano yote ya campaign.

Kwa kweli Dr upo sahihi sana kwa maamuzi yako. Naomba tuheshimu maamuzi yake.
 
wengi wape!,

SHETAN WA HILA NA CHUKI NA ASHINDWE!

PEPO YEYOTE AWAYE KTK MWONEKANO WA KIBINADAMU AMPOTOSHAYE SLAA FINAIKUL MAUTI IWE JUU YAKE!

AMIIN

ii
 
Dr rudi tu cdm, kwani si unajua hata wewe hukua na ushahidi wa kumtuhumu Ngoyai?
Na ukae ukielewa kwamba bila wanachama wa ccm kuhama chama chao, upinzani hauwezi kushika hatamu!
 
Kusamehe ni tabia ya kristo yesu alikaa na maadui. Dr hili lifikilie kwa makini naamini upadrii bado umo moyoni mwako ni Mimi mwinjilist.
 
chadema ni taasisi hivyo kama kiongozi hataki kukubaliana na maamuzi ya kikao basi hana tena mamlaka ya kuwa ofisini
 
Dr Slaa ana kura moja tu, haitomfanya lowasa asiingie ikulu wakati tunaambiwa kaja na mamilioni.
 
Back
Top Bottom