Nimetapeliwa zaidi ya Tsh. 45,000,000 kwa kuuziwa kiwanja feki

Nitafutie mbuzi weusi watatu, ng’ombe mmoja awe wa kisasa jike wa maziwa awe amezaa mara moja ndio dawa itashika, kuku wawili mmoja jogoo na jike, nitafutie na mchele wa kyela ndoo mbili kubwa ili kutoa kafara kwa wazee, na vitenge vitatu was original vya kufunikia dawa halafu hela usinipe yoyote ukifanikiwa utarudi kushukuru.
Haa ha ha ha, hi ndio tunaitaga, "MGANGA HAOMBAGI TEMBELE"
 
haya mambo yasikie tu.

Nina siku ya nne leo tangu nigundue kwamba nimepigwa, hata kula vizuri siwezi, nawaonea wivu wenzangu walionunua maeneo madogo kwa bei za 15m kushuka chini. Naona hasara yao ni ndogo kuliko yangu.
Upo humu jf kama member halafu unatapiliwa kirahisi hivyo?? kwanini hukuuliza kuepukana na hilo kuuliza sio ujinga ni kupata maarifa fulani fulani, , pili kuna uzi uliozungumzia sana namna ya kupata kiwanja halali pasipo kutapeliwa njia za kutumia kukwepa mitego
 
Kwa hiyo mkataba wa mauziano, ofisi ya mtaa na mashahidi hawatambuliki kabisa, anayetambulika atakuwa nani sasa?
Mkuu kwenye sheria ya ardhi, hao hawatambuliki kabisa kwenye kuuziana , labda kama ni ardhi ya kijiji.
Anayetambulika ni hakimu, na mawakili tu, ndio wanaoweza kusimamia mauziano hayo na yakawa na nguvu ya kisheria.zile hati za serikali za mtaa ni makaratasi tu, ambayo kisheria hayana nguvu kabisa.Ukiwa nalo hilo halafu akaja mtu akauziwa hicho kiwanja chako tena na akawa na hati ya mauziano yaliyosimamiwa na wakili, huwezi kushinda hiyo kesi kwa kuonyesha hizo karatasi.
 
Point muhimu Bexb, zungumzia viwanja vya vyenye migogoro ya kifamilia.
Nime'edit kidogo, pitia tena. Ila mkuu hata kama kiwanja umekipenda vipi, endapo tu ukasikia kuwa kuna mgogoro wa kifamilia USINUNUE narudia tena USINUNUE kwani wewe mnunuzi utakua kwenye upande mgumu zaidi
 
Watu wanatapeliwa huku wakiwa na hati original toka wizarani, sembuse hivyo vipeperushi vya ofisi ya mtendaji!!kwa taarifa yako kisheria kwenye mauziano ya ardhi hakuna sehemu iwe, mwenyekiti, ama mtendaji anatambulika kuwa atayasimamia.
Huwa nashangaa sana, yaani unakuta eti jamaa msomi kabisa yupo busy eti tumeuziana na shahidi ni mwenyekiti wa serikali ya mtaa😂😂😂😂😂 kinachoniuma zaidi hao wenyeviti wanakula 10% ya mauzo ghafi dah! Huwa natamani kuwatia hata makofi wanunuzi wa namna hiyo.
 
Mkuu kwenye sheria ya ardhi, hao hawatambuliki kabisa kwenye kuuziana , labda kama ni ardhi ya kijiji.
Anayetambulika ni hakimu, na mawakili tu, ndio wanaoweza kusimamia mauziano hayo na yakawa na nguvu ya kisheria.zile hati za serikali za mtaa ni makaratasi tu, ambayo kisheria hayana nguvu kabisa.Ukiwa nalo hilo halafu akaja mtu akauziwa hicho kiwanja chako tena na akawa na hati ya mauziano yaliyosimamiwa na wakili, huwezi kushinda hiyo kesi kwa kuonyesha hizo karatasi.
Asante sana mkuu kwa kuendelea kuwafumbua macho. Utakuta kiwanja kinauzwa 50M, mwenyekiti anapewa eti 5M ya kusimamia mauzo halafu ukishauri akamwone wakili anasema wakili gharama wakati wangeweza hata kumomba kumlipa hata 3M na kuepusha hasara inayoweza kutokea mbeleni
 
Ni rahisi sana mkuu hili suala ukimshirikisha wakili atakuongoza vizuri Sanaa na utapunguza chances za kuingia kwenye hasara. Mfano umeambiwa hii nyumba ni ya familia na mimi ndiye kiongozi wa familia, simple tu unamwambia mimi nawataka wanafamilia wote wawepo. Wakati huo unapita hata kwa majirani wawili watatu kuuliza kuhusu idadi ya wanafamilia, uzuri sisi watanzania tutakunyima mchongo wa hela lakini sio umbea😂😂😂😂😂
Wakati mwingine hujui kama kuna mgogoro wa kifamilia. Ukiongeza hicho kipengele kitawasaidia wengi.n
 
haya mambo yasikie tu.

Nina siku ya nne leo tangu nigundue kwamba nimepigwa, hata kula vizuri siwezi, nawaonea wivu wenzangu walionunua maeneo madogo kwa bei za 15m kushuka chini. Naona hasara yao ni ndogo kuliko yangu.
Unatapeliwaje 45m mkuu? Kwani hukujiridhisha kabla ya kuitoa?
 
Ni rahisi sana mkuu hili suala ukimshirikisha wakili atakuongoza vizuri Sanaa na utapunguza chances za kuingia kwenye hasara. Mfano umeambiwa hii nyumba ni ya familia na mimi ndiye kiongozi wa familia, simple tu unamwambia mimi nawataka wanafamilia wote wawepo. Wakati huo unapita hata kwa majirani wawili watatu kuuliza kuhusu idadi ya wanafamilia, uzuri sisi watanzania tutakunyima mchongo wa hela lakini sio umbea😂😂😂😂😂

Muhimu kwa faida ya wengi, kujua jinsi ya kuchukua tahadhari mbalimbali.
 
Ninaamini kabisa kuwa utapeli upo lakini kuna namna huwa watu tunaweza kuchukua tahadhari na kupunguza visa vya kutapeliwa.
KWA VIWANJA VILIVYOPIMWA:
Baada ya kuwa umeoneshwa kiwanja husika na mmekubaliana bei, hakikisha kuwa unampa wakili kazi ya kusimamia mauzo hayo maana ni lazma atafanya search katika mamlaka husika kujua mmiliki halali ama kama kuna attachment yoyote juu ya kiwanja husika
Hakikisha unajua marital status ya muuza kiwanja, kama atakwambia wameachana hakikisha anakuonesha hati ya talaka ama ya kutengana iliyotolewa na MAHAKAMA na sio vinginevyo.
Endapo ametengana kienyeji na mwenza wake hakikisha huyo mwenza anajaza fomu maalumu (spousal consent) ya kuridhia mauzo ya kiwanja husika yaani hata kama wamenuniana hakikisha mwenza amejaza hiyo form yeye mwenyewe.
Kama kutakua na wasiwasi wowote wa vipimo vya kiwanja husika vile vya kwenye nyaraka na uhalisia hakikisha mnaitumia mamlaka ya ardhi eneo husika kisha kuwakutanisha na majirani wako ili kuweka sawa suala hilo.

KWA VIWANJA/MAENEO AMBAYO HAYAJAPIMWA:
Hakikisha kuwa unawapata watu wote wa pande zote ambazo eneo hilo mnapakana na wakuoneshe na mkubaliane wote mipaka halisi ya eneo unalotaka kununua na hawa ndio watakua mashuhuda wa mjataba wako.
Hakikisha mauziano hayo yanasimamiwa na wakili ambaye atakuongiza katika kufanya search na taratibu sahihi.
Hakikisha mwenza wa anayekuuzia eneo husika anajaza form maalumu ya kuridhia mauzo hayo na kama wameachana hakikisha unapata nyaraka ya mahakama kuthibitisha hili.

KWA MAENEO YA UKOO/FAMILIA/URITHI.
Hapa ndio kuna kivumbi na wanunuzi hupoteza sana pesa hapa.
Kuna wakati ambapo mzazi/mmiliki wa eneo akifariki basi familia haifungui mirathi mahakamani bali hukaa kikao na kuamua kutoaiuza ardhi lakini wakagawanya vyumba ama hisa katika nyumba husika mfano, huweza kugawana vyumba hivyo kila mmoja akawa na mpangaji wake ama wakaipangisha kisha kila kodi ikitolewa basi wanagawana.
Sasa endapo unataka kununua ardhi ya mazingira ya namna hii unatakiwa kuwa makini sanaaa na endapo nyumba ni ya familia hakikisha kuwa wale wanafamilia woooote yaani namaanisha WOTE sio wengi hapana, nasema WANAFAMILIA WOTE wahaohusika na ardhi ama nyumba husika ndipo muweze kuendelea na mauzo. Hii ni kwa sababu endapo ikatokea mmoja ama sehemu ya wanahisa wa hiyo ardhi ya familia hakuridhia basi utakua umepigwaaa(rejea kilichomkuta S. H. Amon hapo Kariakoo)
Iwapo nyumba inamilikiwa na Ukoo yaani vizazi hata viwili ama vitatu yaani nyumba alikua anamiliki babu yangu ambaye alikua na watoto nane na wote hao walikua na familia, wakafariki 4 na watoto wa babu wakazaa tukatokea sisi na baadhi yetu tumeshafariki lakini tumeacha watoto wetu ambao wana haki kupitia baba na babu zao aisee mimi NINAKUSHAURU USINUNUE ARDHI HIYO hakikisha kabla ya kununua au kulipia hata sh mia unawasiliana na wakili wako.

Kiukweli wakuu ukitapeliwa kwenye kiwanja kilichopimwa ni lazma wewe mnunuzi kuna mahali ulizembea kwenye utaratibu mzima wa manunuzi maana kwa upande wa hivi viwanja vilivyopimwa utaratibu upo wazi sana.
Nilichogundua ni kuwa wengi wana mazoea na kukalili taratibu za kizamani zisizotambuliwa kisheria yaani mtu anaona kutoa 2M kwa wakili asimamie mchakato mzima wa mauziano ya 50M anamuamini dalali ambaye atalipwa 10% na mtedaji/mwenyekiti halafu anatoa hela

HAKIKISHENI MNAFUATA MIONGOZO YA WANASHERIA KUPUNGUZA KUTAPELIWA
Mkuu vipi kama ...nimeuziwa kiwanja cha familia na mwanamke ambaye mume wake ameishafariki na waliosaini ni watoto 2 kati ya wanne na mama yao (huyo mwanamke),mwenyekiti na katibu wao pia....hapo kuna hitilafu....???
 
kuna siku nilisema humu ukitaka kununua kiwanja au shamba jitahidi kuuliza majirani zako watarajiwa kuhusu hicho kitu.
Pili usiwe mvivu kwenda wizara ya ardhi kujiridhisha kuhusu hicho kiwanja Cha Nani na anamiliki Nani.
Nani usifanye malipo bila kuwa na WAKILI
Nakazia...

Hata Serikali za Mitaa siku hizi nao ni wale wale tu...
Wanachojali ni ile asilimia yao.. likikupata janga huko unapambana mwenyewe..
 
Nakazia...

Hata Serikali za Mitaa siku hizi nao ni wale wale tu...
Wanachojali ni ile asilimia yao.. likikupata janga huko unapambana mwenyewe..
Mkuu sio kwamba serikali ya mtaa hawakusaidii ila HAWANA MAMLAKA WALA UWEZO WOWOTE WA KUKUSAIDIA KWA LOLOTE KISHERIA. Labda iwe hiyo ni ardhi ya kijiji, ila kama ni ardhi binafsi aisee hao ni sawa na hakuna. Wakili ama hakimu ndio maafisa pekee wanaoruhusiwa kusimamia mikataba ya mauziano ya ardhi.
 
Mkuu vipi kama ...nimeuziwa kiwanja cha familia na mwanamke ambaye mume wake ameishafariki na waliosaini ni watoto 2 kati ya wanne na mama yao (huyo mwanamke),mwenyekiti na katibu wao pia....hapo kuna hitilafu....???
Mkuu kila situation huwa inaamuliwa kwa namna yake. Katika sheria ya mikataba Tanzania kuna kitu kinaitwa 'voidable contract ' hii ni aina ya mkataba ambao ni halali hadi pale mmoja wa pande za mkataba atakapogundua tatizo na kutoendelea na mkataba, ila akiamua kuendelea nao kunakua hakuna tatizo kisheria.

Sasa kwa wewe sijui kama msimamizi wa mirathi ya marehemu baba mwenye nyumba ni nani na kama kiwanja kilikua cha urithi, na kama kila upande wa urithi umepata mgao wake. Nadhani tukipata maelezo ya kutosha tunaweza kuwa na chochote cha kutoa maoni.
 
Haya mambo yasikie tu.

Nina siku ya nne leo tangu nigundue kwamba nimepigwa, hata kula vizuri siwezi, nawaonea wivu wenzangu walionunua maeneo madogo kwa bei za 15m kushuka chini. Naona hasara yao ni ndogo kuliko yangu.
Kama ni siyo maeneo yaliyopimwa basi hukufikiri kabla ya kutenda. 45ml nunua surveyed area.
 
Back
Top Bottom