Mhe. Godbless Lema alichana Jeshi la Polisi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mhe. Godbless Lema alichana Jeshi la Polisi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pascal Mayalla, Jul 28, 2011.

 1. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #1
  Jul 28, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,565
  Likes Received: 18,307
  Trophy Points: 280
  Mbunge wa Arusha, ambaye pia ni Waziri Kivuli wa Mambo ya Ndani, Mhe. Godbless Lema analichana Jeshi la Polisi!.

  Mhe. Lema, anatoa shutuma mbalimbali kwa jeshi hilo, wakati akiwasilisha maoni ya kambi ya upinzani kwenye bajeti ya Mambo ya Ndani.

  Amelishutumu Jeshi la Polisi kuhusu serikali kutumia mabavu. Naibu Spika amezuia paragraph fulani isisomwe, Lema akalazimisha kutaka kuisoma kwa kutetea kuwa yeye kama Waziri Kivuli wa Upinzani, asitegemee yuko hapo kuitetea serikali.

  Huku akinukuu wapiginia haki maarufu duniani akiwemo Martin Luther King Jnr kuwa 'Amani sio kuweko kwa utulivu, bali kutendwa kwa haki", hivyo Tanzania sio nchi ya amani kwa vile haina haki!

  Amelaani mauji yanayofanywa na polisi kama ukwiukwaji mkuu wa haki za binaadamu.

  Uchanaji huo wa jeshi la polisi unaofanywa na Mhe. Lema, unafanywa huku Mkuu wa Jeshi la Polisi, Inspecta Jenerali wa Polisi, Said Mwema na makamanda wake wakuu wakiwa wote wako bungeni.

  Uptate kwa hisani ya Edson.
   
 2. Edward Teller

  Edward Teller JF-Expert Member

  #2
  Jul 28, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,818
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Naibu spika amlazimisha lema aruke page moja-na asiisome
  Lema akamjibu kuwa hawezi kiitetea serikali
   
 3. Mosachaoghoko

  Mosachaoghoko Senior Member

  #3
  Jul 28, 2011
  Joined: Apr 19, 2011
  Messages: 137
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naibu speaker analazimisha kuondoa kifungu cha madhira yanayofanya na serikali why by the way yeye anatakiwa asikilize hoja zitajibiwa na waziri husika
   
 4. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #4
  Jul 28, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Endelea kutujuza Mkuu tumekatiwa umeme
   
 5. muwaha

  muwaha JF-Expert Member

  #5
  Jul 28, 2011
  Joined: May 13, 2009
  Messages: 743
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tunaomba page iliyotakiwa kurukwa iwekwe hapa jamvini
   
 6. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #6
  Jul 28, 2011
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 9,002
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  teh teh teh! uwooo! wana wabanwa ni mbwai. sasa huyo naibu spika anataka kifungu kirukwe kwa maslahi ya nani?
   
 7. K

  Kiluvya2011 JF-Expert Member

  #7
  Jul 28, 2011
  Joined: Feb 18, 2011
  Messages: 215
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Dah naibu spika kaamuru lema aruke paragraph moja...lema aligoma kukawa na majibishano kidogo, lema amwambia naibu spika hayupo kusoma ripoti kuitetea serikali so kasema hiyo paragraph iingie kwenye hansadi....

  Leo ngoja tuone mwisho wake.
   
 8. Mpatanishi

  Mpatanishi JF-Expert Member

  #8
  Jul 28, 2011
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 1,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  haaah haaah watakoma mwaka huu. Big up Lema
   
 9. K

  Kiluvya2011 JF-Expert Member

  #9
  Jul 28, 2011
  Joined: Feb 18, 2011
  Messages: 215
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wapigiania haki tunaombeni hiyo page iliyorukwa kwa manufaa yetu wanyonge
   
 10. K

  Kiluvya2011 JF-Expert Member

  #10
  Jul 28, 2011
  Joined: Feb 18, 2011
  Messages: 215
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Anachana mbaya, anasema risasi za polisi wasiozidi elfu hamsini haziwezi kumaliza watizd zaidi ya milioni arobaini...
   
 11. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #11
  Jul 28, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,565
  Likes Received: 18,307
  Trophy Points: 280
  Hotuba ya Mhe. Lema, anaendelea kutoa hotuba yake, ilijaa vitisho kuwa amani ya nchi hii haiwezi kulindwa kwa udhalimu wa jeshi la polisi na FFU wake.

  Amedai kuwa Wananchi wameanza kuzoea vitisho vya polisi, na muda sii mrefu, wanaweza kuwa tayari kufanya lolote, bila kuogopa risasi za polisi, na kutolea mfano, nguvu ya umma kwenye maandamano yaliyotokea nchi mbalimbali mbali mbali barani Afrika na kusema maandamano hayo sasa yako jirani kwetu nchini Malawi, hivyo ametoa onyo kuwa lolote linaweza kutokea Tanzania!.
   
 12. RUMANYIKA

  RUMANYIKA JF-Expert Member

  #12
  Jul 28, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 315
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Lema kwa kweli ni jembe. Anachana vibaya serikal legelege. Bonge la hotuba sijawai sikia.
   
 13. M

  Mwanaume Senior Member

  #13
  Jul 28, 2011
  Joined: Oct 11, 2009
  Messages: 122
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  kazi ya spika ni kuzuia hoja kwenye mijadala au kuongoza mijadala? Mbona watu hawa wanakuwa waoga wa hoja zinazopaswa kujibiwa na serikali.?
   
 14. Kishongo

  Kishongo JF-Expert Member

  #14
  Jul 28, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hana jipya! anamwaga pumba tupu. Ni aibu kwa wapiga kura wake na kwa mji wa Arusha.
   
 15. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #15
  Jul 28, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Swafi saaaana hawa ndo wanatufanya tujione Wa Tanzania lkn hiyo mibunge mingine hovyoooooo kabisa
   
 16. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #16
  Jul 28, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Wamezowea kufichiana madhambi hawa!
  CCM bila uwongo na kufukiafukia mambo haiwezi kudumu hata kwa nusu saa!
   
 17. mgt software

  mgt software JF-Expert Member

  #17
  Jul 28, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 10,719
  Likes Received: 1,628
  Trophy Points: 280
  anaogopa kufichua siri za maruhani wakiwemo, hasa za kudhoofisha upinzani, madawa ya kulevya na kubambikiwa kesi
   
 18. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #18
  Jul 28, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Unajifunza kutumia keyboard au??
   
 19. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #19
  Jul 28, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,565
  Likes Received: 18,307
  Trophy Points: 280
  Nadhani hiyo paragraph ama ilikuwa na maneno ambayo ni uhaini, Naibu Spika alipoliona hili, akaamua kupindisha kanuni kwa kuzuia jinai isitendeke ndani ya bunge.

  Tutafuatilia kama kanuni zinaruhusu, naamini baada ya hotuba hii tuu, utafuatia ombi la muongozo wa spika, toka kwa chief whip, Tundu Lissu, kumuuliza Naibu Spika ametumia kanuni gani.
   
 20. Edward Teller

  Edward Teller JF-Expert Member

  #20
  Jul 28, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,818
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  wewe una matatizo ya akili-
   
Loading...