Nimeshindwa kuvumilia!!

Unajua siyo wote wenye akili timamu na ubinadamu pia;wengine ni vichaa na wanyama wakali.Kwa hao waliofanya haya matukio ni kwamba,hamnazo kichwani;yaani hata kichwa cha kuku kina kitu cha kujivunia.
 
sisi wenyewe tumeyataka hayo kwa kuzidharau njia za Bwana.

1. kufanya mapenzi kinyume na maumbile hata wanyama wenyewe hawajawahi kujaribu, angalia sisi tunavyoshabikia!
2. kutumia midomo, mikono/vidole, mafuta, sabuni, madawa ya kemikali kama viagra nk katika kuanya mapenzi tunaona sawa tu na tunashangilia! jana alilalalmika kijana wa watu kuwa kashindwa kutumia mdomo/ulimi kufanyia mapenzi na matokeo yake alinyimwa unyumba na mkewe wa ndoa, alichekwa hapa na kuitwa mshamba!
3. mabikira mnawazomea na kuwaona wapumbavu kujinyima ngono hadi wafikie ndoa
4. kutoa mimba siku hizi ni kama kutumbua chunusi, tunawaona hao waliowaunguza wanao lakini wakazibakisha roho zao hai kuwa waovu kuliko wale wanaotoa mimba na kuangamiza roho hai zisizo na hatia
5. neno la Mungu hamtaki kusikia, mnataka njia za mkato za mambo ya rohoni
6. na maasi mengine mengi tunayoyajua na tusiyoyajua.

niambieni ni mnyama gani hufanya hayp yote niliyotaja. sasa hayo ni symptoms tu lakini maradhi ya mwanadamu yamo moyoni na wengi wetu tunaolaani hapa tunaugua tena wengine wako hatua mbaya zaidi ya hao wazazi

Neema ya Mungu yatutosha!

wapendwa tumtumaini Bwana pekee kwa mioyo yetu yote,
tena tumkiri Yeye katika njia zetu kwa maana ameahidi kuwa hatatupungukia,
kwa jinsi ileile alivyokuwa na Musa, atakuwa pia pamoja nasi
i
 
Matendo ya wanadamu siku hizi yanatisha kwani hata shetani anashangaa unyama wa binadamu
 
.......mzazi kumfanyia mwanao ukatili kama huu jamaniiiiiiiiii!!Mtoto anavyouma jamani, upo wapi upendo wa mzazi kwa mtoto? Mimi huwa sitaki hata mwanangu alie, yaani akilia tu nasikia tumbo lote linauma.

Kwa developed countries mzazi kama huyu kwanza anawekwa jela na watoto wanachukuliwa na serikali hawaoni tena watoto wake.
 
Tatizo ni kwamba unapohachika ujue kuwa mume ndiye mwenye haki ya kukaa na mtoto kisheria (ya Jamhuri ya Tanzania) sasa kama mwanao ni over 7, na baba yake ndo hataki uondoke nae , utafanyaje? Wengi wanahacha watoto si kwa kupenda ni sheria zinazotunyanyasa wanawake. Nadhani hapo inaonyesha ni jinsi gani divorce should be the last resort. Ndo maana wazazi wetu walivumilia mengi, ukiwauliza ni nini unang'ang'ania kwa baba? anakwambia watoto. Otherwise tuanzishe movement za kubadili sheria hizi kandamizi

Ndo maana hata siku moja siwezi kumwacha mtoto wangu alelewe na mwanamke anaeitwa mama wa kambo.Bora nilale nae njaa kuliko kumuacha kwenye nyumba yenye chakula bila uwepo wangu.
 
Watoto ni taifa la kesho, tuwapende kama tulivyoagizwa na Mungu
 
Miss Judith,
Umeongeza ufafanuzi, ni vema kabisa. Tatizo la wazazi hao ni moyoni (Hawana hofu ya Mungu na labda wamefanya hivyo kutekeleza ushirikina. Pia wanapinga kwa uwazi kabisa uumbaji na uthamani wa watoto hao katika jamii ), akilini (ni wajinga na wasiojua wajibu wao sio tu kama wazazi bali pia kama wanajamii) na pia kimtazamo (kwao chakula na materials ni muhimu kuliko utu na pia wanaendeshwa na tamaa yenye mkono wa shetani moja kwa moja). Solution ni: Yaanzishwe mashirika ya uma yanayojengea uwezo watoto kama hao waliotelekezwa na wazazi/jamii, ili watoto hao wasiendelee kuchukia kwa nini walizaliwa na pili wazazi waliohusika wapelekwe jela kufundishwa tabia.
 
Wanawake mjirekebishe kwa ukatili wenu kwani nyie ndio chanzo cha michafuko yote duniani toka enzi za tunda la kati
 
Hii inaonyesha kuwa kuna watu na viatu, hao wazazi sio watu ni viatu tu! Inaumiza sana moyo!
 
watoto wa tanzania wengi wao wanateseka sana.
matukio kama haya ni mengi sema asilimia kubwa hayafiki ktk vyombo vya habari.
kuna yule mtoto alivutwa macho na mwalimu sikuweza kujizuia kulia,sikutaka kuitizama ile picha mara mbili.
sasa kama huyu mtu unashindwa kuelewa huruma zetu binadamu tumeziacha wapi.
tumekua wakatili sana,hakuna huruma kabisa kwa watoto.
 
kila kitu kinaanzia moyoni.

hao wazazi mngekutana nao siku moja kabla hawajafanya uovu wao mngeweza kutambua kuwa ni wakatili kiasi hicho? si wanafanana na sisi wote hapa kwa muonekano? na hata rohoni? waliyofanya ni kazi ya shetani, so keep distance with satan!

mnataka tuwe na huruma wakati moyoni tumeikataa kweli na tumeruhusu shetani atukanyagekanyage jinsi apendavyo na sisi kusema eti ndio mambo ya kisasa?

hakika haiwezekani. tumrudie Mungu, tumkatae shetani na mambo yake, tumtake sana Bwana pamoja nguvu zake na tutakuwa safi mioyo yetu

Mungu awabariki nyote

mtakeni Bwana pamoja nguvu zake
utafuteni uso wake Bwana Mungu siku zote
isifuni kweli na jinale takatifu
na ufurahi moyo wa hao wanaomtafuta Bwana
 
Hivi kama Tanzania kuna social services inayofuatilia maisha ya watoto haswa? Au mtu unapoweza ripoti?
 
Wamama wengine roho mbaya tu, anakutesa kwa vile mama yako alikuwa mke wa mumewe sasa yale mateso anayotoa anafikiri anampiga au kumkomoa huyo mke mwenzake
 
Hivi kama Tanzania kuna social services inayofuatilia maisha ya watoto haswa? Au mtu unapoweza ripoti?

ipo ndg yangu watu ni workshops tu na kulipana per diem. child protection zipo wizara ya mambo ya ndani na wizara ya maendeleo ya jamii jinsia na watoto. Nilishakutana nao lakin hakuna wanachofanya.
 
jamani sio step ma wote tuna tabia hizo jamani, wengine tunakaa na watoto wa wanaume zetu kama wetu vile sema baadhi wanatuharibia jina kwa matendo wanayoyafanya...pole sana mtoto kweli kuna v2 unajiuliza kama ni binadamu esp mwanamke anavifanya anaejua uchungu wa mtoto ulivyo unabaki na mashangao.....
 
Back
Top Bottom