Nimeombwa kuwa "Husband for hire"

Nimeombwa kuwa "Husband for hire"

Hata hivyo nasikia siku hizi kigezo cha ndoa hakikubaliki sana utaambiwa chagua moja kati ya ndoa na kazi
 
Una wendawazimu mwanamke?
Kimbia ufe wallah
Ana mume wake afunge nae.
ila kama unampenda funga nae kwa maana yeye yupo mbali kiakili kuliko wewe na kashajua njia ya kukupata ndo hiyo
 
Hapana The Boss

Huyu rafiki angu nilimwonea huruma sana alivyopangiwa huko Tabora ndanindani.

Hatuna feelings kabisa.

The easy way kutoka huko ndo hyo suggestion.

Original certificate nitakaa nayo yeye nitampa copy, akishahamishiwa dar naichana na kila mtu anaendelea na maisha yake,
Angalia msimamo uwe huo huo ukigusa kidogo ndoa inakuwa halali.
 
Mdau usikubali, huo mchezo sio kabisa, kwani moyo wa mtu kichaka unaweza kumsaidia kwa nia njema ila baadaye ikala kwako. Kuna mdada aliomba msaada kama huo kwa jamaa,dili likatiki ila bahati mbaya miaka 2 baadae mdada akafariki,jamaa alijitokeza kama mume wa ndoa na kudai mirathi ya mkewe,wazazi na ndugu walibaki midomo wazi! So take care. Atafute cheti feki,mbona vinapatikana kirahisi.
 
Mimi nadhani hapo ni kwamba dada ataondoka kijijini kwa kigezo cha kuenda kwa mumewe (mleta uzi). Ndivyo nilivyomuelewa mimi

Kwa mujibu wa mleta uzi,huyu dada ana mume!Na mume pamoja na mleta uzi wanakaa wote Dar anakotaka kuhamishiwa bi dada
 
Hapana The Boss

Huyu rafiki angu nilimwonea huruma sana alivyopangiwa huko Tabora ndanindani.

Hatuna feelings kabisa.

The easy way kutoka huko ndo hyo suggestion.

Original certificate nitakaa nayo yeye nitampa copy, akishahamishiwa dar naichana na kila mtu anaendelea na maisha yake,

Kuchana original siyo solution, nakala itabaki bomani, akiamua kukufix atakufix tu. Atasema wewe ni mumewe, vyeti vilipotea/kuibiwa n.k. ushahidi uko bomani. Akifungua kesi, mtu wa bomani atakuja kuthibitisha hiyo ndoa mahakamani, think before you leap
 
Habari zenu wakuu.

Nina rafiki angu (sio mpenzi, just a friend) mwalimu amepangiwa mkoani halafu porini sana.

Leo kaniomba twende tukafunge ndoa za bomani ili apate cheti akaombe transfer arudishwe Dar (kwa mume wake).

Akishahamishiwa Dar ndoa yetu inavunjika kila mtu na maisha yake.

Naombeni msaada wa kunieleza ndoa za bomani zinakuwaje.

Shukrani kwa msaada.

Uhamisho siyo kitu rahisi rahisi namna hiyo...........

ningeweza kutoa ushauri hapa , lakini ushauri wenyewe ni wa kuvunja vunja sheria na utaratibu kiasi kwamba siyo vyema kuuweka hapa.........
 
Jaman kuna vitu vya kufoji lakin katka hili mbona naona ukungu machoni jaman
 
Amesema anataka mme dar, c tayari ana cheti cha ndoa? Kwann asikipeleke? Na kama bado walikua hawajafunga ndoa kwann asiende na huyo mme wake wakafunge ndoa bomani? Je ww unaetaka kumsaidia umeshaoa? Au una mchumba? Kama unae utamwambiaje? Jibu hayo maswali ili nikusaidie vizuri
 
Ukigeukwa utakuwa mume wa ukweli bila ubishi
Nafikiri ushauri ulitolewa na wadau ni wa manufaa. "at your own risk" ukipenda.
 
Uhamisho siyo kitu rahisi rahisi namna hiyo...........

ningeweza kutoa ushauri hapa , lakini ushauri wenyewe ni wa kuvunja vunja sheria na utaratibu kiasi kwamba siyo vyema kuuweka hapa.........

weka mzee nimasaidie best angu. Nipo serious
 
Kuchana original siyo solution, nakala itabaki bomani, akiamua kukufix atakufix tu. Atasema wewe ni mumewe, vyeti vilipotea/kuibiwa n.k. ushahidi uko bomani. Akifungua kesi, mtu wa bomani atakuja kuthibitisha hiyo ndoa mahakamani, think before you leap

Asante kwa ushauri. Naamini hatofanya hivyo.

Naomba niambie process za kwenda bomani
 
Habari zenu wakuu.

Nina rafiki angu (sio mpenzi, just a friend) mwalimu amepangiwa mkoani halafu porini sana.

Leo kaniomba twende tukafunge ndoa za bomani ili apate cheti akaombe transfer arudishwe Dar (kwa mume wake).

Akishahamishiwa Dar ndoa yetu inavunjika kila mtu na maisha yake.

Naombeni msaada wa kunieleza ndoa za bomani zinakuwaje.

Shukrani kwa msaada.
Inawezekana,ila ni risk kwa huyo mdada,maana akiishapata mwenzi akagundua aliwahi kufunga ndoa italeta shida.
Pia na kwako kama hujaoa na huyo bi-dada anakumezea mate,maana ukiamua kuoa anaweza kukuwekea zengwe na akatoa uthibitisho wa cheti cha ndoa yenu.Ni vigumu kisheria kueleza kuwa mlifanya deal ili kumfanya aamishiwe dar kikazi,hii itakusababishia kufungwa jera.
Fikiria mara mbili kabla ya kuchukua uamzi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom