Jamani tusidanganyane kwa kufarijiana katika Nchi hii.Sikubaliani na maamuzi ya Lema kimsingi kwani hakuna anachofundisha zaidi ya kuwafanya waharifu waendelee kuwa waharifu kwa maana ya kuhisi kuonewa.
Wananchi wanahitaji kiongozi wa kuwahamasisha katika maendeleo.Hawana shida ya kutafuta haki kwani wana uhuru wa kufanya yote watakayo ilimradi wasivunje sheria.Uhuru wa kiuchumi,kijamii na kisiasa vyote vinapatikana Tanzania tofauti na nchi nyingine kama Uganda na Libya tuliyofananisha na nchi yetu.Kamwe tusikufuru na kubakia watu wakulalamika tu pasipo kufanya kazi.
Tazama, nimeona vijana wakiwa katika hali isiyoridhisha kwa maana ya kutokuwa nadhifa hapa ITV wakinyoosha vidole viwili kwa maana ya kumuunga mkono Lema.Maisha haya yatadumu mpaka lini, vijana hawa mbali na kutokuwa na kazi,wakipata kazi watafanya kazi kweli?.Nasema uhuru wa kisiasa tunao,ndio maana tunazunguka nchi nzima na kumtukana Rais pasipo hofu.
Tunahitaji ukombozi wa kifikra hasa kufikiri kujishughulisha badala ya kuhisi kuonewa kila wakati.Tukiendelea na hali hii, hata ije serikali gani bado tutaikosoa na kuendeleza usaliti hatimaye kugharimu maisha yetu.
Obama kasifiwa na kupewa ushindi, lakini leo anabezwa na hata kutishiwa kutorudi tena ''white house''.Ubinadamu kazi.