Nimeumizwa sana na Dr. Slaa

Nimeumizwa sana na Dr. Slaa

Mkuu kamanda sio mbinafusi ila anajaribu kusimamia alicho kiamini tangu mwanzo

Mkuu, naamini kabla ya Dokta kuamini kwamba Lowassa ni Fisadi, alikuwa padre na aliamini kwamba msamaha na kusamehe ni wajibu wake kama mkristo.. kwa hivyo kama suala ni alivhokiamini tangu mwanzo Basi ni Msamaha tu...
 
Naaam hilo ndilo ombi langu kwake
 
Ni dhahiri kuwa maamuzi ya mtu hutegemea na mtazamo alionao na hisia juu ya jambo analotaka kulifanyia maamuzi. Kimsingi Dr. Slaa ni mtu mwenye hisia za ndani na dhamiri inayoonyesha kuwa na mapenzi mema na watanzania tangu uongozi wake wa kuwa mbunge Karatu hadi sasa. Wengi mnakumbuka kuwa amepata ulemavu wa mkono pamoja na vipigo katika harakati za kutaka kuwakomboa watanzania kutoka ktk mikono ya wakoloni weusi yaani CCM. Watu wenye misismamo kama Dr. Slaa huwa wanakuwa wachache sana katika Dunia hii, binafsi kwa mtazamo wangu nianaona tulihitaji sana mtu kama yeye ambaye anaweza kusema jambo na kusilisimamia kwa kadri anavyoamii kwa maslai ya wengi. Hivi tujiulize yaliyotokea Dodoma mwaka huu ya kukatwa kwa majina ya wagombea Lowassa ndiyo anayaona leo hayo? la pili kama alikuwa anakubaliana na sera za chama cha Chadema kwa nini hakuamua mapema kabla ya jina lake kukatwa? Hivi ni kwa nini hataki kueleza kwa kinagaubaga juu ya Richmond na mengineyo ya umiliki wa Jengo la ubalozi huko Afraka ya kusini? Nini kilimzuia asielezee kwa uwazi katika miaka ile 2008 juu ya mambo yote yaliyokuwa yanaelekekezwa kwake? Binafsi napata shida juu ya siasa za Tanzania na vyama hivi vya Tanzania kama wale wanaoongoza wana dhamira ya kweli kuwakomboa watanzania au wanahitaji kuingia katika Dora kwa kusudi la kujinufaisha wenyewe. Tuendeleee kuliombea taifa letu ili pasiwe na jambo lolote la kuharibu umoja wetu na utulivu tulionao ndani ya Nchi yetu.
 
ANGALIZO KWA DR SLAA NA LOWASA
Kabla sijaanza kuelezea lolote napenda kumukumbusha Slaa ambaye ana taalum ya upadri.
Katika kitabu cha matendo ya Mitume kuna ushahidi kwa Sauli alikuwa muuaji na tena alikuwa anauwa mitume lakini alipata padiliko la kweli na kujiunga na mitume wengine.

Wakati Sauli anafanya hivyo Mitume wengine walianza kumunyanyapaa na kumuogopa lakini katika bibilia , imethibitishwa kwamba hadi leo Paulo (aliyekuwa Sauli) ndiye aliyefanya kazi kuliko Mitume wote.

Bila shaka kuna watu ndani ya Chadema na hata nje ya chadema wanataka kujenga hoja ya kumunyanyapa LOWASA ati ni Fisadi , hata mimi niliingia mtego huu lakini napenda kuhojhi yafuatayo:
(1)Lowasa amehama CCM na kwa hatua hiyo ameingamiza nafsi yake kwa kiwango Kikubwa.
(2)Lowasa yupo tayari kutumia Pesa yake na mali yake kubomoa CCM
(3)LOWASA anahasira kali na CCM na miungu watu ndani ya CCM
(4)LOWASA kama waziri Mkuu mstafu ametake risk ya Kifo kiasi kwamba anataka kupiga CCM kwa Nyaraka zito za Siri ambazo Slaa hawezi kuzielezea
(5) Lowasa anajua mikakati ya Wizi wa Kura ndani ya CCM kwa miakazaidi ya 40
(6) Ndani ya CCM hawakutarajia wala hawakuwahi kupanga kuwa mtu kama Lowasa ambaye amewshijka nafasi nyeti kama waziri mkuu anaweza kuasi serikali kiasi hiki
Huu uasi unatisha na haujawahi kutokea, na hata pale ulipojaribu kutokea wahusika hawakubaki hai
(7)Kwa sasa CCM wanahaha sana juu ya Lowasa kuchukua form. Mikakati ya CCM iliielekeza Nguvu kumshambulia Slaa lakini Mungu amebadili Plan ghafla na kumuleta Lowasa amabaye hawajajipanga nan i Pigo kubwa
(8)Kwa sasa Uasi uliojitokeza CCM ni vigumu kujua nani yupo kwa nani
Angalia mtandao wa Lowasa ndani ya CCM unatisha na umetulia Kimia.
Mtandao huu jumlisha nguvu ya Umma ni lazima CCM ibaki kama KANU
MAONI KWA SLAA.
(1)Wakati unagombea urais ulikuwa na Rozi Kamili ukamwacha na kumuoa Josephine
Rozi Kamili alikubali ujio wa Josephine lakini leo Josephine huyo amekuwa kikwazo kwa maamuzi yako.
(2)Mambo ya Chama huwezi kumuhusisha Mwanamke, huo ni udhaifu mkubwa na kama kweli unamsikiliza mwanamke basi ujue hutapata nafsi ya kurudi kwenye jamii na wakakuamini na kukupa heshima kama walivyokupa.
Mke ni mshauri wake kwa mambo yote lakini kikao kama kamati kuu kinapopitisha maamuzi harafu mkeo anapinga maana yake mke huyo hafai kuwa First Lady na hata wewe hufai kuwa Kiongozi
MAONI KWA LOWASA
(1)Umeitwa Mwizi kwa siku nyingi sana na hata mimi nimekuita hivyo , sasa huu ni wakati wa wewe kutuambia mwizi halisi ni nani na utoe Ushahidi
(2) Zipo taarifa kwamba CCM wanapanga kukata jina lako kwenyenye tume ya uchaguzi hivyo nakusihii usikate tama .Muombe Mungu .Hii ni safari ya ushindi na si matumaini tena
(3)Usiogope kushambulia Ikulu kwa kuwa Mussa alikaa Ikulu ya Farao na kulelewa hapo lakini Mungu alimupa kazi ya kumuangamiza Farao.
Hivyo Lowasa umepewa kazi ya Kuingamiza CCM hivyo fanya kweli ujue kwamba Slaa hajui haya.

Nimekubali bandiko lako cobra
 
Ni dhahiri kuwa maamuzi ya mtu hutegemea na mtazamo alionao na hisia juu ya jambo analotaka kulifanyia maamuzi. Kimsingi Dr. Slaa ni mtu mwenye hisia za ndani na dhamiri inayoonyesha kuwa na mapenzi mema na watanzania tangu uongozi wake wa kuwa mbunge Karatu hadi sasa. Wengi mnakumbuka kuwa amepata ulemavu wa mkono pamoja na vipigo katika harakati za kutaka kuwakomboa watanzania kutoka ktk mikono ya wakoloni weusi yaani CCM. Watu wenye misismamo kama Dr. Slaa huwa wanakuwa wachache sana katika Dunia hii, binafsi kwa mtazamo wangu nianaona tulihitaji sana mtu kama yeye ambaye anaweza kusema jambo na kusilisimamia kwa kadri anavyoamii kwa maslai ya wengi. Hivi tujiulize yaliyotokea Dodoma mwaka huu ya kukatwa kwa majina ya wagombea Lowassa ndiyo anayaona leo hayo? la pili kama alikuwa anakubaliana na sera za chama cha Chadema kwa nini hakuamua mapema kabla ya jina lake kukatwa? Hivi ni kwa nini hataki kueleza kwa kinagaubaga juu ya Richmond na mengineyo ya umiliki wa Jengo la ubalozi huko Afraka ya kusini? Nini kilimzuia asielezee kwa uwazi katika miaka ile 2008 juu ya mambo yote yaliyokuwa yanaelekekezwa kwake? Binafsi napata shida juu ya siasa za Tanzania na vyama hivi vya Tanzania kama wale wanaoongoza wana dhamira ya kweli kuwakomboa watanzania au wanahitaji kuingia katika Dora kwa kusudi la kujinufaisha wenyewe. Tuendeleee kuliombea taifa letu ili pasiwe na jambo lolote la kuharibu umoja wetu na utulivu tulionao ndani ya Nchi yetu.

kwahiyo aliposema maelekezo toka ngazi ya juu hukumwelewa au? wee endelea kutuelewa mpaka nchi ichukuliwe ndo tutakuelewesha!
 
Taarifa niliyoisikia kutoka kwa Mwenyekiti wa CHADEMA kuwa wameridhia Katibu Mkuu wetu Dr Slaa, kupumzika kwa mda usio julikana.

Kiukweli nimeumizwa na kusikitishwa kwa uamuzi huo wa Dr Slaa hasa nikikumbuka taabu na mateso aliyoyapata katika kukikuza na kukisimamia leo anaamua kuacha kwa namna alivyo amua kufanya.

Naomba nitumie fursa hii kumuomba Mh😀r Slaa fikiri mara nne ni maumivu makali kiasi gani utakuwa umeyasababisha kwa watanzania wenzako na hasa tunao kuunga mkono na kutambua umuhimu wako na mchango wako ndani ya chama cha CHADEMA na UKAWA kwa ujumla tafadhari nakuomba rejea kambini kwa masilahi ya chama na Taifa.

Wafuasi wa Lowassa wameondoka naye kutoka CCM hadi CHADEMA, vivyo hivyo kama nawe ni mfuasi wa Dr. Slaa toka hapo alipotoka mfuate huko alikoenda.
 
Back
Top Bottom