mgt software
JF-Expert Member
- Nov 1, 2010
- 13,793
- 7,165
Babuyao, pole sana!! Lakini wakati mwingine ni mipango ya kukuandaa kupata pesa nyingi zaidi!! kwa hiyo usisikitike sana. We chukulia tu kuwa hiyo pesa umeichange kwa exchange rate ya chini sana.
Mambo ya mazingaombwe yapo kama hayajakutokea wewe shukuru Mungu. Afadhali huyo ametapeliwa pesa ndogo. Mimi nilitapeliwa Dollar 2,100 nikajikuta nina 270,000 tu.
welcome bongo darisalama
Yani watu wanatafuta pesa kwa juhudi kumbe bado kuna mijinga inakwenda kutupa pesa kwa watu wa Filmeee!!?? hiyo ndio inaitwa Wash kaka.
Unbelievable! hii lazima umetunga tu, no way, absolutely impossible.
Yaani leo, Machi 2013, uibiwe kiZOMBIE namna hiyo? no way.
Kama ni kweli basi AMKA!.
Asante sana. Mimi ni mbulula.Nini bwana ... ''machingaombwe'' ''machingaombwe''. Ni umbulula wako tu ndio unakufanya uone kama yalikuwa ni mazingaombwe. Na UNA HAKI KABISA ya kuyaita mazingaombwe au uchawi kwani hujui kilichotendeka. Lakini mimi nakuhakikishia kabisa sio!
Nilivyomwelewa jamaa hakubisha au haamini kama hao watu wana exist. Yeye haamini kama kuna mtu anaweza kutapeliwa kimbulula namna hii miaka hii, kwani huo utapeli ni siku nyingi sana...
Nini? bahati mbaya? Unapelekwa kwenye ngazi wakati umeacha maduka chungu nzima halafu unasema bahati mbaya?
Sasa ambush ya kiakili ndo nini kama si mazingaombwe? Au hypnosis?Bi mkora amini nakuambia hakuna kiini macho wala kiini masikio. Ni kupelekwa chaka tu. Hii kwa kifupi tunaweza kusema wanakupiga ''ambush'' ya ki-akili. Kabla huja-recover wanakuwa wameshafanya damage.
Asante sana. Mimi ni mbulula.
Wewe ndo tapeli wangu. Unaudhi sana kwa majibu yako.
Sasa ambush ya kiakili ndo nini kama si mazingaombwe? Au hypnosis?
Hapana. Ambush ya akili ni pale mtu anapokuingia kwenye angle ambayo usingetegemea. Mkuu Babuyao kama hii michezo ya mazingaumbwe kuna mingi ikionyeshwa Tanzania watu wengi wataamini na kusema ni uchawi kumbe ni ujanja tu. Hebu jaribu kuangalia kwenye bwana mmoja anaitwa Pauli daniel akifanya Pauli Daniel magic show. Kama hujui ujanja anautumia wewe utabaki kinywa wazi na usiku hutalala kwani utafikiria umekutana na jini. Kumbe ni ujanja tu. Baada ya hapo jaribu kuangalia ''Magic's Biggest Secrets Finally Revealed'' ambapo wanaonyesha ujanja unaotumika hapo utagundua mengi.