Changamoto ni sehemu ya maisha, bila changamoto hakuna radha ya maisha

passion_amo1

JF-Expert Member
Dec 3, 2023
1,578
3,148
Wakuu habari za uzima?

Najua wengi tulishapitia katika hali fulani kwenye maisha tukaona kwamba hatuwezi kuendelea na hapo ndio mwisho wetu.

Watu wengi wakiwa kwenye maumivu huwa wanachelewa kuchukua hatua muhimu za maisha. Unakuta sababu ya maumivu anakuwa ameganda na hafanyi chochote, yaani kila kitu kimesimama.

Wengine wanaamua kususia maono yao, wengine hawajipendi tena kwa sababu ya maumivu. Kwa taarifa, waliokusababishia maumivu wenyewe wanaendelea na maisha yao na wengine walishasahau walichokufanyia. Usiendelee kudumaa fungua ukurasa MPYA.

Kuna wakati unatamani Dunia yote ijue ambavyo umetendwa vibaya,umeonewa au namna ulivyoumizwa.unatamani ungeonewa huruma na kila mtu, kwa sababu hiyo utajikuta kila saa unapenda kuwasimulia watu mambo yako na maumivu unayopitia. Sio sababu unataka suluhisho Bali unatafuta kuonewa HURUMA.

Kumbuka, wengi utakaowasimulia watageuza stori na wengine watakuona haujielewi umechanganyikiwa, usiongee na kila mtu kipindi unapopitia nyakati ngumu katika maisha, ongea na wachache, tafuta UPONYAJI na usitafute HURUMA.

Usisahau kuna wakati ambao wale waliokusababishia maumivu ndio watakuwa wa kwanza kuwaelezea wengine maneno ya UONGO kuhusu wewe, wanafanya hivi waonekane wema.

Amua kutafuta UPONYAJI wa Hisia zako bila kujali kama wanajali au laah.

Ukisubiri wakujali kama unavyotaka utaendelea kuishi kwenye maumivu siku zote.
 
Back
Top Bottom