Nimepata mchumba kupitia JamiiForums

Nimepata mchumba kupitia JamiiForums

Hongera sana Dumelo!
Hii Jamii Forum hata mimi ilinipatia mume mwema sana. Yani tupo kwenye ndoa zaidi ya miaka mitatu sasa na tumebarikiwa mtoto pia. Tunapendana na kuheshimiana sana. Ila ni muhim kuwa na subira kwenye kutafuta na pia kumuomba sana Mungu akuongoze kwenye utafutaji wako.
Hongera sana
 
Hongeren sana aisee kumbe kuna baadhi ya watu wapo serious
 
Watu wananiambiaga eti nalingana na ndoo mbili za maji...zikiwa zimeekwa juu juu....

Ingawa sina uhakika....

Jumapili hii nitaenda hospitali kupima.....nitakupa majibu..
hahahahaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa aiseee umeniacha hoi leo inabidi uanze maigizo ya vichekesho kwani naona unaelekea kama akina masanja mkandamizaji vile

halafu kwani haulingani na masanja au yeye kakupita kwenda juu
 
Watu wananiambiaga eti nalingana na ndoo mbili za maji...zikiwa zimeekwa juu juu....

Ingawa sina uhakika....

Jumapili hii nitaenda hospitali kupima.....nitakupa majibu..
jumapili huendi kusali au wewe sio wa jumapili
 
Hongera yako,kabla ya harusi msisahau kupima....( pressure )
 
ina maana unasali kila siku sasa muda wa kukaa hapa si unautumia vibaya maana kama kusali kila siku kwanini upo masaaa mengi hapa jf?

nasubiria hayo majibu toka kwa docta wako hiyo jpili
Mimi si wa jumapili....mimi wa kila siku....
 
ina maana unasali kila siku sasa muda wa kukaa hapa si unautumia vibaya maana kama kusali kila siku kwanini upo masaaa mengi hapa jf?

nasubiria hayo majibu toka kwa docta wako hiyo jpili

Mimi kwangu ibada ni kufanya jambo linalompendeza Mungu.....

Kwa maana hiyo kila nikifanya jambo la kumpendeza Mungu maana yake nipo kwenye ibada.....

Hata kukaa hapa kushauriana na watu maswala mbali mbali yanayohusu maisha yao....kuwapa tumaini watu waliopoteza matumaini.....kuwatia watu moyo kupitia magumu...pia ni ibada.....
 
Hongera sana

Shukran sana Shunie. Mapenzi hupatikana popote tu na wala hakuna sehemu maalum ya kutafutia mwenza iliyo bora kuliko nyingine. Cha msingi ni kuwa na nia ya dhati na wala si dhihaka.
 
really??? i thought r just jokes!!!

Hapana NO04 wala sio utani. Sina sababu ya kudanganya kwa kitu kama hiki. Kweli namshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa kunikutanisha nae na wala sifikirii vibaya kwamba wote tulikuwa tunatafuta wenza humu na ndio tukakutana. Hii ni sehemu tu kama vile sehemu nyingine ambayo unaweza kupata mwenza.
 
Shukran sana Shunie. Mapenzi hupatikana popote tu na wala hakuna sehemu maalum ya kutafutia mwenza iliyo bora kuliko nyingine. Cha msingi ni kuwa na nia ya dhati na wala si dhihaka.
Usijekuwa ww ndo mke wangu maana hata mm mke wangu kwa mara ya kwanza nilikutana naye mtandaoni mwaka 2009 kama sikosei. Ila mtandao sio jf wala fb. Pia toka tumefunga ndoa ni miaka mitatu na tuna mtoto mmoja. Mke wangu ni mtu mwema sana pia. Sisi ilianza urafiki wa muda mrefu kabla ya kwenda kwenye uchumba ilichukua zaidi ya mwaka just as friends. Binafsi naamini Mke au mume waweza kutana nae popote pale. Kikubwa muombe mwenyezi MUNGU na mtegemee yeye tu.
 
Usijekuwa ww ndo mke wangu maana hata mm mke wangu kwa mara ya kwanza nilikutana naye mtandaoni mwaka 2009 kama sikosei. Ila mtandao sio jf wala fb. Pia toka tumefunga ndoa ni miaka mitati na tuna mtoto mmoja. Mke wangu ni mtu mwema sana pia. Ss ilianza urafiki wa muda mrefu kabla ya kwenfa kwenye uchumba ilichukua zaidi ya mwaka just as friends

Hahaha Tarakilishi umenifurahisha sana. Yani unataka kujua kama mimi ndio mkeo? Hapana bwana. Mimi ID ya mumewangu naijua sio hii yako. Na pia maelezo yako sio kama vile mimi na yeye tulivyofahamiana. Sisi tulichukua miezi kumi toka tufahamiane hapa JF mpaka kufunga ndoa.

Shukran pia kwa kuchangia chanya hoja hii!
 
Hahah Poa Nareem. Just coincidence. Ndio maana nikasema mm na mke wangu hatukukutana JF. Tulikutana mtandao unaitwa The Grid ulikuwa unamilikiwa na voda enzi hizoooo. Sisi ilichukua miaka mitatu tangu kukutana kwa mara ya kwanza hadi kuoana. Tuna miaka mitatu ya ndoa lkn tuna miaka kama saba hivi tangu kukutana kwa mara ya kwanza.

Kwa ujumla lengo ni kuwashuhudia wenzetu kuwa mwenza waweza kutana naye popote pale maana kuna watu hawaamini kama waweza pata mke au mume kwa njia hii.

Nashuhudia uaminifu pia, mm tangu nikutane naye sijawahi kuwa na mahusiano yoyote na wala sitarajii. Naamini mke wangu ni muaminifu pia. So jf watu wema wapo na wabaya pia wapo. Mtandao ni ulimwengu mwingine kuna wezi, majambazi, wauaji, wapole, malaya nk. Be careful.
 
Nimekuelewa Tarakilishi kwa maelezo yako yenye busara.
Ukweli kuna watu hawaamini kama mitandao ya kijamii inaweza kuwapa wenza wema wa maisha yao. Lakini pia hata huko wanakokuzungumzia kuwa ni salama kupata mwenza, bado watu hukutana na changamoto nyingi sana. Kwa mimi naamini Mungu wetu pekee ndio anaweza kutuongoza vyema katika hili maana kwa akili na utashi wetu pekee ni rahisi sana kukosea na haijalishi kama ni kwenye mtandao wa kijamii au kanisani/msikitini.
 
Bado yule bibi anaetafta mume wa 50yrs aliefiwa mke nae aje atupe Mlejesho hahahaha aiseee
 
Back
Top Bottom