Nimepata mchumba kupitia JamiiForums

Nimepata mchumba kupitia JamiiForums

Dumelo

Senior Member
Joined
Apr 23, 2015
Posts
139
Reaction score
235
Naomba nitoe pongezi kwa uongozi wa JamiiForums kwa kuanzisha hii platform ya mahusiano. Niliwahi kutoa thread yangu hapa kuwa natafuta mchumba/ baadae awe mke wangu. Zilikuaja PM kibao lakini wengi hawakuwa serious, finally nilimpata aliyekuwa serious.

Ni zaidi ya mwezi sasa. Tuna mipango mingi. Ikifikia wakati wa ndoa nitawajulisha wadau.

Thanks Again JamiiForums.
======
Hongera sana Dumelo!
Hii Jamii Forum hata mimi ilinipatia mume mwema sana. Yani tupo kwenye ndoa zaidi ya miaka mitatu sasa na tumebarikiwa mtoto pia. Tunapendana na kuheshimiana sana. Ila ni muhimu kuwa na subira kwenye kutafuta na pia kumuomba sana Mungu akuongoze kwenye utafutaji wako.
 
Mc wa harusi nipo mkuu...naamini pia kadi utatoa kwa mashemeji wote wa MMU.
NB: Ni PM sio DM
 
So genuine, nikiyasoma maandishi yako naona kabisa inatoka moyoni na unamaanisha.

Kila la kheri mkuu.
 
Hongera sana Dumelo!
Hii JamiiForums hata mimi ilinipatia mume mwema sana. Yaani tupo kwenye ndoa zaidi ya miaka mitatu sasa na tumebarikiwa mtoto pia. Tunapendana na kuheshimiana sana. Ila ni muhimu kuwa na subira kwenye kutafuta na pia kumuomba sana Mungu akuongoze kwenye utafutaji wako.
 
kwanini pana mengi mkuu hahahahahahaaaaaaaaaaaaa


hujui kuwa hiii ndo jf chezea jf weweeeee hapa ni kitivo cha vichekesho na mauzauza ya kila namna
je nawe umepata jf au bado? (jokes)

Vijana nitawawezea wapi mimi....!!!??
Wasije wakanitengua kiuno bure....
 
Back
Top Bottom