Nimeshindwa kuvumilia!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nimeshindwa kuvumilia!!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Susy, Mar 31, 2011.

 1. Susy

  Susy JF-Expert Member

  #1
  Mar 31, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 1,450
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Nawapenda nyote, na ninawasalimu pia!!!

  katika soma soma ya habari wapendwa kuna habari na picha nimekutana nazo zimenitoa machozi, nimesikitika sana, na nimeumia sana, sijui wewe mwenzangu ndio maana nimeamua tuone pamoja!!

  chakusikitisha zaidi wameunguzwa na wazazi wao wenyewe!, wala si wazazi wa kambo bali wa kuwazaa kabisaa tena huyo mmoja ndio kamketisha mwanawe kwenye jiko la mkaa kama sufuria ya maharage.

  unaamua kumchoma mwanao eti kwa sababu kala ubwabwa bila idhini yako je hii ni haki??

  ukatili huu kwa watoto utaisha lini jamani!! Mapenzi kwa watoto wetu yakowapi??
   

  Attached Files:

 2. MkimbizwaMbio

  MkimbizwaMbio JF-Expert Member

  #2
  Mar 31, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Madhara ya mama wa kambo hayo. Wakina mama mkiachika msiwaache watoto kwa baba yao, hujui atamuoa nani.
   
 3. Susy

  Susy JF-Expert Member

  #3
  Mar 31, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 1,450
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  mmoja kachomwa mikono na mama yake mzazi kwakuwa alikula wali bila ruhusa ya mama yake, na mwingine ni baba yake mzazi hapo hakuna cha wakambo wala nini.
   
 4. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #4
  Mar 31, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Ndo maana hata siku moja siwezi kumwacha mtoto wangu alelewe na mwanamke anaeitwa mama wa kambo.Bora nilale nae njaa kuliko kumuacha kwenye nyumba yenye chakula bila uwepo wangu.
   
 5. sweetdada

  sweetdada JF-Expert Member

  #5
  Mar 31, 2011
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 540
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  maskiniii..binadamu tumekuwa na roho chachuu kuliko wanyama..looh
  sasa hapo tuseme alilazimishwa kuzaa au mapenzi hakuna au ni vipi
  mi sipati jibu na sidhani kama nitalipata
  baba/mama kumtenda mwanae wa kumzaa hivyoo,..looh
  tuendapo sio kabisa
  INASIKITISHA..MUNGU ATUEPUSHE
   
 6. Susy

  Susy JF-Expert Member

  #6
  Mar 31, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 1,450
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Lizy hao wamechomwa na wazazi wao wa damu kabisa.
   
 7. RR

  RR JF-Expert Member

  #7
  Mar 31, 2011
  Joined: Mar 17, 2007
  Messages: 6,720
  Likes Received: 206
  Trophy Points: 160
  Watu wanakua wazazi kabla hawajajua majukumu ya wazazi....
   
 8. B

  Buke Senior Member

  #8
  Mar 31, 2011
  Joined: Feb 15, 2011
  Messages: 105
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Binadamu tuna roho tofauti sana, ubwabwa tu huo! Ingekuwa pesa sabuni ya roho...!!!???
   
 9. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #9
  Mar 31, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Hapo ndo ujue sio kila mtu anafaa/takiwa kuwa mzazi!
   
 10. Susy

  Susy JF-Expert Member

  #10
  Mar 31, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 1,450
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  hilo ndio jibu dia!!
   
 11. Makindi N

  Makindi N JF-Expert Member

  #11
  Mar 31, 2011
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 1,068
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Kuna tatizo ukiangalia, hayo matatizo yanazidi sana hizi. There's a root cause that is not significantly addressed..... moja maisha yamekua magumu sana - budget inakua ngumu - inayozidisha ugumu wa maisha na hasira, msongo wa mawazo (stress), mbili, watu wamechoka / wamekata tamaa kwa sababu ya kwanza............. etc Mwisho wa siku something has to be done......... kumbuka wanaofanya hivyo vitendo ni wa hali ya chini - ambao ni wengi miongoni mwetu Tanzania........ na sioni dalili ya serikali kufanya mambo mazuri - meaning hivyo vitendo vitazidi kama jitahada za makusudi hazitachukuliwa..........
   
 12. Susy

  Susy JF-Expert Member

  #12
  Mar 31, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 1,450
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  inawezekana ikawa uchumi ndio reason kubwa, lkn kumbuka kunakipindi tanzania miaka ya 74 nasikia kulitokea njaa mpaka wazazi wakawa wanachemshia mawe watoto wao, je ingekuwa ndio leo kipindi hicho wazazi wangetupa watoto wao au ingekuwaje?? nafikiri hapa ni swala la upendo hakuna, au kuzaa bila kujitambua kuwa umeshafikia umri wa kuitwa baba au mama!!
   
 13. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #13
  Mar 31, 2011
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 160
  Nikisikia tu habari ya mtoto kateswa sijui kafanywaje naishiwa nguvu na siku yangu imeharibika kabisa
   
 14. MkimbizwaMbio

  MkimbizwaMbio JF-Expert Member

  #14
  Mar 31, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Soma vizuri hiyo heading. "....Ni baada ya kumfukuza mama mzazi na kumleta mwanaMKE mwengine"

   
 15. Susy

  Susy JF-Expert Member

  #15
  Mar 31, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 1,450
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Bwana da Dena hembu tuliza huo mtima wako!! haya ndio maisha lazima ya songe!! tuliza moyo mama!!
   
 16. Akthoo

  Akthoo JF-Expert Member

  #16
  Mar 31, 2011
  Joined: Nov 5, 2007
  Messages: 587
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 60
  Mtoto aadhibiwa kwa kuning'inizwa mtini

  MWANAFUNZI wa darasa la kwanza katika Shule ya Msingi Dukamba, amepewa adhabu ya kuning'inizwa mtini miguu juu kichwa chini, huku amefungwa miguu na mikono.
  Inadaiwa mtoto huyo mkazi wa kijiji na kata ya Kharumwa wilayani hapa, Dickson Mjarifu (8), alipewa adhabu hiyo kwa karibu wiki moja na mama yake wa kufikia, Dafroza Masilu (25) kwa kushirikiana na baba yake mzazi, Hezron Mjarifu (35) huku akionywa kuwa angesema angeuawa.
  Akisimulia kisa hicho mwanzoni mwa wiki hii katika mahojiano maalumu na gazeti hili, mwalimu wa darasa analosoma mwanafunzi huyo, Agnes Boniphace, alidai kuwa Alhamisi iliyopita asubuhi, wanafunzi wenzake walitoa taarifa shuleni kuhusu mateso aliyokuwa akipata mwenzao.
  Kwa mujibu wa Mwalimu Agnes, ambaye sasa anaishi na Dickson, wanafunzi hao walipokuwa wakipita njiani karibu na nyumba anayoishi mtoto huyo, Dickson aliwaita kuwaomba msaada.

  Mwalimu Agnes alidai kuwa wanafunzi hao waliposogea karibu na nyumba hiyo, walimkuta mwenzao amening'inia mtini huku akiomba wasaidie kumnasua kutoka katika mti huo.

  "Baada ya kuwaita, wenzake walikwenda na kumwona, wakakimbia hadi shuleni na kutoa taarifa kwa Mwalimu Mkuu, ambaye alituchukua sisi baadhi ya walimu na wanafunzi hao na kwenda kwenye eneo la tukio.

  "Tulimkuta Dickson ananing'inia huku amefungwa kamba mikono yote na miguu huku kichwa kikielekezwa chini mfano wa popo.

  "Tulipoona hali hiyo, ilitulazimu kutoa taarifa kwa uongozi wa Kijiji ambapo Ofisa Mtendaji wa Kijiji alifika na kushuhudia, tukamfungua akateremshwa na kwenda naye shuleni akatusimulia kila kitu, yakiwamo mateso ambayo amekuwa akifanyiwa na mama huyo wa kambo,'' alidai Mwalimu Agnes.

  Walipofika shuleni, walimvua mtoto huyo nguo na kushuhudia makovu sehemu mbalimbali za mwili na hasa mgongoni, makalioni na kifuani, huku akionesha alama za fimbo.

  Kutokana na hali ya makovu na alama za fimbo, uongozi wa Shule ulimwita mama huyo na kumhoji juu ya hali ya mtoto huyo.

  "Cha ajabu, mama alipofika na kuhojiwa, alisema anayehusika na kipigo cha mtoto huyo ni baba yake mzazi, Hezron Mjarifu, ambaye ni mkulima katika kijiji hicho.

  "Tuliamua kuwaita polisi ambao walimkamata mtuhumiwa na kumpeleka kituoni na kumpatia mtoto fomu namba tatu ya matibabu,'' alifafanua.

  Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya cha Kharumwa, Dk. Leonard Mugema, aliyempa matibabu mtoto huyo alisema baada ya uchunguzi wa kina, alibaini mambo mengi yaliyosababishwa na kipigo hicho.

  Dk. Mugema alisema walibaini majeraha ya ndani yaliyosababisha damu kuvilia mwilini.

  "Hali ya mtoto si nzuri ana makovu mwili mzima akikuvulia nguo kama una roho nyepesi unaweza kumkimbia bila kumpa matibabu ... lakini nashukuru manesi wangu wamejitahidi kumsafisha vidonda vizuri.

  "Tulitaka tumlaze, lakini yeye akaomba akae kwa mwalimu wake wa darasa ambaye amekuwa akimleta asubuhi na jioni hapa hospitalini kwa matibabu," alisema Dk. Mugema.
  Dk. Mugema aliongeza kuwa baada ya kumfanyia vipimo vya kina mtoto huyo, walibaini anakabiliwa pia na utapiamlo uliosababishwa na kukosa chakula mara kwa mara.
  Akizungumza na gazeti hili, Dickson alidai amekuwa akipigwa kwa mwezi na wiki tatu kila siku na mama yake alimwekea ‘dozi' ya kuchapwa viboko kila siku asubuhi na jioni.

  Alidai pia mara nyingi amekuwa akinyimwa chakula na kufanyishwa kazi nyingi na ngumu, ikiwa ni pamoja na kusomba maji kutoka kisimani na kwenda kusenya kuni porini.
  Mtoto huyo alibainisha kwamba alionywa na mama yake huyo kwamba endapo atatoa siri atamwua, hali iliyosababisha akae kimya siku zote hizo, hadi siku hiyo alipoomba msaada kwa wanafunzi wenzake.
  Alidai kuwa aliamua kuomba msaada, kwa kuwa mama huyo hakuwapo, kwani alikwenda shambani na kumwacha akining'inia mtini.
   
 17. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #17
  Mar 31, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  kwa kweli siku hizi kuna matukio mengine hata kuamini unapata shida. lo, masikini watoto hawa waliopendwa na Bwana Yesu hawapendwi na wazazi wao. iliandika siku zitakapoyoyoma upendo wa wengi utapoa.

  huu ni ushahidi mwingine kuwa shetani yuko kazini hata sasa.

  kwa kweli tunahitaji kinga ya Mungu

  hakuna aliyemuona Mungu wakati wowote
  la Mwana pekee atokaye katika kifua cha Baba,
  huyo ndiye aliyemfunua
   
 18. Elia

  Elia JF-Expert Member

  #18
  Mar 31, 2011
  Joined: Dec 30, 2009
  Messages: 3,442
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Susy, Tatizo ni Roho mbaya, makuzi ya utotoni, na kutomjua MUNGU.
   
 19. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #19
  Mar 31, 2011
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 722
  Trophy Points: 280
  mimi nilistuka tu lile tukio la Goms.....kuna wazaz nadhani hadi leo watot wao wako vituo vya kulelea yatima......yaani kuna wazaz waliona ni heri mtoto apotee......halafu ziku hiz susy nikwambie watu hawana utu na upend hawakwa watoto wao...ndio maana siku hizi unakuta mzazi wa kiume anatembe na binti yake na binti anafurahi tu.....

   
 20. Blaki Womani

  Blaki Womani JF-Expert Member

  #20
  Mar 31, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 8,463
  Likes Received: 3,724
  Trophy Points: 280
  Utu umekwisha umebaki unyama
  wamefanya unyama huu kwa watoto wa kuwazaa itakuwa vipi kwa wengine
  wanastahili adhabu kali kabisa hawafai kwa jamii

   
Loading...