Nimetapeliwa jamani

Babuyao hebu check tena huo mfuko wa pembeni, inawezekana umejichanganya.
 
Babuyao, pole sana!! Lakini wakati mwingine ni mipango ya kukuandaa kupata pesa nyingi zaidi!! kwa hiyo usisikitike sana. We chukulia tu kuwa hiyo pesa umeichange kwa exchange rate ya chini sana.

Hahahahaha! umenichekesha aisee na ushauri wako kiboko eti chukulia umiechange kwa exchange rate ya chini sana!
 
Mambo ya mazingaombwe yapo kama hayajakutokea wewe shukuru Mungu. Afadhali huyo ametapeliwa pesa ndogo. Mimi nilitapeliwa Dollar 2,100 nikajikuta nina 270,000 tu.
 


pole sana ndugu.. ni bora umesema hapa nawengine tuchukue tahadhari


jamani tusipende njia zisizo kubalika . tujenge tabia ya kupata huduma kutoka sehemu zilizo rasmi. hakuna sababu ya kuchukuliwa na mtu eti utapata bei nzuri. kama unataka kwenda dukani kupata huduma pata huduma dukani. siyo nje ya duka mtu anakuuliza unataka nini unasema nataka kununua saa , halafu unaambiwa mimi nina saa nauza..... hiini hatari si kwa pesa yako tu bali pia kwa usalama wako
 
Pole sana ndugu yangu, mimi pia ni mhanga wa utapeli hapa bongo kwa hiyo naweza kuwa miongoni mwa wale walio kuelewa barabara.
 
Asamte kwa ushauri. Ukweli pes hiyo wala sijaitumia kwani inanipa kichefuchefu.

Kama kipato chako ni kikubwa ni bora ukaipereka kwenye vituo vya yatima, umeshajiuliza kwa nn pesa zilipotea kimiujiza??
 
Jenga tabia ya kutokukubali kuingia kwenye mazungumzo na mtu au watu usiowafahamu. Hii ni kanuni yangu niliyojiwekea.
 
Yani watu wanatafuta pesa kwa juhudi kumbe bado kuna mijinga inakwenda kutupa pesa kwa watu wa Filmeee!!?? hiyo ndio inaitwa Wash kaka.
 
karibu mjini and always kupenda urahisi vina gharama zake na hiyo ndo gharama yenyewe
 
Babuyao, pole sana!! Lakini wakati mwingine ni mipango ya kukuandaa kupata pesa nyingi zaidi!! kwa hiyo usisikitike sana. We chukulia tu kuwa hiyo pesa umeichange kwa exchange rate ya chini sana.

Mkuu hata kama ni kumfariji mwenzio si kwa mtindo huu! Kutoka laki 2 na elfu 22 hadi elfu 50 wewe unaiita hii exchange rate ya chini? Naona hapo ulitaka kutufurahisha tu!! Haina neno lakini manake pole yako ameipata!!
 
Mkuu pole sana ndiyo Dunia ilivyo.Ujumbe wako ni somo kwa wengine,ingawa kuna watu wanafikiri haiwezi kuwatokea.

Kabisa. Mimi haiwezi kunitokea katika mazingira kama hayo. Yaani maduka ya kubadilisha yalivyojaa halafu mtu anibadilishie fedha kwenye ngazi?
 
Pole sana mkuu, when the deal is too good think twice
 

Nini bwana ... ''machingaombwe'' ''machingaombwe''. Ni umbulula wako tu ndio unakufanya uone kama yalikuwa ni mazingaombwe. Na UNA HAKI KABISA ya kuyaita mazingaombwe au uchawi kwani hujui kilichotendeka. Lakini mimi nakuhakikishia kabisa sio!
 
Mambo ya mazingaombwe yapo kama hayajakutokea wewe shukuru Mungu. Afadhali huyo ametapeliwa pesa ndogo. Mimi nilitapeliwa Dollar 2,100 nikajikuta nina 270,000 tu.

Hayo utamkikishia na kumwaminisha mtu/watu wako huko kijiweni. Si hapa kwenye forum ambako kuna watu wenye exposure na elimu za kila aina.
 

Nilivyomwelewa jamaa hakubisha au haamini kama hao watu wana exist. Yeye haamini kama kuna mtu anaweza kutapeliwa kimbulula namna hii miaka hii, kwani huo utapeli ni siku nyingi sana...
 
Nilivyomwelewa jamaa hakubisha au haamini kama hao watu wana exist. Yeye haamini kama kuna mtu anaweza kutapeliwa kimbulula namna hii miaka hii, kwani huo utapeli ni siku nyingi sana...

Hao watu nahisi wanatumia kiini macho, ni kama wale ambao walikuwa Mlimani City, anajidai nataka kwenda mahali sasa sipajui naomba unipeleke nina madini naenda kuuza, upuuzi mtupu, ukiwasikiliza tu umekwisha. Na hao ni hivyo hivyo ukiwapa muda wa kuongea nao tu tayari.
 
jamani sio kikondoo kwani sote tupo kwa ajili ya faida na si vinginevyo, hiyo ni bahati mbaya kwani nikatika utafutaji2.

Nini? bahati mbaya? Unapelekwa kwenye ngazi wakati umeacha maduka chungu nzima halafu unasema bahati mbaya?
 

Bi mkora amini nakuambia hakuna kiini macho wala kiini masikio. Ni kupelekwa chaka tu. Hii kwa kifupi tunaweza kusema wanakupiga ''ambush'' ya ki-akili. Kabla huja-recover wanakuwa wameshafanya damage.
 
Kuna jamaa yangu alikuwa ananiambia kuwa hawezi kununua kitu ambacho hakupanga kununua tokea akiwa nyumbani hata kiwe kizuri namna gani anakwambia sikupanga kununua hicho kitu kumbe alikuwa wa maana. Wewe umetoka nyumbani kwenda dukani kubadili fedha iweje ukabadili fedha kwenye ngazi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…