MIXOLOGIST
JF-Expert Member
- Mar 1, 2016
- 12,695
- 31,498
Sikiliza akili kubwa kama ifuatavyo:
Dunia hii imejaa mitihani mingi sana yaani tangu unazaliwa mpaka unarudi six feet under;
Utakabiliana na mambo mengi, kwa kuchagua au kwa lazima;
Utapoteza wapendwa na wapenzi wako;
Utaumwa na kuugua maradhi yanayotibika na yasiyotibika;
Utashutumiwa na kusingiziwa mambo ambayo haujafanya;
Utapigwa fitina, majungu na pengine kuchukiwa bila sababu ya msingi;
Utavunjwa moyo na uwaaminio na pengine utakata tamaa kabisa; na
Wakati mwingine utakosa hela, utakosa marafiki na kukosa amani na kujutia maisha yako.
Lakini akili kubwa inakuambia, maisha lazima yaendelee, huo ndiyo uanadamu, na hauko peke yako wote tunapita kwenye njia hiyo. Simama piga moyo konde, yote yatapita. Endelea kuamini siku utakapo kosa changamoto hizo hapo juu, basi kimbia hospitalini kuangalia kama umekufa au uko hai.
Kama unabisha, andamana.