MKOA WA KINONDONI KANDA MAALUM YA DAR ES SALAAM
Tamko la katibu wa mkoa wa Kinondoni Kanda Maalum ya Dar es salaam
Ndugu zangu wanahabari
Nimewaita hapa leo kwa lengo la kuwapa watanzania msimamamo wangu na
wa chama ngazi ya mkoa kuhusu tukio la kukamatwa na kupelekwa magereza
kwa Mhe. Godbless Lema Mbunge wa jimbo la Arusha Mjini.
Imekuwa ikizoeleka kwa muda mrefu sasa kwamba waheshimiwa wabunge wa
CHADEMA na wale wanaaotokana na vyama vya upinzani wamekuwa
wakinyanyaswa sana kwa lengo la kuwafanya wajute kuingia katika siasa
za upinzani Tanzania.
Hii kwa CHADEMA haitokei tu kwa waheshimiwa wabunge bali hata kwa
viongozi wa ngazi zote. Inaonekana kuwa sasa serikali ya Chama Cha
Mapinduzi imeamua kutekeleza kwa vitendo mkakati wa kuwatesa kwa siri
na kwa wazi wale wote wanaoipinga siasa kandamizi na zisizowalazimisha
watawala kuwajibika kwa wananchi.
Mkakati huu umetungwa na CCM, unasimamiwa na usalama wa taifa na
unatekelezwa na jeshi la polisi. Kwa hakika hatuhoji tena kwamba jeshi
la polisi ni kitengo cha kusimamia maamuzi na maelekezo ya CCM badala
ya kulinda raia na mali zao.
Mheshimiwa Godbless kama mbunge wa wananchi wa jimbo la Arusha Mjini
amekuwa akifuatwafuatwa na jeshi la polisi kila mara na kufanyiwa
vitendo vingi vya udhalilishaji na unyanyasaji hasa kwa kupitia OCD wa
Arusha Mjini Zuberi.
Mathalani wiki iliyopita siku ya ijumaa tarehe 28/10/2011 Mhe.
Godbless lema akitoka mahakamani alisindikizwa na wananchi wake kutoka
mahakamani hadi ofisini kwake. Wafuasi wake walipomfikisha ofisini
waliondoka na kurejea makwao. Huko ofisini aliwakuta wananchi
wakimsubiri ili awahudumie kama mbunge wajimbo lao. Wakati akiongea na
wananchi ghafla polisi walifika na kuwakamata wananchi wote waliokuja
kuomba usikivu wa mbunge na kuwapeleka kituo kikuu cha polisi.
Mbunge Lema alipokwenda kituo cha polisi kwa lengo la kuwawekea
dhamana naye aliwekwa chini ya ulinzi kwamba eti amefanya maandamano
bila kibali.
Tunahoji: Ni maandamano yapi hayo ambayo Lema aliyafanya na wananchi
wake akiwa angali ofisini kwake? Je maandamano wanayoyazungumzia ni
kuondoka na wananchi mahakamani hadi ofisini kwake? Je kama kuondoka
kwake na wafuasi wake mahakamani ni kosa kisheria; Je kwa Mhe Ole
Sendeka alipokuwa akitoka mahakamani, alikuwa akiondoka na kundi kubwa
la wafuasi wake na kusindikizwa na OCD huyu huyu? Vile vile Mwenyekiti
wa UV-CCM mkoa wa Arusha amekuwa akienda kituo kikuu cha polisi
akisidikizwa na kundi kubwa la wafuasi wake wa CCM. Polisi hawakuwahi
kuwakamata wala kuwaonya. Sasa haya yote yalikuwa maandamano ama
matembezi ya hisani? Maana Arusha kuna msiba mkubwa wa CCM kukataliwa
na wananchi.
Kwa hakika tukio la kukamatwa kwa Mhe Lema, kupelekwa mahakamani na
hatima ye kupelekwa gerezani ni ushahidi wa kutosha kwamba jeshi la
polisi sasa linakamilisha sehemu kubwa wa wajibu wake wa kuibaka
demokrasia.
Hata hivyo tunalitaka jeshi la polisi na serikali ya CCM wajue kwamba
kitendo cha kumpeleka Lema magereza ni ushindi tosha katika harakati
za ukombozi wa taifa hili. Maana hakuna silaha yoyote duniani ama
jeshi la polisi popote pale duniani ambavyo viliweza kushinda vita
dhidi ya ukweli, haki na uwazi.
Ndugu zangu watanzania
Tunawaunga mkono wana Arusha kwa kumpata mbunge ambaye anayatetea
maslahi yao kwa mzigo hata pale inapobidi kwenda gerezani kwa ajili ya
watu wake na hata ikibidi kifo anaweza kusimamia hilo. Alisema Martin
Luther King Jr. 1963 A man who wont die for something is not fit to
live na akaendelea kusisitiza Nobody can give you freedom, nobody
can give you justice or right or anything. You take it! (STAND UP;
STAND UP 4, UR RIGHT) Hayo yalikuwa maono ya bob marley ambayo
aliyaona mwaka wa 1973,baada ya kuwa amekaa katika mto mmoja huko
jamaica akaona samaki wanapita katika maji lakini samaki wakubwa
wakawa wanawaonea samaki wadogo,hivyo akaona hata hapa duniani hata
wa2 walio juu wanawaonea watu wa hali ya chini.
Kwa watu wanaopinga ama kukejeli maamuzi ya Godbless lema kukataa
dhamana, Wathubutu kufanya ziara huko Mahospitalini wavae sura za
uhasilia wa kibinadamu wakaone watu waliokuwa kama wao jinsi
wanavyotaabika kwa kukosa matibabu ile hali ni walipa kodi wa taifa
hili. Kwanini Godbless asiende jela wakati anasimamia mambo ya msingi
na hayatekelezwi, tukiandamana tunaonekana tunavunja sheria ni
afadhali kwenda sehemu wanayodhani tunaogopa kuliko kukaa kimya kumbe
hatuogopi. Mungu yupo upande wetu na tunaelekea kushinda unyanyaswaji
huu.
Kama ambavyo alivyowahi kusema Martin Luther king jr, ndivyo tunavyo
wahakikishia wana wa Arusha, we will work together; we will stand up
together, we will go to jail together, until justice runs down like
water. maana mateso tunayoyapata ni makubwa kuliko huko jehanam
tusipopajua.
Kwa kuonyesha tuko pamoja katika harakati hizi za kudai demokrasia ya
kweli tunampogeza Godbless lema mbunge wa Arusha mjini kwa kupeleka
ujumbe kwa watawala wanaodhani wanaweza kutumia magereza kama sehemu
ya vitisho kurudisha harakati zozote zile nyuma.
Ujumbe huu uwafikie watawala yakuwa jela sisehemu ya kumtishia mtu
yeyote Yule mwenye akili timamu, mpenda haki bali ni sehemu ya kawaida
ambapo binadamu yeyote Yule anaweza kwenda.
ASANTENI ASANTENI NA MUNGU AWABARIKI WATANZANIA WENZANGU