Nimeumizwa sana na Dr. Slaa

Nimeumizwa sana na Dr. Slaa

Sio chadema hii .chadema ni mpango wa Mungu .atudanganyiki .asuse sisi tunaendelea hatuna namna ccm out 2015 nilazima .Sauti ya wengi ni sauti ya Mungu .wewe na Dr ninani muweze kumkwaza Mungu.

Nendeni hamjafungwa lakini kuna mto una MAMBA mbele msisahahu mkatukana,kumbe hajavuka bado..............
 
Hili furukoto na timbwili lililotokea ndani ya CHADEMA kutokana na ujio si tu wa Lowassa kuingia CHADEMA, bali kupewa fursa kuwa mgombea wa nafasi ya urais, matokeo yake yameanza kuonekana wazi.

Wanamageuzi si tu wameshikwa na bumbuazi kwa mabadiliko haya ya ghafla katika uongozi wa CHADEMA bali vile vile muelekeo wa chama chenyewe.

Mimi siamini kana Lowassa pamoja na marafiki zake wana nia ya dhati ya wanachadema katika kuleta mageuzi.
Tunachokubaliana na Lowassa ni kwamba yeye anapenda kwenda zikulu na sisi tunataka kuiondoa CCM.

Zaidi ya hapo Lowassa si mwana CHADEMA wa kupikwa akaiva.
Na hapo mdo namuunga mkono Dr Slaa.

Hata hivyo timbwili hili ni kama manna iliyotelemka toka mbinguni kwa CCM.
Tujitayarishe kwamikwara mizito watakayoitumia kuendkeza mtafaruku huu.
 
Slaa hawezi kula matapishi yake
 
Kwani Paul aliendea kuwachukia watu kwa kiasi hicho?
Mtu hawezi ukatumia pesa nyingi sana kupata madaraka afu ukawa na malengo mazuri?

Umebamiza ndugu ASANTE.Halafu hatujiulizi atazirudishaje?Au ndiyo miaka mingine 10 ya kurudisha madeni ya uchaguzi?
 
Huenda tukabaki wachache sana tusionunulika, kweli sote ni wapinzani, na hoja kubwa ni kuiondoa CCM na mfumo wake wa kifisadi. Lakini mara fisadi mkuu ambaye hata mafisadi wenzake wamemkataa ananunua chama chetu fasta. Tunampokea na kumshangilia kama mazuzu.
Hapana, nasema hapana, mkikumbatia ufisadi na fedha za akina Rostam mmetupeleka siko, aheri Dr Slaa amesema hapana! mnaomkejeli kuwa ana uroho wa madaraka ebu kesho muwekeni Mnyika au mwingine muone kama Dr. hajaunga mkono, anachopinga ni Mbowe na wezake kumwita fisadi eti leo ni malaika na mkombozi wa Tanzania.
Bora tubaki wachache na dhamiri zetu safi, nje ya vyama kwani CHADEMA IMENUNULIWA!
 
Tawashangaa CCM kama hawatomfuata Slaa kumshawishi arudi ccm kusaidia chama kusafisha mafisadi. Slaa ni mtu muhimu sana, ccm inatakiwa isilale hadi impate dk Slaa, mpambanaji wa kweli wa mafisadi.

Mh!Hawawezi kumpata hata kwa dawa.
 
Lowasa unapaswa kuonyesha ubora wowote alionao katika hili. Umekuja CHADEMA baada ya kuona kiko safi na imara na kwamba kinakubalika ili udandie muunganishe nguvu. Wewe lengo lako likiwa ni kuiua ccm na kuwa raisi, huku ukitambua uwezo wako mdogo wa kujenga chama na hivyo ukitambua umahiri wa dr. Slaa katika kujenga chama na taifa imara.

Ukiona uliowakuta wanakukimbia, ujue wanakimbia na mchango wao katika kufanikisha azma yako pia. Hutaenda ikulu kwa mteremko wa CHADEMA uliyoikuta bila Dr. Slaa. Na sasa bila Dr. Slaa unaonekana wewe ni laana, umeleta laana CHADEMA kitu ambacho unapaswa kukikataa.

Ninakushauri kwamba umwombe Mungu sana akuondolee kiburi na hasira, pamoja na roho ya visasi uliyonayo.

Pili unatakiwa kuita press comference uruhusu maswali yote kutoka kwa waandishi ambayo wana maduku duku nayo juu ya histori yako iliyojaa maswali. Kuwajibu watu kwa kejeli kwamba mwenye ushahidi aende mahakamani, ni kashfa kwasababu ukweli unaujua.

Tatu sina imani na upenzi wako juu ya ChADEMA kama chama,ila katika ufahamu wangu naona unakipenda chaddema kama mtumbwi wa kukupeleke ikulu. Na hivo imani yetu kwako bila viongozi waliotufikisha hapa, haipo. Peke yako hukubaliki CHADEMA. Ili tujue chama chetu kinaendelea kuwa salama, na kwamba hata ukiwa Ikulu utaendeleza itikadi za CHaDEMa kwa ubora wake, tunataka uwarudishe viongozi wetu wanaokukumbia. Hao ndi tunaowaamini na siyo wewe kama wewe. Bila hivyo, hatukupeleki Ikulu Mheshimiwa kwa sasa. Tutahitaji kukaa na wewe miaka mitano ili tukufahamu rangi yako halisi juu ya uzalendo unaotaka tuuamini.


Nne, ninaomba Mungu uongee na wanasheria wa UKaWA juu ya maisha yako ukiwa ulikotoka ili wapime na kuona kama huna kosa la kuwekewa pingamizi tukakosa mgombea kwa ajili ya tamaa zako kumbe huna hata sifa.

Tano wafuasi wako, waambie wawe na adabu. Waache kukupigia debe kwa kumtukana Dr. Slaa wakidhani watamdhdoofisha iili upate nafasi ya bure usije kukatwa na huku. Tunawaelewa kwamba wengi ni wahuni tu hapa mitandaoni. Lakini wafahamu kwamba wanavyomtukana Dr. wanazidi kukuweka mbali na mioyo yetu. Ongea na watu wako uwaambie huku siyo ccm, hakuna cha kulilndana, wala kusimamia uovu.

Ukimrudisha Dr. Slaa, tutaungana kukupigia kampeni za nguvu tukiamini hujaleta laana ya mafarakano na kwa tamaa zako unaua CHADEMA.

Ninaomba Mh. Lowasa uingie kazini wala usikae kama mgeni ili ueleweke na upate Support ya CHADEMA ambayo ni muhimu sana kuliko madonda na vinyongo vilivyopo sasa dhidi yako.
 
Slaa hawezi kula matapishi yake
hilo ni jema,ila tukubaliane sasa kuwa ni mnafiki na kigeugeu.wote tumelalama hapa kuwa Jk ni kigeugeu,sasa Dr.Slaa na JK hawana tofauti ktk hili?
 
Dk ameishavibaya kwa umri alionao ajiandae kwenda kuuza mchicha sio urais
 
Amani iwe kwenu watanzania wote!

Kumekuwa na mtikisiko ndani ya Chadema baada ya Dr slaa kutoonekana ndani ya vikao vya chama. Bila Dr slaa Lowassa huwezi kushinda urais hili liko wazi.

Kama unania njema ya kwenda Ikulu nakuomba kwa kutumia hiyo nia njema liunganishe Taifa kwanza kwa kumrudisha

Dr Slaa Chadema. Ukishindwa hilo najua wewe ni msanii hutufai umekuja kutubomoa!

Nimekuwa kwenye maombi kwa siku 5 bila kula mlo wa kutosheleza ili Dr slaa arudi Chadema.

Mungu ibariki Chadema, Mungu mbariki Dr slaa, Mungu ibariki Tanzania.
Amina!

Unaweza usile, usinywe n.k unavyoita eti unafunga, haya hata kuoga usioge.Dr Slaa ameomba apumzike kwa muda, hajatangaza kuacha chama, viongozi bado wapo na kumbuka yeye hakutangazwa mgombea wa chadema, na chama sio mtu mmoja. Kinachokuuma kinajulikana wazi impact ya Dr Slaa kupumzika na sio kuacha chama ni ndogo sana kwa chadema ukilinganisha na impact ya Lowasa kuhama CCM kwa CCM
 
Dr. Kumbuka MUNGU alivomtumia malaya Rahab kuwasaidia wana wa Israel kushinda vita dhidi ya adui zao ambao walikuwa ni ndugu na jamaa za huyo malaya. Vivyo hivyo Mungu anaweza kimtumia Lowassa mtuhumiwa wa ufisadi kuwasaidia watz kuwaangusha ccm kiwanda cha mafisadi na wauwaji. "TAZAMA YA KALE YAMEPITA NA SASA YAMEKUWA MAPYA" MUNGU AKUBARIKI SANA WEWE NA FAMILIA YAKO.
 
Hili ni doa kubwa sana. Dr namshauri kukubali kujishusha ili tupate upinzani wa kweli. Akubali win win situation. Kiukweli muda huu ulitakiwa utumike katika Umoja na Mshikamano mkubwa. Kama hali hii itaendelea, ni doa kubwa sana!
hakuna umoja na mafisadi wananchi wanatuelewaje? jana tunasema fulani fisadi leo shujaa, NOT POSIBO
 
Ila kuhusu Dr slaa kuonesha kutoridhika na ujio wa Lowassa ndan ya CHADEMA na kupewa hidhini ya kupepelisha bendera ya CHADEMA ni kutokana na yeye kutaka pia kugombea urais kwa ticket ya CHADEMA
 
Mbowe na mashabiki wake wanaweza wasielewe madhara ya hii hatua wanayoipigia debe sasa, ila ukweli unabaki palepale kwamba Chadema sasahivi haijulikani inapigania nini. Mimi kama mwananchi wa kawaida sijui misingi ya itikadi ya Chadema ni ipi kwa sasa.Je ni kuingia ikulu tu; na wakishindwa kuingia ikulu Chadema watatuambia nini, wakati tayari wameshakana "principles" zao; kwamba wao ni chama kinachopinga ufisadi nchini? Najiuliza, next time Chadema watasafiri kwenda nchi tajiri kutafuta support ya kitu gani kama wameamua kwamba ufisadi siyo vita wanayopigana nayo?
 
Pongezi zinatoka CCM.Katika upinga ufisadi Dr.Slaa amemtaja JK kuwa fisadi no.7 je mnaunga mkono na hili
 
Back
Top Bottom