Nimesanuka, Bila kutumia akili kwenye haya maisha...

Yofav

JF-Expert Member
Mar 12, 2021
3,956
6,887
Maskani na Chocho zote kila ukiongelea situations zako kuzitafutia tatuzi jibu la mwisho utasikia tu kasauti kanachomekea "Tafta hela" Kiufupi hizi Karatasi zenye harufu ni kama zinataka kututoa roho kabisa kama sio kutufanya walemavu, Ukipita maeneo ya masoko na sehemu zilizochanganya kila kichwa ukionacho kipo busy na maisha yake yaani kitaswira tu ya nje ni uhakika kwamba kila kichwa kinawaza shilingi.
Anyways twende chap kwenye point bana,

Haya maisha yamefika hatua yanahitaji sana akili kuyaishi maana mzani unaonesha Nguvu imezidi uzito kuliko akili ndo maana maisha yanazidi kuwa magumu so ili mzani ukae sawa basi yatupasa tupate watu wengi wenye kutumia akili kwenye mzani ili kufanya mzani ukae sawa na maisha yaweze kukaa level.

Haina haja ya kuishi kwa kukariri kwamba kila mmoja ni lazima achangie kuijaza dunia. Yes, namaanisha kwamba wengine tunaweza tukaishi tu kwa ku-enjoy matunda ya hii Dunia. Hapo najua wengi sasa mnajiuliza "Huyu jamaa vipi anamaanisha nini" Okay, Tulia ndo naelekea kwenye point sasa.

Ukichunguza watu tunazaa kwanini na tunawaza nini kwenye akili zetu utagundua ni kwamba tunawekeza, Somebody is tryin to invest in somebody so somebody will maybe help him on future na ndivyo ilivyo. Ubaya unakuja kwamba maisha ya sasa yamekuwa mafupi sana kulinganisha na zamani yaani mtu kufika 60yrs tu hoi na tena ni kwa bahati. Siri ipo kwenye aina ya maisha tunayoyaishi ya kukariri katika kufanya investment kwa watoto yaani kila mmoja anataka azae ili aje asaidiwe na watoto uzeeni na ukiangalia wanaume wengi hawaji kufaidika na hilo, Safari ya mwanaume ambae ndiye muanzilishi wake huisha kabla ya kufika lengo, Wanaofaidika na lengo hili la wanaume ni wanawake waliozaa nao.

Hivyo mimi kama Flames nimegundua hilo na sitokubali hilo linitokee, Nitapambana kuilinda afya yangu zaidi na kujiimarisha kiuchumi kwa kiasi fulani, Nitakuwa m'binafsi na mwenye kujipenda sana kwa kuwa naamini Uzeeni pia nitakula kwa mgongo wa watoto wa wenzangu ambao watakuwa wamekwisha kufariki na kuacha wake zao na watoto wao.

Nitaoa mwanamke mjane nami nitakuwa nikimpa company na kumfariji, Muda huo kila mmoja (mwanamke au mwanamke) humuhitaji zaidi mwenzake kwaajili ya kufarijiana na kusubiri kifo, Mwanamke atanipenda sana kwa kuwa tutakuwa tunaendana kimri na Mumewe marehemu na Kwa kuwa muda huo wanaume wa marika yetu tuu wachache maana wengi walikwisha fariki na wengi Wakimwa ila mimi nitakuwa shupavu zaidi, Watoto wa marehemu nitawageuza wangu na mimi nitakuwa Baba yao wa kambo kama jinsi Mama yao atakavyonitambulisha kwao na nisipingwe na yeyote.

Ahsanteni.
 
Kwahiyo mke wako kipindi hicho unamfariji mjane atakuwa kafa?
Au hutaoa kabisa ukisubiri uzeeni kurithi mjane?
 
aisee, ukizaa mtoto ukiwa na miaka 25 , maana yake hap utakuja kufaidi matunda ya mwanao miaka 25 ijayo ukiwa na miaka 50+


Ila wote tukiamua kuwa kama wewe Nani atakuja kukukea sasa ?!
 
aisee, ukizaa mtoto ukiwa na miaka 25 , maana yake hap utakuja kufaidi matunda ya mwanao miaka 25 ijayo ukiwa na miaka 50+


Ila wote tukiamua kuwa kama wewe Nani atakuja kukukea sasa ?!
hapana jamani mimi sitaki wote tuwe hivyo, ila hapo nazungumzia akili ninayotakakuja kuitumia
 
Wazo zuri. Litekeleze kwanza ndio utupe ushuhuda kama limeleta tija au la. Best I luck chalii
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom