Nimetokea mahabusu kumuona Lema leo

kwa inavyoelekea kesi imemkalia vibaya; sasa anatafuta kujihalalisha kisiasa kupitia ukabila, udini na eneo analotoka! Nafikiri siku zake za mwisho zimekaribia
 
Ujumbe wa Godbless Lema (Mbunge wa Arusha Mjini) kwa mke wake leo wakati alipomtembelea katika gereza la Kisongo Mkoani Arusha "BE STRONG, The purpose of life sio kisses (busu) na maisha mazuri. BE STRONG KAMA MKE WA MARTIN LUTHER CORETTA KING,Wanaonibeza wacha wanibeze lakini kukaa gerezani kuna maana kubwa sana kwangu." Nini maoni yako?

Source; Stephen Owawa facebook page
 
Asante sana kwa taarifa
Nimekumbuka siku nilipokuta na Magdalena Sakaya, anajiita yeye ni mama wa gerezani. Si mnakumbuka alivyosota gerezani kwa wiki kadhaa. Lema umeonyesha mfano mzuri
 
Shaka yangu kubwa sana ni kuwa ufikiri wa Lema ni mkubwa sana, sasa endapo kutakuwa na gap kubwa baina ya ufikiri wake na wananchi walio wengi wenye mtazamo wa kati na wasio washabiki hataeleweka na atakuwa na jukumu kubwa sana la kujieleza aeleweke.
 
Namuunga mkono mbunge Godbless Lema haya ndo mapambano tunayoyataka Tanzania.
 
Nimefungua vitabu vya history lukuki hasa vya Martin Luther King na Nelson Madiba Mandela sijaona sehemu ambayo wapambanaji hawa walikuwa wakikataa dhamana na kuamua kwenda jela (sehemu kubwa walikuwa wakinyimwa dhamana hali ya kuwa ni haki yao kimsingi).

Hii ya Lema kidogo inanipa shida, nadhani kuna umuhimu wa kupima kichwa yake hapa si bure.
 
kwa inavyoelekea kesi imemkalia vibaya; sasa anatafuta kujihalalisha kisiasa kupitia ukabila, udini na eneo analotoka! Nafikiri siku zake za mwisho zimekaribia
Lema ni waziri kivuli wa mambo ya ndani,nafasi inayotambuliwa na bunge.Lema ni boss wa hao mapolisi na magereza indirectly!! Kume kuwa na udhalilishaji wa wabunge wa upinzani makusudi na ccm wanakenua hawajui kesho wao!!! Kwa issue hii Lema anamaanisha!! Watu wanapuuzia vitu kama vile tumekuwa kisiwa siku kikiwaka hapa Tz watu wa kwanza kuwalaani ni wazee wengi wanaoheshimika kama akinaj salim ahmed salim kukaa kimya na kuona fahari wakiitwa nje kusuluhisha migogoro while kwake moshi unafuka! Hakuna wazee wanaoweza kuisema serikali na ccm moja kwa moja bila woga!
 
Shaka yangu kubwa sana ni kuwa ufikiri wa Lema ni mkubwa sana, sasa endapo kutakuwa na gap kubwa baina ya ufikiri wake na wananchi walio wengi wenye mtazamo wa kati na wasio washabiki hataeleweka na atakuwa na jukumu kubwa sana la kujieleza aeleweke.

Mkuu mageuzi huletwa na wacheche wenye uthubutu............ asiyalielewa hilo akae pembeni asubiri matokeo....
 
Nimefungua vitabu vya history lukuki hasa vya Martin Luther King na Nelson Madiba Mandela sijaona sehemu ambayo wapambanaji hawa walikuwa wakikataa dhamana na kuamua kwenda jela (sehemu kubwa walikuwa wakinyimwa dhamana hali ya kuwa ni haki yao kimsingi).

Hii ya Lema kidogo inanipa shida, nadhani kuna umuhimu wa kupima kichwa yake hapa si bure.
Ndugu soma waraka wa Lema uelewe ujumbe anaoufikisha.Mandela na Luther wanatajwa kwa kufananisha baadhi ya vitu usipindishe maana.
 
Jamani tusidanganyane kwa kufarijiana katika Nchi hii.Sikubaliani na maamuzi ya Lema kimsingi kwani hakuna anachofundisha zaidi ya kuwafanya waharifu waendelee kuwa waharifu kwa maana ya kuhisi kuonewa.

Wananchi wanahitaji kiongozi wa kuwahamasisha katika maendeleo.Hawana shida ya kutafuta haki kwani wana uhuru wa kufanya yote watakayo ilimradi wasivunje sheria.Uhuru wa kiuchumi,kijamii na kisiasa vyote vinapatikana Tanzania tofauti na nchi nyingine kama Uganda na Libya tuliyofananisha na nchi yetu.Kamwe tusikufuru na kubakia watu wakulalamika tu pasipo kufanya kazi.

Tazama, nimeona vijana wakiwa katika hali isiyoridhisha kwa maana ya kutokuwa nadhifa hapa ITV wakinyoosha vidole viwili kwa maana ya kumuunga mkono Lema.Maisha haya yatadumu mpaka lini, vijana hawa mbali na kutokuwa na kazi,wakipata kazi watafanya kazi kweli?.Nasema uhuru wa kisiasa tunao,ndio maana tunazunguka nchi nzima na kumtukana Rais pasipo hofu.

Tunahitaji ukombozi wa kifikra hasa kufikiri kujishughulisha badala ya kuhisi kuonewa kila wakati.Tukiendelea na hali hii, hata ije serikali gani bado tutaikosoa na kuendeleza usaliti hatimaye kugharimu maisha yetu.

Obama kasifiwa na kupewa ushindi, lakini leo anabezwa na hata kutishiwa kutorudi tena ''white house''.Ubinadamu kazi.
 
Nimetokea magereza kuu ya mkoa wa Arusha, Kisongo ambako nilikwenda na mke wa Lema na watoto wake. Watoto wake wawili Allbless na Brilliant hawakuruhusiwa kumuona baba yao na wamelia kwa uchungu mkubwa sana wakati askari magereza walipowazuia.

Lema yupo Imara na still msimamo wake uko palepale. Ameona na azidi kujifunza mengi, amewakuta watu wengi wanaolalama kwa kubambikiziwa kesi, amewakuta maskini kibao ambao wamefungwa kwa sababu ya kushindwa kulipa faini ya pesa kidogo na ameomba watu wenye nia njema wachange fedha kuwasaidia watu hao waondoke magereza.

Amewakuta wafungwa wanawaKe wakikosa huduma muhimu kama vitambaa vya kike yaani pedi na hali ni mbaya sana.

Wakati tunaondoka alimwambie mke wake "BE STRONG, The purpose of life sio kisses na maisha mazuri. BE STRONG KAMA MKE WA MARTIN LUTHER CORETTA KING"

Wanaonibeza wacha wanibeze lakini kukaa gerezani kuna maana kubwa sana kwangu.

Nawasilisha.

Hivi alifanya nini huyu mwizi mstaafu wa magari????ok anywayz vyovyote iwavyo pole kwa mama Lema na wanae,namimi namuongezea nukuu hii kutoka kwa mwanaharakati kijana machachari rais wa ANC youth league ya south africa bwana Julius Malema ambae hupenda kusema hivi

""This is a war. In a war, never expect red roses, and in a war there are casualties. But we can guarantee that we will win,".

Kesho ni siku ya kuwaona mahabusu katika gereza la kisongo arusha. Wananchi wa arusha na maeneo ya jirani wamepanga kujitokeza kwa wingi mahabusu kumwona mh. Lema saa tatu asubuhi.
 
Jamani tusidanganyane kwa kufarijiana katika Nchi hii.Sikubaliani na maamuzi ya Lema kimsingi kwani hakuna anachofundisha zaidi ya kuwafanya waharifu waendelee kuwa waharifu kwa maana ya kuhisi kuonewa.

Wananchi wanahitaji kiongozi wa kuwahamasisha katika maendele.Hawana shida ya kutafuta haki kwani wana uhuru wa kufanya yote watakayo ilimradi wasivunje sheria.Uhuru wa kiuchumi,kijamii na kisiasa vyote vinapatikana Tanzania tofauti na nchi nyingine kama Uganda na Libya tuliyofananisha na nchi yetu.Kamwe tusikufuru na kubakia watu wakulalamika tu pasipo kufanya kazi.

Tazama, nimeona vijana wakiwa katika hali isiyoridhisha kwa maana ya kutokuwa nadhifa hapa ITV wakinyoosha vidole viwili kwa maana ya kumuunga mkono Lema.Maisha haya yatadumu mpaka lini, vijana hawa mbali na kutokuwa na kazi,wakipata kazi watafanya kazi kweli?.Nasema uhuru wa kisiasa tunao,ndio maana tunazunguka nchi nzima na kumtukana Rais pasipo hofu.

Tunahitaji ukombozi wa kifikra hasa kufikiri kujishughulisha badala ya kuhisi kuonewa kila wakati.Tukiendelea na hali hii, hata ije serikali gani bado tutaikosoa na kuendeleza usaliti hatimaye kugharimu maisha yetu.

Obama kasifiwa na kupewa ushindi, lakini leo anabezwa na hata kutishiwa kutorudi tena ''white house''.Ubinadamu kazi.
Hujui usemalo!! Anza kuwahamasisha ndugu zako kule kijijini kwenu ambako pengine ukienda unawaonea kinyaa! Vijana wanajiajiri hakuna umeme miaka 50 ya uhuru! Unajua Arusha mgao unaendaje? Unajua mfumko wa bei sasa sukari inauzwa bei gani? Unga kilo 1800 maskini wataweza vp? Alafu kwa dharau mnawaita panya!! Wewe huna dhiki ila jamaa zako wanataabika anza kuwahamasisha hao utoe mfano.
 
Aluta continua,mapambano ndo kwanza yanashika kasi,Mh. Lema lengo na nia yako kuelekea ukombozi wa nchi hii ni kubwa kuliko thamani ya kukaa gerezani,hakuna wa kuwasemea wanyonge walioko huko,hii ndo nafasi adimu ,umeonyesha uzalendo mkubwa kwa wananchi wanyonge wanaonyanyaswa ndani ya nchi inayojiita ya amani.Amani hii ya kusemea mdomoni mwisho wake nini.Na hakika una nyumba nzuri mh,Lema ila dhamira ya kweli ndo imekupeleka huko.Mungu akupe afya tele sisi wadanganyika katika nchi hii tupo nyuma yako wakati tuna subiri harakati hizo za ukombozi toka miongoni mwa tabaka la wanyonyaji weusi.

by sammosses
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom