Nimetapeliwa zaidi ya Tsh. 45,000,000 kwa kuuziwa kiwanja feki

Haya mambo yasikie tu.

Nina siku ya nne leo tangu nigundue kwamba nimepigwa, hata kula vizuri siwezi, nawaonea wivu wenzangu walionunua maeneo madogo kwa bei za 15m kushuka chini. Naona hasara yao ni ndogo kuliko yangu.
Fafanua kidogo
Kilikuwa kwenye gunia kama mbuzi au documents feki?
 
Unachanganya kati ya title deed na offer letter. Offer letters ndio zinaweza kutoka zaidi ya mbili. Wanaolewa haya mambo wanalifahamu hili
Tumekusoma mkuu! Wengine wana mahaba Tu kila kitu mwendazake! Wangejua ni marais wote wanafanya kutengua title deeds! Ni mchakato wa kawaida ingawa huwa ni wa muda mrefu!
Hata mwendazake hizo kesi kazikuta zote zina muda mrefu!
 
Hilo jiulize wewe, ilikuwaje watu wengi wakajikuta, kwenye kiwanja kimoja kina hati mbili, tena zote zimetolewa na wizara ya ardhi?hadi rais kuamua kuingilia kati kuwa yule aliyepata hati kwanza ndio mwenye kiwanja?na ndio hilo tatizo lilikuwa solved kwa style hiyo.
Mimi naweza kuchallenge Kwa hoja hiyo ya GN na Newspaper na nikashinda, nakuhakikishia
 
Naomba maelezo mkuu,,, nataka kununua kiwanja hapa Dar, ktk haya makampuni yanayojinadi kuwa mteje ana ruhusa ya kulipia kidogo kidogo, na alimaliza anapewa hati... NAOMBA MAELEZO NAMI NISIJE NIKAPIGWA

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
wakuu bado niko kwenye mapambano makali ya kupata haki yangu nikitulia nitatoa mrejesho
 
Wakuu nimetapeliwa na hali bado tete nahisi hili jambo linaweza kuchukua mda mrefu na huku nikiendelea kutumia gharama zingine
 
Ninaamini kabisa kuwa utapeli upo lakini kuna namna huwa watu tunaweza kuchukua tahadhari na kupunguza visa vya kutapeliwa.
KWA VIWANJA VILIVYOPIMWA:
🔥Baada ya kuwa umeoneshwa kiwanja husika na mmekubaliana bei, hakikisha kuwa unampa wakili kazi ya kusimamia mauzo hayo maana ni lazma atafanya search katika mamlaka husika kujua mmiliki halali ama kama kuna attachment yoyote juu ya kiwanja husika
🔥 Hakikisha unajua marital status ya muuza kiwanja, kama atakwambia wameachana hakikisha anakuonesha hati ya talaka ama ya kutengana iliyotolewa na MAHAKAMA na sio vinginevyo.
🔥 Endapo ametengana kienyeji na mwenza wake hakikisha huyo mwenza anajaza fomu maalumu (spousal consent) ya kuridhia mauzo ya kiwanja husika yaani hata kama wamenuniana hakikisha mwenza amejaza hiyo form yeye mwenyewe.
🔥 Kama kutakua na wasiwasi wowote wa vipimo vya kiwanja husika vile vya kwenye nyaraka na uhalisia hakikisha mnaitumia mamlaka ya ardhi eneo husika kisha kuwakutanisha na majirani wako ili kuweka sawa suala hilo.

KWA VIWANJA/MAENEO AMBAYO HAYAJAPIMWA:
🔥Hakikisha kuwa unawapata watu wote wa pande zote ambazo eneo hilo mnapakana na wakuoneshe na mkubaliane wote mipaka halisi ya eneo unalotaka kununua na hawa ndio watakua mashuhuda wa mjataba wako.
🔥Hakikisha mauziano hayo yanasimamiwa na wakili ambaye atakuongiza katika kufanya search na taratibu sahihi.
🔥Hakikisha mwenza wa anayekuuzia eneo husika anajaza form maalumu ya kuridhia mauzo hayo na kama wameachana hakikisha unapata nyaraka ya mahakama kuthibitisha hili.

KWA MAENEO YA UKOO/FAMILIA/URITHI.
Hapa ndio kuna kivumbi na wanunuzi hupoteza sana pesa hapa.
Kuna wakati ambapo mzazi/mmiliki wa eneo akifariki basi familia haifungui mirathi mahakamani bali hukaa kikao na kuamua kutoaiuza ardhi lakini wakagawanya vyumba ama hisa katika nyumba husika mfano, huweza kugawana vyumba hivyo kila mmoja akawa na mpangaji wake ama wakaipangisha kisha kila kodi ikitolewa basi wanagawana.
Sasa endapo unataka kununua ardhi ya mazingira ya namna hii unatakiwa kuwa makini sanaaa na endapo nyumba ni ya familia hakikisha kuwa wale wanafamilia woooote yaani namaanisha WOTE sio wengi hapana, nasema WANAFAMILIA WOTE wahaohusika na ardhi ama nyumba husika ndipo muweze kuendelea na mauzo. Hii ni kwa sababu endapo ikatokea mmoja ama sehemu ya wanahisa wa hiyo ardhi ya familia hakuridhia basi utakua umepigwaaa(rejea kilichomkuta S. H. Amon hapo Kariakoo)
Iwapo nyumba inamilikiwa na Ukoo yaani vizazi hata viwili ama vitatu yaani nyumba alikua anamiliki babu yangu ambaye alikua na watoto nane na wote hao walikua na familia, wakafariki 4 na watoto wa babu wakazaa tukatokea sisi na baadhi yetu tumeshafariki lakini tumeacha watoto wetu ambao wana haki kupitia baba na babu zao aisee mimi NINAKUSHAURU USINUNUE ARDHI HIYO hakikisha kabla ya kununua au kulipia hata sh mia unawasiliana na wakili wako.


Kiukweli wakuu ukitapeliwa kwenye kiwanja kilichopimwa ni lazma wewe mnunuzi kuna mahali ulizembea kwenye utaratibu mzima wa manunuzi maana kwa upande wa hivi viwanja vilivyopimwa utaratibu upo wazi sana.
Nilichogundua ni kuwa wengi wana mazoea na kukalili taratibu za kizamani zisizotambuliwa kisheria yaani mtu anaona kutoa 2M kwa wakili asimamie mchakato mzima wa mauziano ya 50M anamuamini dalali ambaye atalipwa 10% na mtedaji/mwenyekiti halafu anatoa hela😂😂😂😂😂😂

HAKIKISHENI MNAFUATA MIONGOZO YA WANASHERIA KUPUNGUZA KUTAPELIWA
Habari wakuu, hii post inazidi kusaidia wengi japo kuna watu wamenibeza kuwa natafuta wateja. Ila hadi sasa nina feedbacks kadhaa DM watu wamesaidika na kuepusha kutapeliwa ama kuingia kwenye migogoro ya ardhi mbeleni. Kama bado hujanunua ardhi pitia hapo na umshirikishe mwenzako umpendae.
 
Wakuu nimetapeliwa na hali bado tete nahisi hili jambo linaweza kuchukua mda mrefu na huku nikiendelea kutumia gharama zingine
Ipo hivyo mkuu, hiyo ndivyo haki hupatikana. Kama umewabananisha komaa nao tu maana unajua mwisho wa siku utapata chako hata kama utakua umeingiza hasara kidogo
 
KIWANJA KINAUZWA KIBAHA PANGANI
________________

Maelezo ya ardhi: Matumizi yoyote
_____________________
Kiwanja No: 70
_____________________
Mahali: Kibaha Pangani Mbele kidogo ya Stendi ya Mabasi Loliondo na ni kilomita 3 kutoka barabara ya Morogoro road, Kibaha Pangani, Dar es salaam. Tanzania
_____________________
Ukubwa wa Kiwanja: mita za mraba 698 SQM
_____________________
Bei: Tsh 9,500,000 (Inaweza Jadiliwa)
_____________________
Kwa maelezo zaidi Wasiliana nami kupitia:
Namba ya simu: 0626090873
0652251374 (WhatsApp)
Barua pepe: ismaildasilva92@gmail.com
IMG_20220515_184423_661.jpg
 
Nashukuru ndugu zangu nimepambana nimeweza kurudishiwa viwanja vingine vya thamani ya tsh 32m, nimeshauriwa kuliko kuwafunga nikose thamani ya pesa iliyobaki ni bora niingie nao makubaliano kisheria ili waweze kunilipa hiyo 13m iliyobaki ambapo tumefanya hivo chini ya dhamana ya watu wao wa karibu walio na mali zisizohamishika ambazo wameweka bond
 
Back
Top Bottom